SoC03 Elimu ya Kidato cha Tano na Sita iondolewe

SoC03 Elimu ya Kidato cha Tano na Sita iondolewe

Stories of Change - 2023 Competition

Mkoba wa Mama

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2021
Posts
208
Reaction score
91
Kulingana na utaratibu uliopo hivi sasa, mwanafunzi anapo hitimu elimu ya sekondari (kidato cha nne) na kufikisha alama zinazohitajika anaweza kuchaguliwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano na sita/kujiunga na vyuo vya kati (astashahada/stashahada)

1. Mwanafunzi atakayechaguliwa/kuchagua mwenyewe kujiunga na elimu ya kidato cha tano na sita, akihitimu kidato cha sita na kufikisha alama zinazohitajika, atajiunga na elimu ya chuo kikuu (shahada). Na ikitokea mwanafunzi amehitimu kidato cha sita na hajafikisha alama zinazohitajika ili ajiunge na elimu ya chuo kikuu, itambidi arudi nyuma atumie cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili aweze kutuma maombi ya kujiunga na elimu ya vyuo vya kati (astashahada/stashahada).
Kwa maana hiyo mwanafunzi huyo atakuwa amepoteza miaka miwili aliyosoma kidato cha tano na sita, lakini pia wazazi wanakuwa wameingia gharama pamoja na serikali kugharamia elimu kwa mda wa miaka miwili ambayo haina manufaa wala matokeo chanya kwa mwanafunzi mwenyewe, kwa wazazi na taifa kwa ujumla, kwa sababu mwanafunzi huyo anakuwa bado hana ujuzi katika fani yoyote ile utakao muwezesha yeye kuajiriwa ama kujiajiri.

2. Kwa mwanafunzi atakaye chaguliwa/kuchagua mwenyewe kujiunga na vyuo vya kati, atakapo hitimu anaweza kuchagua kuendelea na elimu ya chuo kikuu/kuajiriwa/kujiajiri mwenyewe kwa sababu tayari anakuwa na ujuzi na maarifa ya kutosha kulingana na fani aliyosoma.

Napendekeza kuondolewa kwa elimu ya kidato cha tano na sita kwa sababu, ni njia inayopoteza mda kwa wanafunzi na kuingiza gharama kubwa wazazi na serikali kugharamia elimu ambayo mwisho wa siku mwanafunzi itambidi arudi tena kutumia cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili kujiunga na vyuo vya kati.

Sasa kwa nini mwanafunzi huyu asitumie cheti cha elimu ya sekondari mara tu anapohitimu kidato cha nne na kujiunga moja kwa moja na elimu ya vyuo vya kati kulingana na masomo aliyofaulu au fani atakayo ichagua yeye.

Nitoe mfano mmoja hapa:
Unatakiwa kufika kituo D (elimu ya juu/maisha ya kujiajiri/ kuajiriwa) ukitokea kituo C (kidato cha nne), kuna njia mbili za kukuwezesha kufika kituo D, ambazo ni elimu ya kidato cha tano na sita (njia A) au vyuo vya kati (njia B).

Njia A ni fupi (miaka miwili ya kidato cha tano na sita) lakini inakatiza mtoni, na njia B ni ndefu (miaka mitatu ya stashahada) lakini haikatizi mtoni.

Endapo utaenda na njia A unakuwa hauna uhakika wa moja kwa moja wa kufika kituo D maana kuna uwezekano ukakuta mto umefurika maji na usiweze kuvuka, kwa hiyo itakulazimu urudi tena nyuma uanze safari upya kwa kutumia njia B ambayo haikatizi mtoni ili ikufikishe kituo D.

Ikitokea hivyo, unakua umetumia jumla ya miaka mitano kwa safari ambayo kama ungelichagua njia B tangu mwanzo ingelikugharimu mda wa miaka mitatu tu kufika kituo D.

Mfano huu namaanisha nini:
Elimu ya kidato cha tano na sita mwanafunzi anapohitimu na kushindwa kufikisha alama za kumuwezesha kujiunga na elimu ya chuo kikuu, itamlazimu arudi tena nyuma kutumia cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili aombe kujiunga na elimu ya vyuo vya kati (astashahada/stashahada).

Lakini mwanafunzi aliyehitimu elimu ya vyuo vya kati, tayari anakuwa na ujuzi wa kutosha kumuwezesha yeye kujiajiri/kuajiriwa mahali popote kulingana na fani aliyoisoma na anakuwa na uwezo wa kuendelea na elimu ya juu kama atahitaji kufanya hivyo.

Elimu ya vyuo vya kati inatolewa kwa kiasi kikubwa ikijikita katika ujuzi na kwa vitendo kwa sababu wanafunzi wanaenda kufanya mafunzo kwa vitendo na wakiwa huko wanasimamiwa na kukaguliwa ni tofauti na elimu ya kidato cha tano na sita ambapo wanafunzi wanatumia mda mwingi kukaa darasani kukariri masomo ya nadharia na hata wakiingia maabara, majaribio wanayoyafanya hayana uhalisia kwa asilimia 100 na maisha watakayo kutana nayo baada ya shule aidha ni katika kujiajiri/kuajiriwa.

Elimu ya kidato cha tano na sita kwa sasa haina umuhimu kwa nchi yetu, ni lazima tuchague njia moja iliyo bora zaidi, maana mtu anahitimu kidato cha sita akiwa hana ujuzi wowote ule tofauti na elimu ya vyuo vya kati, ni kwa nini serikali iendelee kuingia gharama kugharamia suala ambalo tunaweza kuachana nalo na kujikita katika njia moja na gharama hizo zote kuelekezwa katika kuboresha mazingira na miundombinu (hasa katika suala la teknolojia) ya kujifunzia na kufundishia katika vyuo vya kati ili viwe bora zaidi na vizalishe wataalamu mahili wenye ujuzi na ubora unaohitajika.

Ni maarifa gani/ujuzi gani wa ziada anaoupata mwanafunzi aliyepita elimu ya kidato cha tano na sita utakao msaidia yeye katika ulimwengu wa sasa. Ama ni kitu gani cha ziada chenye manufaa watakikosa wanafunzi iwapo elimu ya kidato cha tano na sita itaondolewa na kubakia na elimu ya vyuo vya kati tu.

Naomba wadau, wizara ya elimu na serikali kwa ujumla ilitazame suala hili, tusiendelee kuwa na mifumo ya elimu kwa sababu ilikuwepo tangu mwanzo, kwa sasa inatakiwa tutazame zaidi mabadiliko yaliyopo, ulimwengu umekuwa wa sayansi na teknolojia na unahitaji watu wenye ujuzi zaidi (ili kuwawezesha aidha kujiajiri ama kuwa na sifa za kuajiriwa na kuwa wabunifu zaidi katika nyanja mbalimbali) kitu ambacho elimu ya kidato cha tano na sita haiwezi kutupatia jibu la suala hilo, zaidi ya wanafunzi kukariri vitu ili waje wajibu mitihani wafaulu, tofauti na elimu ya vyuo vya kati, ambapo mwanafunzi anapata mda wa kutosha wa kufanya mafunzo kwa vitendo na tena katika uhalisia, hivyo kumuwezesha kuwa na maarifa, ujuzi wa kutosha, uwezo mkubwa wa ubunifu na utatuzi wa changamoto zinazoikabili dunia katika fani aliyoisomea.

Hivyo itumike elimu ya vyuo vya kati mara tu mwanafunzi anapohitimu kidato cha nne. Hii itasaidia vijana wengi kuwa na ujuzi mapema zaidi na kuwa wabunifu na wenye uwezo mkubwa wa kujiajiri na sio kutegemea kuajiriwa tu.

Serikali iweke utaratibu maalum mwanafunzi anapohitimu kidato cha nne aangaliwe ni masomo gani alikuwa akifanya vizuri zaidi tangu mwanzo na sio mtihani wa mwisho tu, ili aende kusomea fani inayoendana na masomo hayo, au mwanafunzi achague mwenyewe fani anayoona anaimudu na anauwezo wa kuisoma na baadae kuwa na ujuzi wa kutosha katika fani hiyo.

Ahsanteni.
 
Upvote 43
Je content ambayo anaipata mwanafunzi wa kidato cha nne na sita je ni sawa? na impact yake kwa hao ipoje je wanakua sawa? ukiwaleta hapa je wanakua sawa?
Umezungumzia kufeli kwa kidato cha sita na kutofika chuo,unaona sio sawa, kwanin uone waliofeli kidato cha nne ni sawa
 
maneno mengi ila hapo kwenye kituo d ndio nimeishia kusoma....mimi ni mufaika wa elimu pasipo kupitia form 5 and six...walikuja watu wanatoka five na six huko wameangukia pua pcb eka pcm wakaja kupiga certificate ya uhasibu au procure.... ila hawakuwa na maajabu yoyote full sup!? kwa hio ni kuchoshana akili tu kwenda five na six
Why relying only on these who failed, what about these who made something out of it. This is what I call low thinking capacity.
 
Je content ambayo anaipata mwanafunzi wa kidato cha nne na sita je ni sawa? na impact yake kwa hao ipoje je wanakua sawa? ukiwaleta hapa je wanakua sawa?
Umezungumzia kufeli kwa kidato cha sita na kutofika chuo,unaona sio sawa, kwanin uone waliofeli kidato cha nne ni sawa
Your replies prove that you know nothing about Advanced level, neither do you know the scope and important of it , so sad unakuta mtu kama wewe upo kwenye sekta ya elimu hapa Tz.
 
kuna haja elimu ya msingi kuishia darasa la tano kisha dara la sita na saba kuwa form one two sekondari.kwenye mtaala mmoja wa mkondo.
sababu ukipeleka mtoto shule za internation mtoto akimaliza lasaba unakuta yale ya form one na two yote anayajua.

ili form 3,4,5,6 ziwe ndo sekondary waweze kwenda chuo
 
Your replies prove that you know nothing about Advanced level, neither do you know the scope and important of it , so sad unakuta mtu kama wewe upo kwenye sekta ya elimu hapa Tz.
Jibu hoja,suala hapo umejaji kufika chuo pekee lakini ujuzi hukujaji,ndio maana huyo wa form 4 anasoma diploma na huyu degree, tuongelee contentwise,
 
kuna haja elimu ya msingi kuishia darasa la tano kisha dara la sita na saba kuwa form one two sekondari.kwenye mtaala mmoja wa mkondo.
sababu ukipeleka mtoto shule za internation mtoto akimaliza lasaba unakuta yale ya form one na two yote anayajua.

ili form 3,4,5,6 ziwe ndo sekondary waweze kwenda chuo
Wanayajua Kwa sababu ni yale yale tu ila huyu aliyesoma kayumba anayaona mapya Kwa sababu ya kubadirika Kwa Lugha

Elimu ya nchi hii imekuwa na mzunguko mrefu Kwa sababu ya kutumia lugha ya kiswahili shule za msingi

Siku serikali itakapozinduka usingizini na kuanza kutumia lugha ya kingereza kuanzia shule za msingi mambo yote yatakaa sawa

Na Mimi binafsi sijaelewa Kwa nini serikali inalazimisha lugha ya kufundishia masomo ya shule za msingi yawe Kwa kiswahili

Hi nchi ngumu sana
 
Advance ikifutwa
masomo yake unayasoma wapi maana ukifika University hayapo unasoma Mambo tofauti wkt mwngn
Kuna ulazima wowote wa kusoma masomo ya kidato cha tano na sita?
Mfano: daktari ambaye hakusoma kidato cha tano na sita (alisoma stashahada na baadae shahada) kuna kitu chochote anapungukiwa kwenye taaluma yake kwa sababu hakusoma kidato cha tano na sita?
 
Mimi huwa nawaza kama muhitimu wa chuo aliyekaa mtaani miaka nane (8 years) toa ile mitatu ya masomo na hajafanikiwa kupata kazi ya kutumia elimu aliyoisotea huwa anajisikiaje linapokuja suala la kumpeleka mwanae hadi elimu ya juu?

Elimu ya darasani sasa hivi hasa kwa mtoto wa maskini haina inachomsaidia uangaliwe utaratibu wa kuwapa mafunzo mbalimbali vijana ili angalao wakitoka hapo four au six wawe na wepesi kujichanganya mitaani tofauti na sasa kukaa kusubiri matokeo ili waende vyuo,point yangu hapa ni kwamba wakati anaposubiri matokeo awe na msukumo wa kwenda kujaribu yale maarifa aliyofundishwa akiona yana-apply kwenye maisha yake anakomaa humo humo siyo kama sasa wanaenda chuo wote wanamaliza na vyeti wote then wanamwagwa mitaani wote kugombania goal ambalo limeshajazwa na ndugu wa mabosi
Wazo zuri sana, inatakiwa elimu ya sasa ijikite zaidi kwenye kuwapa ujuzi wanafunzi, na sio tu kuwakalisha darasani kukariri mambo ili waje wajibu mitihani na wafaulu.
 
Hivi ukitoa vyuo vya kati vya ufundi na mambo ya afya kuna kada gani nyingine mtu anaweza kusoma akitokea form four na akajiajiri?


Je asilimia ngapi ya Watanzania tumefikia kuwa na akili za kujiajiri kwa elimu tulizosomea?

Je elimu ya form four na vyuo vya kati inatosha kukidhi Tanzania tunayoenda nayo miaka 50 ijayo?

Mi nadhani Advance iwe option ila isiondolewe.
Sijazungumzia kujiajiri tu, nimezungumzia pia kuajiriwa na suala la kupata ujuzi na ubunifu mapema ili kuweza kutatua changamoto zilizopo.

Kada nyingi tu mtu anaweza kusoma ukitokea kidato cha nne; sheria, elimu, afya ya jamii na mazingira, utawala, biashara, siasa na diplomasia, mambo ya fedha n.k

Na suala la kujiajiri halitegemei tu akili au elimu uliyosomea, ni suala pana linalohusisha pia mazingira wezeshi, mitaji, ujuzi na ubunifu.

Elimu ya sekondari na vyuo vya kati inaweza kukidhi kwa sababu baada ya hapo unaweza kuendelea na elimu ya juu. Na hakuna kitu mtu atakikosa au atashindwa kukitekeleza kwenye taaluma yake eti kwa sababu hakusoma kidato cha tano na sita.
 
Je content ambayo anaipata mwanafunzi wa kidato cha nne na sita je ni sawa? na impact yake kwa hao ipoje je wanakua sawa? ukiwaleta hapa je wanakua sawa?
Umezungumzia kufeli kwa kidato cha sita na kutofika chuo,unaona sio sawa, kwanin uone waliofeli kidato cha nne ni sawa
Kwanza kabisa, sijasema walio feli kidato cha nne ni sawa.

Suala la pili, sijalinganisha kati ya elimu ya kidato cha nne na elimu ya kidato cha tano na sita, mimi nimezungumzia kati ya vyuo vya kati na kidato cha 5&6

Kitu kingine umeuliza kuhusu contents za kidato cha tano na sita, mimi sioni kama ni hoja sana, maana chukulia mfano huu, daktari ambaye hakupita kidato cha tano na sita, alimaliza tu kidato cha nne kwenda kusoma stashahada na baadae shahada, je? daktari huyu katika kutimiza majukumu yake, kuna baadhi ya vitu hatoweza/hatokuwa na uwezo wa kuvifanya au hatoruhusiwa kufanya kwa sababu hakusoma kidato cha tano na sita? Jibu ni hapana. Kwa mfano huu chukulia vivyo hivyo na kwa kada nyingine.
 
Mimi naona isiondolewe nilipofika chuo ndo nimeona umuhimu wa advance
Umuhimu wake ni upi? Tueleze tafadhali, na kuna tofauti gani kati ya yule aliyepita kidato cha 5&6 na ambaye hakupita wakifika chuo kikuu?
 
Why relying only on these who failed, what about these who made something out of it. This is what I call low thinking capacity.
Leta hoja acha ku jaji uwezo wa kufikiri wa wengine, utafikiri wewe una kipimo cha kupima uwezo wa watu kufikiri, huu ni mjadala kila mtu anatoa maoni yake kadri anavyoelewa yeye.

Sasa unaanza je kumjadili mtu aliye faulu (maana huyo tayari amesha faulu na ataendelea na masomo), badala ya kupoteza mda kujadili waliofaulu hapa tunangalia kwa nini wengine wanafeli na je baada ya kufeli wanaenda wapi/wanafanya nini? Hiyo ndiyo hoja.
 
Njia zinapokuwa nyingi za kufikia Mafanikio ndo Safi

Kwa Elimu ya TANZANIA kusoma veta sio suluhisho la watu Kupata Ajira au kujiari ni watu wangapi wamesoma hizo hizo Diploma lakini Mambo bado 0-0

Tunabidi kuelewa kuwa hata Kama wewe ni mtoto wa masikini usiogope kusoma kwa kigezo Cha kukosa Ajira ,

Maana huku mtaani unahitaji kuwa na self-control ili kupiga hatua na sio viwango vya Elimu

Elimu ya A level au ya vyuo vya Kati bado sio mbadala wa kumsaidia mtoto wa masikini .
 
Back
Top Bottom