KERO Elimu ya juu ya Sekondari (A-Level) ni elimu bure kweli au kwa makaratasi?

KERO Elimu ya juu ya Sekondari (A-Level) ni elimu bure kweli au kwa makaratasi?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

musa-shija

New Member
Joined
Jun 16, 2026
Posts
1
Reaction score
0
Ninaomba mamlaka husika zitafakari hali halisi ya elimu ya kidato cha tano na sita nchini. Serikali imekuwa ikisema elimu ni bure, lakini ukweli uliopo mashuleni ni tofauti kabisa hasa kwa watoto wa familia za wakulima na wenye kipato cha chini.

Mahitaji yanayotolewa wakati wa kuripoti shule yamekuwa mengi sana. Mzazi anatakiwa kutoa michango, sare nyingi, vifaa mbalimbali, fedha za tahadhari, kitambulisho, nembo, ream paper, vitabu na vitu vingine vingi kiasi kwamba mtoto wa mkulima anashindwa hata kuanza shule kwa wakati.

Swali la msingi ni hili:
Je, kweli mwanafunzi anatakiwa kuripoti na vitu vyote hivyo kwa pamoja ndipo apokelewe shule?

Kwa mazingira ya kawaida ya Mtanzania wa kijijini, mzazi anategemea mavuno ya msimu mmoja kusomesha familia nzima. Inakuwa maumivu makubwa mtoto kupata nafasi ya kujiunga A-Level lakini akose kusoma au achelewe kuripoti kwa sababu ya michango na mahitaji yasiyo rafiki kwa kipato cha wananchi wengi.

Tatizo sio wazazi kukataa kuchangia. Hapana. Lakini michango na mahitaji yanapaswa kuwa na uhalisia wa maisha ya wananchi. Vinginevyo “elimu bure” itaendelea kubaki ni maneno ya kisiasa huku watoto wa maskini wakizidi kuumia kimya kimya.

Mbaya zaidi, baadhi ya wanafunzi wanamaliza shule lakini wanazuiwa vyeti kutokana na madeni ya michango. Hii inaua morale ya vijana wengi waliopambana kusoma katika mazingira magumu.

Tunaomba:
  • Serikali iweke mwongozo unaoeleweka kuhusu mahitaji muhimu na yasiyo muhimu.
  • Shule zisilazimishe kila kitu kulipiwa mara moja wakati wa kuripoti.
  • Watoto wasinyimwe haki ya elimu au vyeti kwa sababu ya hali ngumu ya mzazi.
  • Mamlaka ziangalie upya tafsiri halisi ya “elimu bure” kwa A-Level.
Elimu ni haki, sio mzigo wa kuwavunja moyo watoto wa walalahoi.

Screenshot (956).png

Screenshot (957).png

Screenshot (958).png

Screenshot (959).png

Screenshot (960).png
 
Huo mchango wa uendeshaji wa shule ni wizi wa wazi kabsa, maana kwa lugha nyingne ni ada
 
Back
Top Bottom