SoC03 Elimu ya Kidato cha Tano na Sita iondolewe

Stories of Change - 2023 Competition

Mkoba wa Mama

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2021
Posts
208
Reaction score
91
Kulingana na utaratibu uliopo hivi sasa, mwanafunzi anapo hitimu elimu ya sekondari (kidato cha nne) na kufikisha alama zinazohitajika anaweza kuchaguliwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano na sita/kujiunga na vyuo vya kati (astashahada/stashahada)

1. Mwanafunzi atakayechaguliwa/kuchagua mwenyewe kujiunga na elimu ya kidato cha tano na sita, akihitimu kidato cha sita na kufikisha alama zinazohitajika, atajiunga na elimu ya chuo kikuu (shahada). Na ikitokea mwanafunzi amehitimu kidato cha sita na hajafikisha alama zinazohitajika ili ajiunge na elimu ya chuo kikuu, itambidi arudi nyuma atumie cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili aweze kutuma maombi ya kujiunga na elimu ya vyuo vya kati (astashahada/stashahada).
Kwa maana hiyo mwanafunzi huyo atakuwa amepoteza miaka miwili aliyosoma kidato cha tano na sita, lakini pia wazazi wanakuwa wameingia gharama pamoja na serikali kugharamia elimu kwa mda wa miaka miwili ambayo haina manufaa wala matokeo chanya kwa mwanafunzi mwenyewe, kwa wazazi na taifa kwa ujumla, kwa sababu mwanafunzi huyo anakuwa bado hana ujuzi katika fani yoyote ile utakao muwezesha yeye kuajiriwa ama kujiajiri.

2. Kwa mwanafunzi atakaye chaguliwa/kuchagua mwenyewe kujiunga na vyuo vya kati, atakapo hitimu anaweza kuchagua kuendelea na elimu ya chuo kikuu/kuajiriwa/kujiajiri mwenyewe kwa sababu tayari anakuwa na ujuzi na maarifa ya kutosha kulingana na fani aliyosoma.

Napendekeza kuondolewa kwa elimu ya kidato cha tano na sita kwa sababu, ni njia inayopoteza mda kwa wanafunzi na kuingiza gharama kubwa wazazi na serikali kugharamia elimu ambayo mwisho wa siku mwanafunzi itambidi arudi tena kutumia cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili kujiunga na vyuo vya kati.

Sasa kwa nini mwanafunzi huyu asitumie cheti cha elimu ya sekondari mara tu anapohitimu kidato cha nne na kujiunga moja kwa moja na elimu ya vyuo vya kati kulingana na masomo aliyofaulu au fani atakayo ichagua yeye.

Nitoe mfano mmoja hapa:
Unatakiwa kufika kituo D (elimu ya juu/maisha ya kujiajiri/ kuajiriwa) ukitokea kituo C (kidato cha nne), kuna njia mbili za kukuwezesha kufika kituo D, ambazo ni elimu ya kidato cha tano na sita (njia A) au vyuo vya kati (njia B).

Njia A ni fupi (miaka miwili ya kidato cha tano na sita) lakini inakatiza mtoni, na njia B ni ndefu (miaka mitatu ya stashahada) lakini haikatizi mtoni.

Endapo utaenda na njia A unakuwa hauna uhakika wa moja kwa moja wa kufika kituo D maana kuna uwezekano ukakuta mto umefurika maji na usiweze kuvuka, kwa hiyo itakulazimu urudi tena nyuma uanze safari upya kwa kutumia njia B ambayo haikatizi mtoni ili ikufikishe kituo D.

Ikitokea hivyo, unakua umetumia jumla ya miaka mitano kwa safari ambayo kama ungelichagua njia B tangu mwanzo ingelikugharimu mda wa miaka mitatu tu kufika kituo D.

Mfano huu namaanisha nini:
Elimu ya kidato cha tano na sita mwanafunzi anapohitimu na kushindwa kufikisha alama za kumuwezesha kujiunga na elimu ya chuo kikuu, itamlazimu arudi tena nyuma kutumia cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili aombe kujiunga na elimu ya vyuo vya kati (astashahada/stashahada).

Lakini mwanafunzi aliyehitimu elimu ya vyuo vya kati, tayari anakuwa na ujuzi wa kutosha kumuwezesha yeye kujiajiri/kuajiriwa mahali popote kulingana na fani aliyoisoma na anakuwa na uwezo wa kuendelea na elimu ya juu kama atahitaji kufanya hivyo.

Elimu ya vyuo vya kati inatolewa kwa kiasi kikubwa ikijikita katika ujuzi na kwa vitendo kwa sababu wanafunzi wanaenda kufanya mafunzo kwa vitendo na wakiwa huko wanasimamiwa na kukaguliwa ni tofauti na elimu ya kidato cha tano na sita ambapo wanafunzi wanatumia mda mwingi kukaa darasani kukariri masomo ya nadharia na hata wakiingia maabara, majaribio wanayoyafanya hayana uhalisia kwa asilimia 100 na maisha watakayo kutana nayo baada ya shule aidha ni katika kujiajiri/kuajiriwa.

Elimu ya kidato cha tano na sita kwa sasa haina umuhimu kwa nchi yetu, ni lazima tuchague njia moja iliyo bora zaidi, maana mtu anahitimu kidato cha sita akiwa hana ujuzi wowote ule tofauti na elimu ya vyuo vya kati, ni kwa nini serikali iendelee kuingia gharama kugharamia suala ambalo tunaweza kuachana nalo na kujikita katika njia moja na gharama hizo zote kuelekezwa katika kuboresha mazingira na miundombinu (hasa katika suala la teknolojia) ya kujifunzia na kufundishia katika vyuo vya kati ili viwe bora zaidi na vizalishe wataalamu mahili wenye ujuzi na ubora unaohitajika.

Ni maarifa gani/ujuzi gani wa ziada anaoupata mwanafunzi aliyepita elimu ya kidato cha tano na sita utakao msaidia yeye katika ulimwengu wa sasa. Ama ni kitu gani cha ziada chenye manufaa watakikosa wanafunzi iwapo elimu ya kidato cha tano na sita itaondolewa na kubakia na elimu ya vyuo vya kati tu.

Naomba wadau, wizara ya elimu na serikali kwa ujumla ilitazame suala hili, tusiendelee kuwa na mifumo ya elimu kwa sababu ilikuwepo tangu mwanzo, kwa sasa inatakiwa tutazame zaidi mabadiliko yaliyopo, ulimwengu umekuwa wa sayansi na teknolojia na unahitaji watu wenye ujuzi zaidi (ili kuwawezesha aidha kujiajiri ama kuwa na sifa za kuajiriwa na kuwa wabunifu zaidi katika nyanja mbalimbali) kitu ambacho elimu ya kidato cha tano na sita haiwezi kutupatia jibu la suala hilo, zaidi ya wanafunzi kukariri vitu ili waje wajibu mitihani wafaulu, tofauti na elimu ya vyuo vya kati, ambapo mwanafunzi anapata mda wa kutosha wa kufanya mafunzo kwa vitendo na tena katika uhalisia, hivyo kumuwezesha kuwa na maarifa, ujuzi wa kutosha, uwezo mkubwa wa ubunifu na utatuzi wa changamoto zinazoikabili dunia katika fani aliyoisomea.

Hivyo itumike elimu ya vyuo vya kati mara tu mwanafunzi anapohitimu kidato cha nne. Hii itasaidia vijana wengi kuwa na ujuzi mapema zaidi na kuwa wabunifu na wenye uwezo mkubwa wa kujiajiri na sio kutegemea kuajiriwa tu.

Serikali iweke utaratibu maalum mwanafunzi anapohitimu kidato cha nne aangaliwe ni masomo gani alikuwa akifanya vizuri zaidi tangu mwanzo na sio mtihani wa mwisho tu, ili aende kusomea fani inayoendana na masomo hayo, au mwanafunzi achague mwenyewe fani anayoona anaimudu na anauwezo wa kuisoma na baadae kuwa na ujuzi wa kutosha katika fani hiyo.

Ahsanteni.
 
Upvote 43
Umeshindwa kujiuliza kitu kimoja cha muhimu sana.

1. Lengo letu la elimu hasa ni nini? Elimu ya kidato cha tano na sita inasaidiaje kutimiza lengo hilo?

Ati, wewe utakuwa na amani kufanyiwa upasuaji na daktari ambaye hakupata misingi ya PCB kidato cha sita bali amekomea kidato cha 4 na akaenda sijui vyuo gani vya kati huko unavyovisema (sikumaliza kusoma andiko lako)? Utaweza kupata mhandisi mzuri ambaye hajasoma PCM?

Ni wapi huko ambako hakuna elimu ya Advance au sisi ndiyo tunataka kuwa wa kwanza?

Na muhimu zaidi, bandiko lako hili linasaidiaje kuleta uwajibikaji na uongozi bora ambacho ndicho kipaumbe kikubwa cha shindano la mwaka huu?
 
Advance ikifutwa
masomo yake unayasoma wapi maana ukifika University hayapo unasoma Mambo tofauti wkt mwngn
Na yenye kuhitaji foundations za advance..labda Kama anataka elimu ya advance tuishushe tuichanganye o level ili watoto maji Waite mma
 
Kwa hiyo unataka kumaanisha ambao hawajapitia A level, masomo ya chuo kikuu hawayawezi?
 
Umeshindwa kujiuliza kitu kimoja cha muhimu sana.

1. Lengo letu la elimu hasa ni nini? Elimu ya kidato cha tano na sita inasaidiaje kutimiza lengo hilo?

Ati, wewe utakuwa na amani kufanyiwa upasuaji na daktari ambaye hakupata misingi ya PCB kidato cha sita bali amekomea kidato cha 4 na akaenda sijui vyuo gani vya kati huko unavyovisema (sikumaliza kusoma andiko lako)? Utaweza kupata mhandisi mzuri ambaye hajasoma PCM?

Ni wapi huko ambako hakuna elimu ya Advance au sisi ndiyo tunataka kuwa wa kwanza?

Na muhimu zaidi, bandiko lako hili linasaidiaje kuleta uwajibikaji na uongozi bora ambacho ndicho kipaumbe kikubwa cha shindano la mwaka huu?
Kwa hiyo unataka kuniambia madaktari wote nchi hii wamepita A level? Hujui kama kuna madaktari wengi tu walimaliza kidato cha nne wakaenda vyuo na sahizi wengine ni madaktari bingwa. Kwa hiyo wewe ukienda hospital kutibiwa huwa unafika unauliza daktari gani amepita A level ndio huyo akutibu?
Na kuhusu wahandisi, hujui kwamba pale DIT na vyuo vingine wanatoa wahandisi bora ambao wengine hawakupita A level? Au hata hilo haufahamu?
 
Ninaomba unifahamishe lengo la elimu ya Tanzania tafadhali.
 
Kwa hiyo unataka kumaanisha ambao hawajapitia A level, masomo ya chuo kikuu hawayawezi?
Hujanielewa namaanisha kutoka form four ni ngumu kuunga moja kwa moja chuo kikuu
Labda Kama mseme tufute elimu ya kidato Cha sita halafu tulazimishane wote tukasome diploma baadae tuende degree
Ila Kama mnataka mtu akimaliza form four aunge degree basi tufumue mtaala wetu baadhi ya knowledge ya advance mtu asome olevel mf. Mathematics calculus isomwe olevel maana ndo msingi wa formulas nyingi zinazofundishwa vyuoni!
 
Kwa hiyo unataka kuniambia madaktari wote nchi hii wamepita A level? Hujui kama kuna madaktari wengi tu walimaliza kidato cha nne wakaenda vyuo na sahizi wengine ni madaktari bingwa. Kwa hiyo wewe ukienda hospital kutibiwa huwa unafika unauliza daktari gani amepita A level ndio huyo akutibu?
Na kuhusu wahandisi, hujui kwamba pale DIT na vyuo vingine wanatoa wahandisi bora ambao wengine hawakupita A level? Au hata hilo haufahamu?
Elimu ya advance ni muhimu kwa jinsi mtaala wetu ulivyo kwa Sasa ndo maana hata ukisoma clinical medicine ..ukitaka kujiendeleza MD unaanza upya na wale walotoka advance ...Sasa Nani kapoteza muda? Aliyepitia njia ya panya miaka minne kusoma clinical medicine au aliyesoma miaka miwili tu advance?
 
Hujanielewa namaanisha kutoka form four ni ngumu kuunga moja kwa moja chuo kikuu
Labda Kama mseme tufute elimu ya kidato Cha sita halafu tulazimishane wote tukasome diploma baadae tuende degree
Ila Kama mnataka mtu akimaliza form four aunge degree basi tufumue mtaala wetu baadhi ya knowledge ya advance mtu asome olevel mf. Mathematics calculus isomwe olevel maana ndo msingi wa formulas nyingi zinazofundishwa vyuoni!
Basi nahisi hatukuelewana tokea mwanzo, mimi nimemaanisha kuwa; elimu ya kidato cha tano na sita iondolewe, tubaki na vyuo vya kati (viboreshwe, uwekezaji mkubwa ufanyike hasa katika suala la teknolojia na miundombinu, ili vizalishe wataalamu wenye ujuzi na ubunifu mkubwa) baada ya hapo waendelee na chuo kikuu au kujiajiri na kuajiriwa.
 
Kwa hiyo unataka kuniambia madaktari wote nchi hii wamepita A level? Hujui kama kuna madaktari wengi tu walimaliza kidato cha nne wakaenda vyuo na sahizi wengine ni madaktari bingwa. Kwa hiyo wewe ukienda hospital kutibiwa huwa unafika unauliza daktari gani amepita A level ndio huyo akutibu?
Na kuhusu wahandisi, hujui kwamba pale DIT na vyuo vingine wanatoa wahandisi bora ambao wengine hawakupita A level? Au hata hilo haufahamu?
Nadhani hata sina haja ya kukujibu; maana hoja yako imejikita katika vighairi (exceptions) vya nje ya mfumo. Afadhali tu nikupigie kura halafu nijikalie kimya.....

Wanaotaka kwenda kwenye mfumo moja kwa moja kwa kupita kidato cha sita waachwe wapite. Wanaotaka kupita hizo njia za mzunguko nao wapite. Na sijui kama kuna nchi ambako hawana high school maana hapo ndipo mwanafunzi anakuwa anapevuka na anakata shauri nini cha kufanya maishani mwake.

Ningekuelewa sana kama hoja yako ingeegemea katika kuboresha mitaala ya high school ili iendane na dunia inakokwenda. Ndiko wenzetu wanachofanya huko (mf. Marekani) lakini kuiondoa high school na mitaala yetu hii ya hovyo tutakuwa tunazalisha wasomi wenye pengo kubwa zaidi wakilinganishwa na wenzao. Labda kama tuibane elimu yetu iwe na lengo moja tu la kutupatia watu wenye ujuzi wa chini na wa kati lakini katika dunia ya sasa na hasa tunakokwenda tunahitaji watu wa aina zote.

Elimu yetu ina matatizo mengi na high school ni sehemu ndogo tu. Na suluhisho siyo kuifuta bali kuiboresha!
 
Leta hoja acha ku jaji uwezo wa kufikiri wa wengine, utafikiri wewe una kipimo cha kupima uwezo wa watu kufikiri, huu ni mjadala kila mtu anatoa maoni yake kadri anavyoelewa yeye.

Sasa unaanza je kumjadili mtu aliye faulu (maana huyo tayari amesha faulu na ataendelea na masomo), badala ya kupoteza mda kujadili waliofaulu hapa tunangalia kwa nini wengine wanafeli na je baada ya kufeli wanaenda wapi/wanafanya nini? Hiyo ndiyo hoja.
I like your sense of humor, however what pissed me off is the fact that he jumped to a single conclusion that A'level studies are worthless and this is exactly definition of low thinking capacity, if it's not I don't know what else is?
 
Leta hoja acha ku jaji uwezo wa kufikiri wa wengine, utafikiri wewe una kipimo cha kupima uwezo wa watu kufikiri, huu ni mjadala kila mtu anatoa maoni yake kadri anavyoelewa yeye.

Sasa unaanza je kumjadili mtu aliye faulu (maana huyo tayari amesha faulu na ataendelea na masomo), badala ya kupoteza mda kujadili waliofaulu hapa tunangalia kwa nini wengine wanafeli na je baada ya kufeli wanaenda wapi/wanafanya nini? Hiyo ndiyo hoja.
Or do you also want to tell me "kwenda advance ni kuchoshana akili" like your fellow? What do you call this if it's not nonsense?
 
Kulingana na utaratibu uliopo hivi sasa, mwanafunzi anapo hitimu elimu ya sekondari (kidato cha nne) na kufikisha alama zinazohitajika anaweza kuchaguliwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano na sita/kujiunga na vyuo vya kati (astashahada/stashahada)

1. Mwanafunzi atakayechaguliwa/kuchagua mwenyewe kujiunga na elimu ya kidato cha tano na sita, akihitimu kidato cha sita na kufikisha alama zinazohitajika, atajiunga na elimu ya chuo kikuu (shahada). Na ikitokea mwanafunzi amehitimu kidato cha sita na hajafikisha alama zinazohitajika ili ajiunge na elimu ya chuo kikuu, itambidi arudi nyuma atumie cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili aweze kutuma maombi ya kujiunga na elimu ya vyuo vya kati (astashahada/stashahada).
Kwa maana hiyo mwanafunzi huyo atakuwa amepoteza miaka miwili aliyosoma kidato cha tano na sita, lakini pia wazazi wanakuwa wameingia gharama pamoja na serikali kugharamia elimu kwa mda wa miaka miwili ambayo haina manufaa wala matokeo chanya kwa mwanafunzi mwenyewe, kwa wazazi na taifa kwa ujumla, kwa sababu mwanafunzi huyo anakuwa bado hana ujuzi katika fani yoyote ile utakao muwezesha yeye kuajiriwa ama kujiajiri.

2. Kwa mwanafunzi atakaye chaguliwa/kuchagua mwenyewe kujiunga na vyuo vya kati, atakapo hitimu anaweza kuchagua kuendelea na elimu ya chuo kikuu/kuajiriwa/kujiajiri mwenyewe kwa sababu tayari anakuwa na ujuzi na maarifa ya kutosha kulingana na fani aliyosoma.

Napendekeza kuondolewa kwa elimu ya kidato cha tano na sita kwa sababu, ni njia inayopoteza mda kwa wanafunzi na kuingiza gharama kubwa wazazi na serikali kugharamia elimu ambayo mwisho wa siku mwanafunzi itambidi arudi tena kutumia cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili kujiunga na vyuo vya kati.

Sasa kwa nini mwanafunzi huyu asitumie cheti cha elimu ya sekondari mara tu anapohitimu kidato cha nne na kujiunga moja kwa moja na elimu ya vyuo vya kati kulingana na masomo aliyofaulu au fani atakayo ichagua yeye.

Nitoe mfano mmoja hapa:
Unatakiwa kufika kituo D (elimu ya juu/maisha ya kujiajiri/ kuajiriwa) ukitokea kituo C (kidato cha nne), kuna njia mbili za kukuwezesha kufika kituo D, ambazo ni elimu ya kidato cha tano na sita (njia A) au vyuo vya kati (njia B).

Njia A ni fupi (miaka miwili ya kidato cha tano na sita) lakini inakatiza mtoni, na njia B ni ndefu (miaka mitatu ya stashahada) lakini haikatizi mtoni.

Endapo utaenda na njia A unakuwa hauna uhakika wa moja kwa moja wa kufika kituo D maana kuna uwezekano ukakuta mto umefurika maji na usiweze kuvuka, kwa hiyo itakulazimu urudi tena nyuma uanze safari upya kwa kutumia njia B ambayo haikatizi mtoni ili ikufikishe kituo D.

Ikitokea hivyo, unakua umetumia jumla ya miaka mitano kwa safari ambayo kama ungelichagua njia B tangu mwanzo ingelikugharimu mda wa miaka mitatu tu kufika kituo D.

Mfano huu namaanisha nini:
Elimu ya kidato cha tano na sita mwanafunzi anapohitimu na kushindwa kufikisha alama za kumuwezesha kujiunga na elimu ya chuo kikuu, itamlazimu arudi tena nyuma kutumia cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili aombe kujiunga na elimu ya vyuo vya kati (astashahada/stashahada).

Lakini mwanafunzi aliyehitimu elimu ya vyuo vya kati, tayari anakuwa na ujuzi wa kutosha kumuwezesha yeye kujiajiri/kuajiriwa mahali popote kulingana na fani aliyoisoma na anakuwa na uwezo wa kuendelea na elimu ya juu kama atahitaji kufanya hivyo.

Elimu ya vyuo vya kati inatolewa kwa kiasi kikubwa ikijikita katika ujuzi na kwa vitendo kwa sababu wanafunzi wanaenda kufanya mafunzo kwa vitendo na wakiwa huko wanasimamiwa na kukaguliwa ni tofauti na elimu ya kidato cha tano na sita ambapo wanafunzi wanatumia mda mwingi kukaa darasani kukariri masomo ya nadharia na hata wakiingia maabara, majaribio wanayoyafanya hayana uhalisia kwa asilimia 100 na maisha watakayo kutana nayo baada ya shule aidha ni katika kujiajiri/kuajiriwa.

Elimu ya kidato cha tano na sita kwa sasa haina umuhimu kwa nchi yetu, ni lazima tuchague njia moja iliyo bora zaidi, maana mtu anahitimu kidato cha sita akiwa hana ujuzi wowote ule tofauti na elimu ya vyuo vya kati, ni kwa nini serikali iendelee kuingia gharama kugharamia suala ambalo tunaweza kuachana nalo na kujikita katika njia moja na gharama hizo zote kuelekezwa katika kuboresha mazingira na miundombinu (hasa katika suala la teknolojia) ya kujifunzia na kufundishia katika vyuo vya kati ili viwe bora zaidi na vizalishe wataalamu mahili wenye ujuzi na ubora unaohitajika.

Ni maarifa gani/ujuzi gani wa ziada anaoupata mwanafunzi aliyepita elimu ya kidato cha tano na sita utakao msaidia yeye katika ulimwengu wa sasa. Ama ni kitu gani cha ziada chenye manufaa watakikosa wanafunzi iwapo elimu ya kidato cha tano na sita itaondolewa na kubakia na elimu ya vyuo vya kati tu.

Naomba wadau, wizara ya elimu na serikali kwa ujumla ilitazame suala hili, tusiendelee kuwa na mifumo ya elimu kwa sababu ilikuwepo tangu mwanzo, kwa sasa inatakiwa tutazame zaidi mabadiliko yaliyopo, ulimwengu umekuwa wa sayansi na teknolojia na unahitaji watu wenye ujuzi zaidi (ili kuwawezesha aidha kujiajiri ama kuwa na sifa za kuajiriwa na kuwa wabunifu zaidi katika nyanja mbalimbali) kitu ambacho elimu ya kidato cha tano na sita haiwezi kutupatia jibu la suala hilo, zaidi ya wanafunzi kukariri vitu ili waje wajibu mitihani wafaulu, tofauti na elimu ya vyuo vya kati, ambapo mwanafunzi anapata mda wa kutosha wa kufanya mafunzo kwa vitendo na tena katika uhalisia, hivyo kumuwezesha kuwa na maarifa, ujuzi wa kutosha, uwezo mkubwa wa ubunifu na utatuzi wa changamoto zinazoikabili dunia katika fani aliyoisomea.

Hivyo itumike elimu ya vyuo vya kati mara tu mwanafunzi anapohitimu kidato cha nne. Hii itasaidia vijana wengi kuwa na ujuzi mapema zaidi na kuwa wabunifu na wenye uwezo mkubwa wa kujiajiri na sio kutegemea kuajiriwa tu.

Serikali iweke utaratibu maalum mwanafunzi anapohitimu kidato cha nne aangaliwe ni masomo gani alikuwa akifanya vizuri zaidi tangu mwanzo na sio mtihani wa mwisho tu, ili aende kusomea fani inayoendana na masomo hayo, au mwanafunzi achague mwenyewe fani anayoona anaimudu na anauwezo wa kuisoma na baadae kuwa na ujuzi wa kutosha katika fani hiyo.

Ahsanteni.
mkuu walioweka kidato cha tano sio wajiga we unadhani mtu atakuwa vipi dactari kama hajasoma habari za chemistry,biology ya form six,mtu anaweza vipi kujua kupima rate ya flow ya maji kwenye bomba kama hajui physics ya a level mtu anaweza kutengeneza ma algorithm kama hajala ma calculus..mtu ataweza kudesign vipi engine ya gari ama ndege kama hajui basics foundation za physics ama biology..wewe unadhani hao wachina ,wazungu wanainuka tuu wanatengeneza rocket wanakula kitabu cha hatari...mawazo ya design yako ndio yanasababisha nchi zetu huku turudi nyu,ma kutujaza ujinga kwamba bora kujifunza kulima matikiti kuuza mia mbili wao wanasomesha maengineer na ma prggrammer kuja kutuuzia machine kwa faida huku sisi na vizazi vyetu tukiishia kuwa masikini....wake up brother ukipata chance ya kusoma soma tena soma sana .Elimu haiumtupi mtu ,
 
Kwani kuna sehemu nimesema watu wasisome?
Kwa hiyo unataka kuniambia wale ma engineer ambao hawakupita advance (waliopita diploma pale DIT na sehemu nyingine) hawawezi kufanya hayo mambo uliyoyataja hapo juu?
Na wale madaktari ambao hawakupita advance, sio madaktari bora kwa sababu hawakuchanganya makemikali na kupasua vyura advance?
Suala ni kwamba, mtu asipopita advance, akaenda diploma hizo basics zote anazipata hukohuko diploma, tena huko anapata vitu vingi zaidi maana huko mambo mengi anafanya kwa vitendo zaidi na anaenda field pia.
 
Kulingana na utaratibu uliopo hivi sasa, mwanafunzi anapo hitimu elimu ya sekondari (kidato cha nne) na kufikisha alama zinazohitajika anaweza kuchaguliwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano na sita/kujiunga na vyuo vya kati (astashahada/stashahada)

1. Mwanafunzi atakayechaguliwa/kuchagua mwenyewe kujiunga na elimu ya kidato cha tano na sita, akihitimu kidato cha sita na kufikisha alama zinazohitajika, atajiunga na elimu ya chuo kikuu (shahada). Na ikitokea mwanafunzi amehitimu kidato cha sita na hajafikisha alama zinazohitajika ili ajiunge na elimu ya chuo kikuu, itambidi arudi nyuma atumie cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili aweze kutuma maombi ya kujiunga na elimu ya vyuo vya kati (astashahada/stashahada).
Kwa maana hiyo mwanafunzi huyo atakuwa amepoteza miaka miwili aliyosoma kidato cha tano na sita, lakini pia wazazi wanakuwa wameingia gharama pamoja na serikali kugharamia elimu kwa mda wa miaka miwili ambayo haina manufaa wala matokeo chanya kwa mwanafunzi mwenyewe, kwa wazazi na taifa kwa ujumla, kwa sababu mwanafunzi huyo anakuwa bado hana ujuzi katika fani yoyote ile utakao muwezesha yeye kuajiriwa ama kujiajiri.

2. Kwa mwanafunzi atakaye chaguliwa/kuchagua mwenyewe kujiunga na vyuo vya kati, atakapo hitimu anaweza kuchagua kuendelea na elimu ya chuo kikuu/kuajiriwa/kujiajiri mwenyewe kwa sababu tayari anakuwa na ujuzi na maarifa ya kutosha kulingana na fani aliyosoma.

Napendekeza kuondolewa kwa elimu ya kidato cha tano na sita kwa sababu, ni njia inayopoteza mda kwa wanafunzi na kuingiza gharama kubwa wazazi na serikali kugharamia elimu ambayo mwisho wa siku mwanafunzi itambidi arudi tena kutumia cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili kujiunga na vyuo vya kati.

Sasa kwa nini mwanafunzi huyu asitumie cheti cha elimu ya sekondari mara tu anapohitimu kidato cha nne na kujiunga moja kwa moja na elimu ya vyuo vya kati kulingana na masomo aliyofaulu au fani atakayo ichagua yeye.

Nitoe mfano mmoja hapa:
Unatakiwa kufika kituo D (elimu ya juu/maisha ya kujiajiri/ kuajiriwa) ukitokea kituo C (kidato cha nne), kuna njia mbili za kukuwezesha kufika kituo D, ambazo ni elimu ya kidato cha tano na sita (njia A) au vyuo vya kati (njia B).

Njia A ni fupi (miaka miwili ya kidato cha tano na sita) lakini inakatiza mtoni, na njia B ni ndefu (miaka mitatu ya stashahada) lakini haikatizi mtoni.

Endapo utaenda na njia A unakuwa hauna uhakika wa moja kwa moja wa kufika kituo D maana kuna uwezekano ukakuta mto umefurika maji na usiweze kuvuka, kwa hiyo itakulazimu urudi tena nyuma uanze safari upya kwa kutumia njia B ambayo haikatizi mtoni ili ikufikishe kituo D.

Ikitokea hivyo, unakua umetumia jumla ya miaka mitano kwa safari ambayo kama ungelichagua njia B tangu mwanzo ingelikugharimu mda wa miaka mitatu tu kufika kituo D.

Mfano huu namaanisha nini:
Elimu ya kidato cha tano na sita mwanafunzi anapohitimu na kushindwa kufikisha alama za kumuwezesha kujiunga na elimu ya chuo kikuu, itamlazimu arudi tena nyuma kutumia cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili aombe kujiunga na elimu ya vyuo vya kati (astashahada/stashahada).

Lakini mwanafunzi aliyehitimu elimu ya vyuo vya kati, tayari anakuwa na ujuzi wa kutosha kumuwezesha yeye kujiajiri/kuajiriwa mahali popote kulingana na fani aliyoisoma na anakuwa na uwezo wa kuendelea na elimu ya juu kama atahitaji kufanya hivyo.

Elimu ya vyuo vya kati inatolewa kwa kiasi kikubwa ikijikita katika ujuzi na kwa vitendo kwa sababu wanafunzi wanaenda kufanya mafunzo kwa vitendo na wakiwa huko wanasimamiwa na kukaguliwa ni tofauti na elimu ya kidato cha tano na sita ambapo wanafunzi wanatumia mda mwingi kukaa darasani kukariri masomo ya nadharia na hata wakiingia maabara, majaribio wanayoyafanya hayana uhalisia kwa asilimia 100 na maisha watakayo kutana nayo baada ya shule aidha ni katika kujiajiri/kuajiriwa.

Elimu ya kidato cha tano na sita kwa sasa haina umuhimu kwa nchi yetu, ni lazima tuchague njia moja iliyo bora zaidi, maana mtu anahitimu kidato cha sita akiwa hana ujuzi wowote ule tofauti na elimu ya vyuo vya kati, ni kwa nini serikali iendelee kuingia gharama kugharamia suala ambalo tunaweza kuachana nalo na kujikita katika njia moja na gharama hizo zote kuelekezwa katika kuboresha mazingira na miundombinu (hasa katika suala la teknolojia) ya kujifunzia na kufundishia katika vyuo vya kati ili viwe bora zaidi na vizalishe wataalamu mahili wenye ujuzi na ubora unaohitajika.

Ni maarifa gani/ujuzi gani wa ziada anaoupata mwanafunzi aliyepita elimu ya kidato cha tano na sita utakao msaidia yeye katika ulimwengu wa sasa. Ama ni kitu gani cha ziada chenye manufaa watakikosa wanafunzi iwapo elimu ya kidato cha tano na sita itaondolewa na kubakia na elimu ya vyuo vya kati tu.

Naomba wadau, wizara ya elimu na serikali kwa ujumla ilitazame suala hili, tusiendelee kuwa na mifumo ya elimu kwa sababu ilikuwepo tangu mwanzo, kwa sasa inatakiwa tutazame zaidi mabadiliko yaliyopo, ulimwengu umekuwa wa sayansi na teknolojia na unahitaji watu wenye ujuzi zaidi (ili kuwawezesha aidha kujiajiri ama kuwa na sifa za kuajiriwa na kuwa wabunifu zaidi katika nyanja mbalimbali) kitu ambacho elimu ya kidato cha tano na sita haiwezi kutupatia jibu la suala hilo, zaidi ya wanafunzi kukariri vitu ili waje wajibu mitihani wafaulu, tofauti na elimu ya vyuo vya kati, ambapo mwanafunzi anapata mda wa kutosha wa kufanya mafunzo kwa vitendo na tena katika uhalisia, hivyo kumuwezesha kuwa na maarifa, ujuzi wa kutosha, uwezo mkubwa wa ubunifu na utatuzi wa changamoto zinazoikabili dunia katika fani aliyoisomea.

Hivyo itumike elimu ya vyuo vya kati mara tu mwanafunzi anapohitimu kidato cha nne. Hii itasaidia vijana wengi kuwa na ujuzi mapema zaidi na kuwa wabunifu na wenye uwezo mkubwa wa kujiajiri na sio kutegemea kuajiriwa tu.

Serikali iweke utaratibu maalum mwanafunzi anapohitimu kidato cha nne aangaliwe ni masomo gani alikuwa akifanya vizuri zaidi tangu mwanzo na sio mtihani wa mwisho tu, ili aende kusomea fani inayoendana na masomo hayo, au mwanafunzi achague mwenyewe fani anayoona anaimudu na anauwezo wa kuisoma na baadae kuwa na ujuzi wa kutosha katika fani hiyo.

Ahsanteni.
Binafsi nilipitia elimu ya kidato cha 5 na 6, na kuendelea na chuo, lakini kwa sasa naona imepitwa na wakati na haina tija. Kimsingi elimu hii imekuwa kama daraja la kwenda chuo kikuu (endapo utafaulu kwa alama zinazohitajika) na sii kumpatia mhitimu ujuzi wowote! Nilisoma kemia kwa undani, lakini baada ya kuhitimu sikuweza kutengeneza sabuni nitakazouza nipate hela! Leo najua kuteneza sabuni baada ya kupata mafunzo ya siku moja tu kutoka kwa mtu ambaye hana elimu hata ile sekondari ya kawaida.
 
Umeshindwa kujiuliza kitu kimoja cha muhimu sana.

1. Lengo letu la elimu hasa ni nini? Elimu ya kidato cha tano na sita inasaidiaje kutimiza lengo hilo?

Ati, wewe utakuwa na amani kufanyiwa upasuaji na daktari ambaye hakupata misingi ya PCB kidato cha sita bali amekomea kidato cha 4 na akaenda sijui vyuo gani vya kati huko unavyovisema (sikumaliza kusoma andiko lako)? Utaweza kupata mhandisi mzuri ambaye hajasoma PCM?

Ni wapi huko ambako hakuna elimu ya Advance au sisi ndiyo tunataka kuwa wa kwanza?

Na muhimu zaidi, bandiko lako hili linasaidiaje kuleta uwajibikaji na uongozi bora ambacho ndicho kipaumbe kikubwa cha shindano la mwaka huu?
Nenda DIT,ATC, MUST na vyuo mbalimbali ambavyo viko chini ya nacte utawakuta wahandisi wengi tu ambao hajachoshana na form five na Six
 
Sioni kama ni sawa mzee wangu,kwanza kabisa ulisema hivyo pia useme elimu ya kidato Cha kwanza Hadi nne pia iondolowe ,na sio tuuh elimu pia ya darasa la kwanza Hadi la saba iondolewe ,
Hapa tutakuwa tumekosea ,Bora mfumo Bora wa elimu uelekezwe Ili wanafunzi waweze jifunza kutokana na teknolojia inavyoenda
 
Back
Top Bottom