Elimu ya form four iongezwe masomo zaidi, kuna maprofesa hawajui umuhumu wa kusoma topic electrolysis na electroless

Duhu hadi wewe?
Sikubaliani na wewe. Maana kujua mambo mengi tu theoretically ni afadhali ufahamu mambo machache ambayo unaweza kuyafanyia kazi. Najua kuna watu wengi wamesoma wanajua electrolysis ni nini lakini hawawezi kuifanyia kazi ila wapi uwanja wa kutoa maelezo sasa.
Kwani wewe mkuu mfano ukiumwa si utaenda kwa daktari akutibu kwa sababu ni field yake. Mimi naungana na profesa, watoto wasome vitu vichache ambavyo wataweza kuvijua kwa undani na kuvifanyia kazi. Hapo utapata mtu anajua sheria kweli kweli, huyu ni daktari kweli kweli, huyu ni mhandisi wa barabara anajua kwelikweli sio kuwa na jack of many trades master of none.
Hapa unakutana na jamaa anakwambia anajua karibu programming language 10 lakini mwambie akuundie kitu, hawezi anajua tu kueleza.
 
Serious kabisa sikupingi, anaweza akawa sawa katika alichozungumza ila pia kuboresha hata hao waleta hiyo elimu sasa unafundishwa machine mfano tu muhusika hata hiyo machine hajui.
Haijui hata hiyo machine ko mm naona kwenye elim Kuna utata kidogo kutokana na mazingira yetu mfano mzuli Tanzania tuna watu 60milions lakin hayupo anaeweza hata kutengeneza kipuli hata kimoja wapo Cha kweny Gali, Saa,, computer n.k kwel ama Kuna shida gan
 
Inawezekana kuna vitu vina umuhimu mkubwa ila kwa ufundishaji wa Tz unafanya vionekana havina maana kwani zimebase katika kukariri na sio uelewa na kumjenga mwanafunzi.Kuna vitu vya O_level nilikariri nilijua umuhimu wake baada ya kusoma vitabu vya mitaala ya nje nikakuta wameeleza vizuri sana kwa namna bora ya kumjenga mwanafunzi .

Kingine ni mazingira mabovu ya ufundishaji vitu vya kusomea maabara vinasomwa kama theories,hata ikitokea kuenda maabara idadi ya vifaa inakuwa vichache kuhimili idadi ya wanafunzi.Mimi shule nilizopitia asilimia kubwa ya vitu vya maabara tumesoma kea kukariri kama theories isipokuwa vile ambavyo vinatoka kwenye mtihani maalaumu ya practical hapo tulienda Lab.
Ujue nilisoma chuo kimoja topic Moja ila Kuna vitabu rahisi na vitabu vigumu kwenye topic Moja hiyo hiyo. Hata biblia ipo rahisi na ngumu
 
Nichangamoto kabisa yaani Mimi nisingesoma na ngozi nyeupe ningekuwa kilaza mwelevu
Jamaa wako mbali sana katika ufundishaji, nilicheki pia wajapan katika documentary moja hivi madogo ni kama darasa la 4 tu wanapiga tayari internal combustion engine na darasani zipo kama mifano katika science, hapo bado computer, japanese language, mathematics.

Wakitoka hapo michezo lazima uwe na mchezo wowote ule.

Baadae stadi za maisha kushona, useremala n.k nilifurahi sana.
 
Haijui hata hiyo machine ko mm naona kwenye elim Kuna utata kidogo kutokana na mazingira yetu mfano mzuli Tanzania tuna watu 60milions lakin hayupo anaeweza hata kutengeneza kipuli hata kimoja wapo Cha kweny Gali, Saa,, computer n.k kwel ama Kuna shida gan
Hahahahaha field ya electronics ni ya moto mno kutengeneza hizo printed circuit board na electronics components nyingine siyo swala dogo.

Walau niliwahi kuona TATC maarufu kama nyumbu walitengeneza gear za gear box na mengineyo pia.
 
Nimekutana na professor mmoja mbobezi katika kuplactise na kufundisha sheria shule kuu ya sheria chuo kikuu Dar es salaam katika hotel Moja hapa Kariakoo.

Ghafla tulifikia mada ya ubora wa elimu Tanzania. Nikamwambia watoto wanamaliza wapo weupe na mbaya zaidi hawajui hata haki zao. Akaniambia chanzo ni watoto wanasoma vitu vingi sana wapunguziwe. Mimi nikamwambia wanasoma vitu vichache sana anamaliza wanajua kusoma na kuandika.

Ghafla akarukia kuwa yeye Haoni umuhimu wa electrolysis. Nikamuuliza una Gari? Nikamwambia unayo miaka mingapi akaniambia huu ni mwaka wa tano. Nikawambia bila electrolysis itadumu mwa mmoja tu.

Nikamuuliza una saa hapo akasema ndio. Ugejisikiaje kuvaa mabati yenye kutu?
Akashangaa akaniuliza umesoma Tanzania? Nikamwambia ndio sijawahi kukutana na mtanzania mwenye uwezo kama wako.

Akaniuliza nini kifanyike nikamwambia form ndio elimu pekee mwanafunzi anatakiwa kutawala mazingira yake. Baada ya hapo anajiandaa na professionals. Akakubaliana na Mimi kuwa masomo yaongezwe halafu wanafunzi wasichague masoma ili wapate muongozo wa ulewa wa mambo ya nayo wazunguka.
Hoja ya professa ameshindwa kuitetea lakini ina mashiko,hivi huyo ni profesa kweli mbona ni mweupe sana ?

Inshu ya msingi ni kwamba tunajazwa taarifa ambazo hazina umuhimu kwetu,tunajazwa taarifa ambazo tayari ni idea za watu na wala hazina msaada kwenye maisha yetu ya kila siku.

Sasa kama mtu ambaye hajapita hata form four anamiliki gari zaidi ya miaka mi5 na hajui electrolysis maana yake electrolysis ni ile inayofanyika kwenye gari.

Kusoma kwetu electrolysis ama kutokusoma hakutofanya gari isiendelee kudumu,mtu ukifuata miongozo sahihi ya kutunza gari gari itadumu hata kama huju what is electrolysis.

Ni sawa na kusema bila photosynthesis tusingepanda mahindi.

Sasa hata kama hatujasoma biology hatujui photosynthesis kwani mahindi au mimea haitoota ?

Kwa hiyo tunapewa elimu ambazo tunaishia kujua waliyovumbua watu,na wala elimu hiyo haiwi muongozo wa kutufanya sisi tuvumbue ya kwetu.

Hivyo HOJA YA PROFESA IKO NA MASHIKO.
 
Jamaa wako mbali sana katika ufundishaji, nilicheki pia wajapan katika documentary moja hivi madogo ni kama darasa la 4 tu wanapiga tayari internal combustion engine na darasani zipo kama mifano katika science, hapo bado computer, japanese language, mathematics.

Wakitoka hapo michezo lazima uwe na mchezo wowote ule.

Baadae stadi za maisha kushona, useremala n.k nilifurahi sana.
Kabisa Yan watu wako vizuli sana mm naona tusilaum sana mfumo wetu kielem Bado sana ila Kwa upande mwingne mm naona kama ni uzembe flan hiv unafanyika
 
Hahahahaha field ya electronics ni ya moto mno kutengeneza hizo printed circuit board na electronics components nyingine siyo swala dogo.

Walau niliwahi kuona TATC maarufu kama nyumbu walitengeneza gear za gear box na mengineyo pia.
Kabisa si swala dogo ko ww unasaje elimu yetu iwe hvyohvyo ama tutumie njia gan watu wajifunze na kuelew Zaid maana haya masomo weng wao wanayakwepa,,
 
Hoja ya professa ameshindwa kuitetea lakini ina mashiko,hivi huyo ni profesa kweli mbona ni mweupe sana ?

Inshu ya msingi ni kwamba tunajazwa taarifa ambazo hazina umuhimu kwetu,tunajazwa taarifa ambazo tayari ni idea za watu na wala hazina msaada kwenye maisha yetu ya kila siku.

Sasa kama mtu ambaye hajapita hata form four anamiliki gari zaidi ya miaka mi5 na hajui electrolysis maana yake electrolysis ni ile inayofanyika kwenye gari.

Kusoma kwetu electrolysis ama kutokusoma hakutofanya gari isiendelee kudumu,mtu ukifuata miongozo sahihi ya kutunza gari gari itadumu hata kama huju what is electrolysis.

Ni sawa na kusema bila photosynthesis tusingepanda mahindi.

Sasa hata kama hatujasoma biology hatujui photosynthesis kwani mahindi au mimea haitoota ?

Kwa hiyo tunapewa elimu ambazo tunaishia kujua waliyovumbua watu,na wala elimu hiyo haiwi muongozo wa kutufanya sisi tuvumbue ya kwetu.

Hivyo HOJA YA PROFESA IKO NA MASHIKO.
Ahahaha ndugu umeongea kitu nmekuelew sana
 
Msomi tulia uandike vizuri.
Kujua theory nyingi hakufanyi elimu kuwa bora mkuu
 
Kabisa Yan watu wako vizuli sana mm naona tusilaum sana mfumo wetu kielem Bado sana ila Kwa upande mwingne mm naona kama ni uzembe flan hiv unafanyika
Huo ndiyo uhalisia naamini hatujawa serious kuvuka hapa panapotushinda.
Naomba nikupe mfano mdogo japo si ubaya angalia TAZARA wale reli yao imejengwa miaka ya 70 ila ilikuwa na baadhi na technology ambazo ni very advanced kwa wakati wake.

Leo 2023 kaangalie utagundua sisi tupo wapi. Tunahitaji kuwekeza katika rasilimali WATU, FEDHA na MUDA.

Hii elimu haitakuwa wimbo tena.
 
Kabisa si swala dogo ko ww unasaje elimu yetu iwe hvyohvyo ama tutumie njia gan watu wajifunze na kuelew Zaid maana haya masomo weng wao wanayakwepa,,
Je ni kweli taasisi zetu za elimu na wadau wapo serious kututoa huku? Niliwahi kubahatika kufundishwa na watu wa USA pia India technology fulani fulani kwa vipindi tofauti kabisa.

The way ninavyohoji na kuelezea kile ambacho na mimi na share nao waliwaambia wakuu wetu mbona mnatuita sisi na wataalamu mnao.

Nadhani bado hatujawa tayari kutoka huku, unaweza shauri jambo muhusika atakuja kuhoji kwani ana elimu gani?

Fuatilia documentary za elimu za awali na msingi kwa nchi kama Germany, Japan, U.K au ushafatilia kipindi cha Child Genius UK huwa nafatilia sana hilo shindano Discovery family channel mtoto wa miaka 12 periodic table lote humdanganyi.

HATUPO SERIOUS
 
Ko inamaana kwamba wataalam tunao lakin maZingila na uhitaji ama juhudi za kupambania kile kitu ndo duni,, na pia wataalam tunawez kuwa nao wakadumaa kutokana na maZingila ya ufundishaj yalivyo Kwa nchi yetu
 
"na pia wataalam tunawez kuwa nao wakadumaa kutokana na mazingira ya ufundishaji yalivyo Kwa nchi yetu"

Nimekunukuu na ndiyo JIBU, fikiria kiongozi wako unamwambia lete hiki na hiki mambo yatafanyika anaona huna maana anachukua wataalamu kutoka kiwandani wanakuja baada ya ushirikiano wa siku kadhaa wanamwambia hatuoni haja ya sisi kuwepo hapa experts wapo.

Wenzetu hawana longolongo hasa wanaotoka Europe.
 
Hoja ya professa ameshindwa kuitetea lakini ina mashiko,hivi huyo ni profesa kweli mbona ni mweupe sana ?

Inshu ya msingi ni kwamba tunajazwa taarifa ambazo hazina umuhimu kwetu,tunajazwa taarifa ambazo tayari ni idea za watu na wala hazina msaada kwenye maisha yetu ya kila siku.

Sasa kama mtu ambaye hajapita hata form four anamiliki gari zaidi ya miaka mi5 na hajui electrolysis maana yake electrolysis ni ile inayofanyika kwenye gari.

Kusoma kwetu electrolysis ama kutokusoma hakutofanya gari isiendelee kudumu,mtu ukifuata miongozo sahihi ya kutunza gari gari itadumu hata kama huju what is electrolysis.

Ni sawa na kusema bila photosynthesis tusingepanda mahindi.

Sasa hata kama hatujasoma biology hatujui photosynthesis kwani mahindi au mimea haitoota ?

Kwa hiyo tunapewa elimu ambazo tunaishia kujua waliyovumbua watu,na wala elimu hiyo haiwi muongozo wa kutufanya sisi tuvumbue ya kwetu.

Hivyo HOJA YA PROFESA IKO NA MASHIKO.
Nadhani kitu ambacho hujui elimu ya inakusaidia kutawala Maisha yako. Kama huna uelewa wa vitu ndio maana labda umasikini. Mfano electrolysis ni biashara tayari kabisa ukiwa na uelewa wa electrolysis utafanya printing na kuongeza Tija kwenye bidhaa zako. Sasa ujaza asali kwenye dumu buvubuvu nani atanunua. Hata wewe kutokuelewa electrolysis kwa undani kumekuongezea umasikini. Sasa hivi ungeweka kifungashia cha zinc oxide kwenye chupa yako. Nakuuza kwa bei mbaya kutokana na mwonekano.
 
Haijui hata hiyo machine ko mm naona kwenye elim Kuna utata kidogo kutokana na mazingira yetu mfano mzuli Tanzania tuna watu 60milions lakin hayupo anaeweza hata kutengeneza kipuli hata kimoja wapo Cha kweny Gali, Saa,, computer n.k kwel ama Kuna shida gan
Vipuri vinatengenezwa Sema material ya sasa ni ghari sana. Ni bora kuagiza.
 
Ko inamaana kwamba wataalam tunao lakin maZingila na uhitaji ama juhudi za kupambania kile kitu ndo duni,, na pia wataalam tunawez kuwa nao wakadumaa kutokana na maZingila ya ufundishaj yalivyo Kwa nchi yetu
Ni kukatishwa tamaa na serikali labda waaalimu wametupwa huko TAMISEMI na Halimashauri.
 
Back
Top Bottom