SoC03 Elimu ya Kidato cha Tano na Sita iondolewe

SoC03 Elimu ya Kidato cha Tano na Sita iondolewe

Stories of Change - 2023 Competition

Mkoba wa Mama

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2021
Posts
208
Reaction score
91
Kulingana na utaratibu uliopo hivi sasa, mwanafunzi anapo hitimu elimu ya sekondari (kidato cha nne) na kufikisha alama zinazohitajika anaweza kuchaguliwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano na sita/kujiunga na vyuo vya kati (astashahada/stashahada)

1. Mwanafunzi atakayechaguliwa/kuchagua mwenyewe kujiunga na elimu ya kidato cha tano na sita, akihitimu kidato cha sita na kufikisha alama zinazohitajika, atajiunga na elimu ya chuo kikuu (shahada). Na ikitokea mwanafunzi amehitimu kidato cha sita na hajafikisha alama zinazohitajika ili ajiunge na elimu ya chuo kikuu, itambidi arudi nyuma atumie cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili aweze kutuma maombi ya kujiunga na elimu ya vyuo vya kati (astashahada/stashahada).
Kwa maana hiyo mwanafunzi huyo atakuwa amepoteza miaka miwili aliyosoma kidato cha tano na sita, lakini pia wazazi wanakuwa wameingia gharama pamoja na serikali kugharamia elimu kwa mda wa miaka miwili ambayo haina manufaa wala matokeo chanya kwa mwanafunzi mwenyewe, kwa wazazi na taifa kwa ujumla, kwa sababu mwanafunzi huyo anakuwa bado hana ujuzi katika fani yoyote ile utakao muwezesha yeye kuajiriwa ama kujiajiri.

2. Kwa mwanafunzi atakaye chaguliwa/kuchagua mwenyewe kujiunga na vyuo vya kati, atakapo hitimu anaweza kuchagua kuendelea na elimu ya chuo kikuu/kuajiriwa/kujiajiri mwenyewe kwa sababu tayari anakuwa na ujuzi na maarifa ya kutosha kulingana na fani aliyosoma.

Napendekeza kuondolewa kwa elimu ya kidato cha tano na sita kwa sababu, ni njia inayopoteza mda kwa wanafunzi na kuingiza gharama kubwa wazazi na serikali kugharamia elimu ambayo mwisho wa siku mwanafunzi itambidi arudi tena kutumia cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili kujiunga na vyuo vya kati.

Sasa kwa nini mwanafunzi huyu asitumie cheti cha elimu ya sekondari mara tu anapohitimu kidato cha nne na kujiunga moja kwa moja na elimu ya vyuo vya kati kulingana na masomo aliyofaulu au fani atakayo ichagua yeye.

Nitoe mfano mmoja hapa:
Unatakiwa kufika kituo D (elimu ya juu/maisha ya kujiajiri/ kuajiriwa) ukitokea kituo C (kidato cha nne), kuna njia mbili za kukuwezesha kufika kituo D, ambazo ni elimu ya kidato cha tano na sita (njia A) au vyuo vya kati (njia B).

Njia A ni fupi (miaka miwili ya kidato cha tano na sita) lakini inakatiza mtoni, na njia B ni ndefu (miaka mitatu ya stashahada) lakini haikatizi mtoni.

Endapo utaenda na njia A unakuwa hauna uhakika wa moja kwa moja wa kufika kituo D maana kuna uwezekano ukakuta mto umefurika maji na usiweze kuvuka, kwa hiyo itakulazimu urudi tena nyuma uanze safari upya kwa kutumia njia B ambayo haikatizi mtoni ili ikufikishe kituo D.

Ikitokea hivyo, unakua umetumia jumla ya miaka mitano kwa safari ambayo kama ungelichagua njia B tangu mwanzo ingelikugharimu mda wa miaka mitatu tu kufika kituo D.

Mfano huu namaanisha nini:
Elimu ya kidato cha tano na sita mwanafunzi anapohitimu na kushindwa kufikisha alama za kumuwezesha kujiunga na elimu ya chuo kikuu, itamlazimu arudi tena nyuma kutumia cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili aombe kujiunga na elimu ya vyuo vya kati (astashahada/stashahada).

Lakini mwanafunzi aliyehitimu elimu ya vyuo vya kati, tayari anakuwa na ujuzi wa kutosha kumuwezesha yeye kujiajiri/kuajiriwa mahali popote kulingana na fani aliyoisoma na anakuwa na uwezo wa kuendelea na elimu ya juu kama atahitaji kufanya hivyo.

Elimu ya vyuo vya kati inatolewa kwa kiasi kikubwa ikijikita katika ujuzi na kwa vitendo kwa sababu wanafunzi wanaenda kufanya mafunzo kwa vitendo na wakiwa huko wanasimamiwa na kukaguliwa ni tofauti na elimu ya kidato cha tano na sita ambapo wanafunzi wanatumia mda mwingi kukaa darasani kukariri masomo ya nadharia na hata wakiingia maabara, majaribio wanayoyafanya hayana uhalisia kwa asilimia 100 na maisha watakayo kutana nayo baada ya shule aidha ni katika kujiajiri/kuajiriwa.

Elimu ya kidato cha tano na sita kwa sasa haina umuhimu kwa nchi yetu, ni lazima tuchague njia moja iliyo bora zaidi, maana mtu anahitimu kidato cha sita akiwa hana ujuzi wowote ule tofauti na elimu ya vyuo vya kati, ni kwa nini serikali iendelee kuingia gharama kugharamia suala ambalo tunaweza kuachana nalo na kujikita katika njia moja na gharama hizo zote kuelekezwa katika kuboresha mazingira na miundombinu (hasa katika suala la teknolojia) ya kujifunzia na kufundishia katika vyuo vya kati ili viwe bora zaidi na vizalishe wataalamu mahili wenye ujuzi na ubora unaohitajika.

Ni maarifa gani/ujuzi gani wa ziada anaoupata mwanafunzi aliyepita elimu ya kidato cha tano na sita utakao msaidia yeye katika ulimwengu wa sasa. Ama ni kitu gani cha ziada chenye manufaa watakikosa wanafunzi iwapo elimu ya kidato cha tano na sita itaondolewa na kubakia na elimu ya vyuo vya kati tu.

Naomba wadau, wizara ya elimu na serikali kwa ujumla ilitazame suala hili, tusiendelee kuwa na mifumo ya elimu kwa sababu ilikuwepo tangu mwanzo, kwa sasa inatakiwa tutazame zaidi mabadiliko yaliyopo, ulimwengu umekuwa wa sayansi na teknolojia na unahitaji watu wenye ujuzi zaidi (ili kuwawezesha aidha kujiajiri ama kuwa na sifa za kuajiriwa na kuwa wabunifu zaidi katika nyanja mbalimbali) kitu ambacho elimu ya kidato cha tano na sita haiwezi kutupatia jibu la suala hilo, zaidi ya wanafunzi kukariri vitu ili waje wajibu mitihani wafaulu, tofauti na elimu ya vyuo vya kati, ambapo mwanafunzi anapata mda wa kutosha wa kufanya mafunzo kwa vitendo na tena katika uhalisia, hivyo kumuwezesha kuwa na maarifa, ujuzi wa kutosha, uwezo mkubwa wa ubunifu na utatuzi wa changamoto zinazoikabili dunia katika fani aliyoisomea.

Hivyo itumike elimu ya vyuo vya kati mara tu mwanafunzi anapohitimu kidato cha nne. Hii itasaidia vijana wengi kuwa na ujuzi mapema zaidi na kuwa wabunifu na wenye uwezo mkubwa wa kujiajiri na sio kutegemea kuajiriwa tu.

Serikali iweke utaratibu maalum mwanafunzi anapohitimu kidato cha nne aangaliwe ni masomo gani alikuwa akifanya vizuri zaidi tangu mwanzo na sio mtihani wa mwisho tu, ili aende kusomea fani inayoendana na masomo hayo, au mwanafunzi achague mwenyewe fani anayoona anaimudu na anauwezo wa kuisoma na baadae kuwa na ujuzi wa kutosha katika fani hiyo.

Ahsanteni.
 
Upvote 43
Binafsi nilipitia elimu ya kidato cha 5 na 6, na kuendelea na chuo, lakini kwa sasa naona imepitwa na wakati na haina tija. Kimsingi elimu hii imekuwa kama daraja la kwenda chuo kikuu (endapo utafaulu kwa alama zinazohitajika) na sii kumpatia mhitimu ujuzi wowote! Nilisoma kemia kwa undani, lakini baada ya kuhitimu sikuweza kutengeneza sabuni nitakazouza nipate hela! Leo najua kuteneza sabuni baada ya kupata mafunzo ya siku moja tu kutoka kwa mtu ambaye hana elimu hata ile sekondari ya kawaida.
Uko sahihi mkuu,elimu ya advance in its real sence nikama daraja tu kwa watakaofauru,hugeuka kupoteza mda kwa waliofeli maana hulazimika kurudia cheti cha form four kwenda diploma
 
Ilo ni moja kati ya mengi yanayopaswa kutizamwa kwenye mfumo wetu wa elimu
Achana na kufeli mtu anafaulu PCB anakosa chuo anaenda kusoma sheria/uwasibu hii inaonyesha tunafanya vitu ilimradi vimefanyika lazima elimu yetu iwe inaonyesha lengo
Kwanzia elimu ya msingi iyonyeshe ninini inajenga
 
Binafsi sijafika hizo level za advance, nipo najiendeleza na QT ila hii hainizuii kutoa maoni.

Nimeona baadhi hawajaunga mkono hoja kwa sababu mbalimbali , hii ni moja wapo ya sababu hizo "mwanafunzi anayetarajia kuwa daktari anapaswa asome PCB advance ili aweze kumudu masomo ya Chuo n.k"

Naomba kuuliza,
1. Mfano: Muhitimu wa Stashahada ya Medical Laboratory science kisha akapata Shahada na yule aliyehitimu kidato cha Sita akaenda kusoma Shahada ya Medical Laboratory Science yupi atakuwa na uelewa mpana kwenye kada husika?

2. Hiki kinachofundishwa Kidato cha sita kina mahusiano ya moja kwa moja na kinachoenda kufundishwa chuo ngazi ya shahada?? Kama Jibu ni ndio mahusiano hayo yanaweza kuwa ni asilimia ngapi ukilinganisha na kile kinachofundishwa ngazi ya Stashahada??

3. Muhitimu kidato cha sita mfano PCB, kwa kiwango hicho cha elimu anaweza kuwa na uelewa wa awali kada ya Afya? (MD, Radiology, Laboratory n.k)

4. Kinachofundishwa ngazi ya stashahada ni tofauti na kichofundishwa Kidato cha sita, wanasoma masomo tofauti ila wote wanaweza kusoma Shahada.

Je haya yanayofundishwa Kidato cha sita yanafaida gani kama asiyeyasoma bado anaweza kusoma Shahada? Nikipi special atakuwanacho huyu aliyesoma kidato cha sita kisha akasoma Shahada?

Maoni yangu ya awali ni Kwamba Sioni umuhimu wa kusoma kidato cha sita Ila nipo tayari kubadili msimamo kama nitajibiwa maswali yangu na kupata ufafanuzi zaidi

Asante.
 
Mtoa maada ulisoma advance? na comb gani? Je ni kweli advance umeona Haina umuhimu katika maisha yako. Tuanzia hapo
 
Back
Top Bottom