SoC03 Elimu ya Kidato cha Tano na Sita iondolewe

SoC03 Elimu ya Kidato cha Tano na Sita iondolewe

Stories of Change - 2023 Competition

Mkoba wa Mama

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2021
Posts
208
Reaction score
91
Kulingana na utaratibu uliopo hivi sasa, mwanafunzi anapo hitimu elimu ya sekondari (kidato cha nne) na kufikisha alama zinazohitajika anaweza kuchaguliwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano na sita/kujiunga na vyuo vya kati (astashahada/stashahada)

1. Mwanafunzi atakayechaguliwa/kuchagua mwenyewe kujiunga na elimu ya kidato cha tano na sita, akihitimu kidato cha sita na kufikisha alama zinazohitajika, atajiunga na elimu ya chuo kikuu (shahada). Na ikitokea mwanafunzi amehitimu kidato cha sita na hajafikisha alama zinazohitajika ili ajiunge na elimu ya chuo kikuu, itambidi arudi nyuma atumie cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili aweze kutuma maombi ya kujiunga na elimu ya vyuo vya kati (astashahada/stashahada).
Kwa maana hiyo mwanafunzi huyo atakuwa amepoteza miaka miwili aliyosoma kidato cha tano na sita, lakini pia wazazi wanakuwa wameingia gharama pamoja na serikali kugharamia elimu kwa mda wa miaka miwili ambayo haina manufaa wala matokeo chanya kwa mwanafunzi mwenyewe, kwa wazazi na taifa kwa ujumla, kwa sababu mwanafunzi huyo anakuwa bado hana ujuzi katika fani yoyote ile utakao muwezesha yeye kuajiriwa ama kujiajiri.

2. Kwa mwanafunzi atakaye chaguliwa/kuchagua mwenyewe kujiunga na vyuo vya kati, atakapo hitimu anaweza kuchagua kuendelea na elimu ya chuo kikuu/kuajiriwa/kujiajiri mwenyewe kwa sababu tayari anakuwa na ujuzi na maarifa ya kutosha kulingana na fani aliyosoma.

Napendekeza kuondolewa kwa elimu ya kidato cha tano na sita kwa sababu, ni njia inayopoteza mda kwa wanafunzi na kuingiza gharama kubwa wazazi na serikali kugharamia elimu ambayo mwisho wa siku mwanafunzi itambidi arudi tena kutumia cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili kujiunga na vyuo vya kati.

Sasa kwa nini mwanafunzi huyu asitumie cheti cha elimu ya sekondari mara tu anapohitimu kidato cha nne na kujiunga moja kwa moja na elimu ya vyuo vya kati kulingana na masomo aliyofaulu au fani atakayo ichagua yeye.

Nitoe mfano mmoja hapa:
Unatakiwa kufika kituo D (elimu ya juu/maisha ya kujiajiri/ kuajiriwa) ukitokea kituo C (kidato cha nne), kuna njia mbili za kukuwezesha kufika kituo D, ambazo ni elimu ya kidato cha tano na sita (njia A) au vyuo vya kati (njia B).

Njia A ni fupi (miaka miwili ya kidato cha tano na sita) lakini inakatiza mtoni, na njia B ni ndefu (miaka mitatu ya stashahada) lakini haikatizi mtoni.

Endapo utaenda na njia A unakuwa hauna uhakika wa moja kwa moja wa kufika kituo D maana kuna uwezekano ukakuta mto umefurika maji na usiweze kuvuka, kwa hiyo itakulazimu urudi tena nyuma uanze safari upya kwa kutumia njia B ambayo haikatizi mtoni ili ikufikishe kituo D.

Ikitokea hivyo, unakua umetumia jumla ya miaka mitano kwa safari ambayo kama ungelichagua njia B tangu mwanzo ingelikugharimu mda wa miaka mitatu tu kufika kituo D.

Mfano huu namaanisha nini:
Elimu ya kidato cha tano na sita mwanafunzi anapohitimu na kushindwa kufikisha alama za kumuwezesha kujiunga na elimu ya chuo kikuu, itamlazimu arudi tena nyuma kutumia cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili aombe kujiunga na elimu ya vyuo vya kati (astashahada/stashahada).

Lakini mwanafunzi aliyehitimu elimu ya vyuo vya kati, tayari anakuwa na ujuzi wa kutosha kumuwezesha yeye kujiajiri/kuajiriwa mahali popote kulingana na fani aliyoisoma na anakuwa na uwezo wa kuendelea na elimu ya juu kama atahitaji kufanya hivyo.

Elimu ya vyuo vya kati inatolewa kwa kiasi kikubwa ikijikita katika ujuzi na kwa vitendo kwa sababu wanafunzi wanaenda kufanya mafunzo kwa vitendo na wakiwa huko wanasimamiwa na kukaguliwa ni tofauti na elimu ya kidato cha tano na sita ambapo wanafunzi wanatumia mda mwingi kukaa darasani kukariri masomo ya nadharia na hata wakiingia maabara, majaribio wanayoyafanya hayana uhalisia kwa asilimia 100 na maisha watakayo kutana nayo baada ya shule aidha ni katika kujiajiri/kuajiriwa.

Elimu ya kidato cha tano na sita kwa sasa haina umuhimu kwa nchi yetu, ni lazima tuchague njia moja iliyo bora zaidi, maana mtu anahitimu kidato cha sita akiwa hana ujuzi wowote ule tofauti na elimu ya vyuo vya kati, ni kwa nini serikali iendelee kuingia gharama kugharamia suala ambalo tunaweza kuachana nalo na kujikita katika njia moja na gharama hizo zote kuelekezwa katika kuboresha mazingira na miundombinu (hasa katika suala la teknolojia) ya kujifunzia na kufundishia katika vyuo vya kati ili viwe bora zaidi na vizalishe wataalamu mahili wenye ujuzi na ubora unaohitajika.

Ni maarifa gani/ujuzi gani wa ziada anaoupata mwanafunzi aliyepita elimu ya kidato cha tano na sita utakao msaidia yeye katika ulimwengu wa sasa. Ama ni kitu gani cha ziada chenye manufaa watakikosa wanafunzi iwapo elimu ya kidato cha tano na sita itaondolewa na kubakia na elimu ya vyuo vya kati tu.

Naomba wadau, wizara ya elimu na serikali kwa ujumla ilitazame suala hili, tusiendelee kuwa na mifumo ya elimu kwa sababu ilikuwepo tangu mwanzo, kwa sasa inatakiwa tutazame zaidi mabadiliko yaliyopo, ulimwengu umekuwa wa sayansi na teknolojia na unahitaji watu wenye ujuzi zaidi (ili kuwawezesha aidha kujiajiri ama kuwa na sifa za kuajiriwa na kuwa wabunifu zaidi katika nyanja mbalimbali) kitu ambacho elimu ya kidato cha tano na sita haiwezi kutupatia jibu la suala hilo, zaidi ya wanafunzi kukariri vitu ili waje wajibu mitihani wafaulu, tofauti na elimu ya vyuo vya kati, ambapo mwanafunzi anapata mda wa kutosha wa kufanya mafunzo kwa vitendo na tena katika uhalisia, hivyo kumuwezesha kuwa na maarifa, ujuzi wa kutosha, uwezo mkubwa wa ubunifu na utatuzi wa changamoto zinazoikabili dunia katika fani aliyoisomea.

Hivyo itumike elimu ya vyuo vya kati mara tu mwanafunzi anapohitimu kidato cha nne. Hii itasaidia vijana wengi kuwa na ujuzi mapema zaidi na kuwa wabunifu na wenye uwezo mkubwa wa kujiajiri na sio kutegemea kuajiriwa tu.

Serikali iweke utaratibu maalum mwanafunzi anapohitimu kidato cha nne aangaliwe ni masomo gani alikuwa akifanya vizuri zaidi tangu mwanzo na sio mtihani wa mwisho tu, ili aende kusomea fani inayoendana na masomo hayo, au mwanafunzi achague mwenyewe fani anayoona anaimudu na anauwezo wa kuisoma na baadae kuwa na ujuzi wa kutosha katika fani hiyo.

Ahsanteni.
 
Upvote 43
Mimi huwa nawaza kama muhitimu wa chuo aliyekaa mtaani miaka nane (8 years) toa ile mitatu ya masomo na hajafanikiwa kupata kazi ya kutumia elimu aliyoisotea huwa anajisikiaje linapokuja suala la kumpeleka mwanae hadi elimu ya juu?

Elimu ya darasani sasa hivi hasa kwa mtoto wa maskini haina inachomsaidia uangaliwe utaratibu wa kuwapa mafunzo mbalimbali vijana ili angalao wakitoka hapo four au six wawe na wepesi kujichanganya mitaani tofauti na sasa kukaa kusubiri matokeo ili waende vyuo,point yangu hapa ni kwamba wakati anaposubiri matokeo awe na msukumo wa kwenda kujaribu yale maarifa aliyofundishwa akiona yana-apply kwenye maisha yake anakomaa humo humo siyo kama sasa wanaenda chuo wote wanamaliza na vyeti wote then wanamwagwa mitaani wote kugombania goal ambalo limeshajazwa na ndugu wa mabosi

Ndio maana siku hizi watu wanatoa watoto wao English Mediums wanawapeleka kayumba plus English courses. Shule imekuwa sehemu ya watoto kukua . Wanaandaliwa tu kuajiriwa na sio kutengeneza ajira.
 
Je ni umuhimu upi unaouzungumzia wewe kupata ujuzi, ajira au maarifa ya Hali ya juu
Diploma unapata vyote hivyo ulivyovitaja hapo, lakini kwa advance ni maarifa tu, na sio wote wanapata hayo maarifa, wengine wanatoka advance wakiwa weupe kabisa, sababu walikuwa wanasoma kwa kukariri ili waweze kujibu mtihani wa mwisho
 
Una akil labda i sana ndugu yangu
Vyuo vya nje vizuri huhitaji aliyemaliza kidato cha sita
Labda kama lengo lako kutengeneza mtoto kayumba basi asiende form five.Kuna wazazi wanaanda watoto sio tu kuishia kuwa local product za mitaani
 
Je ni umuhimu upi unaouzungumzia wewe kupata ujuzi, ajira au maarifa ya Hali ya juu
Mbona unauliza Alafu unajijibu mkuu??? Unauliza swali ambalo majibu unayo.

Aliyehitimu Kidato cha sita hana ujuzi wowote, hana maarifa ya fani anayokwenda kusoma chuo, hawezi kuajiliwa kwa kazi zinazohitaji ujuzi labda kazi za nguvu,

Aliyehitimu Stashahada anaoujuzi, anayo maarifa, anaweza kuajiliwa kama mtu mwenye ujuzi.
 
Vyuo vya nje vizuri huhitaji aliyemaliza kidato cha sita
Labda kama lengo lako kutengeneza mtoto kayumba basi asiende form five.Kuna wazazi wanaanda watoto sio tu kuishia kuwa local product za mitaani
Kwa hiyo mtu mwenye diploma hawezi kupata chuo bora nje ya nchi?
 
Kwa hiyo mtu mwenye diploma hawezi kupata chuo bora nje ya nchi?
Hawezi kabisa

Ndio maana kipindi cha waziri Ndalichako aliwaambia vyuo vikuu wasidshili kabisa mtu mwenye diploma baadaye wakalegeza kidogo lakini hata hapa nchini mtu wa Diploma kupata nafasi ya vyuo bora sio rahisi kabisa
 
Cha muhimu ni ufaulu, lakini suala la mtu mwenye diploma kukosa chuo hapo sikubaliani na wewe, maana tunaona watu wengi tu wenye diploma wanaenda kujiendeleza na degree.
 
Cha muhimu ni ufaulu, lakini suala la mtu mwenye diploma kukosa chuo hapo sikubaliani na wewe, maana tunaona watu wengi tu wenye diploma wanaenda kujiendeleza na degree.
Kaangalie anatakiwa kuwa na ufaulu gani
Kaangalie matokeo ya wanaojiunga vyuo vikali kama UDSM au Muhimbili katafute ws diploma wako wangapi

Course karibu zote unaweza usimpate hata mmoja wa Diploma..Ukiona kuna mwenye Diploma ufaulu wake ujue ulikuwa mkubwa .Wengi huwa hawapenyi vyuo bora

Upitie majina ya wajiunga na hivyo vyuo ndio.utajua kuwa Diploma mwisho nyingi ni mitaani sio milango ya chuo kikuu
 
Ndio maana nikasema cha muhimu ni ufaulu.
Vyuo vikuu wanachukua kuanzia GPA ya 3.5. Kama mtu ana GPA nzuri hawezi kuachwa eti kwa sababu hajasoma fm6, hiyo haipo. Nafasi nyingi zinatolewa kwa fm6 kwa sababu tu idadi yao ni kubwa sana ukilinganisha na wale wa diploma.
Na suala la watu wenye diploma kuwa wachache vyuo vikuu wala sio hoja, maana watu wengi wanapomaliza diploma mara nyingi huingia mtaani kwanza kutafuta ajira au kupiga michakato mingine tofauti na wanaomaliza fm6 ambao huunganisha chuo kikuu moja kwa moja. Watu wengi wa diploma mara nyingi hurudi shule baada ya miaka 2 hata na zaidi.
 
Diploma unapata vyote hivyo ulivyovitaja hapo, lakini kwa advance ni maarifa tu, na sio wote wanapata hayo maarifa, wengine wanatoka advance wakiwa weupe kabisa, sababu walikuwa wanasoma kwa kukariri ili waweze kujibu mtihani wa mwisho
Kwa diploma Ujuzi waku ungaunga, ajira mpaka uaajiliwe na kujiajiri kwenyewe ni Kwa pinde kutokana ujuzi wakungaunga, na maarifa zero kabisa wanafunzi wa form Four wanakariri vibaya mno sometimes hawajui hata wanasoma Nini?

Lakini Kwa advance ujuzi hakuna sikatai ila ni elimu ambayo inakufanya Kuwa rafiki na mazingira asilia na ni rahisi kutatua changamoto nyingi sana zinazokuzunguka ni rahisi kucopy kujifunza technology ya aina yoyote Ile duniani.
 
Vyuo vya nje vizuri huhitaji aliyemaliza kidato cha sita
Labda kama lengo lako kutengeneza mtoto kayumba basi asiende form five.Kuna wazazi wanaanda watoto sio tu kuishia kuwa local product za mitaani
Mwambie hivi kua huo mfumo wa ADVANCE ulirithiwa kutoka Kwa mtaala wa muingereza ambao ni ICSE. Hapo hapo nchi nyingine ziliona ni vyema kuunda mtaala kama huo ambazo ni kama marekani alikuja ADVANCE PLACEMENT(A.P). Na Australia amekuja na INTERNATIONAL BACCALAUREATE (I.B). Sasa sisi nikina nani tuukane
 
Mbona unauliza Alafu unajijibu mkuu??? Unauliza swali ambalo majibu unayo.

Aliyehitimu Kidato cha sita hana ujuzi wowote, hana maarifa ya fani anayokwenda kusoma chuo, hawezi kuajiliwa kwa kazi zinazohitaji ujuzi labda kazi za nguvu,

Aliyehitimu Stashahada anaoujuzi, anayo maarifa, anaweza kuajiliwa kama mtu mwenye ujuzi.
Mkuu sio Kila elimu lengo lake ni ajira mzee hii ndio Tatizo la sisi watu weusi. Advance haikuwekwa Kwa malengo hayo ya ajira iliwekwa Ili kuumpa mwanafunzi uwanja wa mpana kupambana na mazingira yake shida ya sisi tunawaza ajira.
 
Hawezi kabisa

Ndio maana kipindi cha waziri Ndalichako aliwaambia vyuo vikuu wasidshili kabisa mtu mwenye diploma baadaye wakalegeza kidogo lakini hata hapa nchini mtu wa Diploma kupata nafasi ya vyuo bora sio rahisi kabisa
Kwanza kabisa kiwango Cha kuingia diploma chenyewe kinajieleza eti D 4 hapa kweli nahisi unapata viashilia kua diploma ni elimu isiyotaka uwelewa wa Hali ya juu Sasa mtu wa diploma utamplekaje ng'ambo
 
Ndio maana nikasema cha muhimu ni ufaulu.
Vyuo vikuu wanachukua kuanzia GPA ya 3.5. Kama mtu ana GPA nzuri hawezi kuachwa eti kwa sababu hajasoma fm6, hiyo haipo. Nafasi nyingi zinatolewa kwa fm6 kwa sababu tu idadi yao ni kubwa sana ukilinganisha na wale wa diploma.
Na suala la watu wenye diploma kuwa wachache vyuo vikuu wala sio hoja, maana watu wengi wanapomaliza diploma mara nyingi huingia mtaani kwanza kutafuta ajira au kupiga michakato mingine tofauti na wanaomaliza fm6 ambao huunganisha chuo kikuu moja kwa moja. Watu wengi wa diploma mara nyingi hurudi shule baada ya miaka 2 hata na zaidi.
mfano medicine ukipitia form four ni njia ngumu sana sababu unahitaji miaka angalau 5 ili uwe eligible kusoma degree ya medicine tofauti na aliyepitia form six akifauli tu njia yake ni rahis sana same kwa kozi nyingi za engineering

In short course za science karibia zote anayepitia form six anatumia njia fupi kuliko hata anayepitia diploma

Kwa diploma ni nzuri kwa course za biashara na arts ila sio science
 
Kwanza kabisa kiwango Cha kuingia diploma chenyewe kinajieleza eti D 4 hapa kweli nahisi unapata viashilia kua diploma ni elimu isiyotaka uwelewa wa Hali ya juu Sasa mtu wa diploma utamplekaje ng'ambo
Hata kwa vyuo vingi wenye gpa kubwa wengi wao ni wale waliopitia form six hii ni sababu pia waliopitia diploma wengi wao walifeli
 
mfano medicine ukipitia form four ni njia ngumu sana tofauti na aliyepitia form six same kwa kozi nyingi za engineering

In short course za science karibia zote anayepitia form six anatumia njia fupi kuliko hata anayepitia diploma

Kwa diploma ni nzuri kwa course za biashara na arts ila sio science
Ni kweli mkuu japo Kuna hivi vyuo vya ufundi Kama dit vinadai vyenyewe vina toa degree ya Engineering Kwa aliyepita diploma lakini ukimwangalia engineer mwenyewe hajui hesabu Hajui physics Sasa huwa nashindwa kuelewa ni engineer ukimlinganisha na standard ipi.
 
Kwa masomo ya science A level anajifunza mambo mengi sana mfano physics ya A level iko deep sana, same kwa mathematics, na biology ziko deep sana kwa A level ukifananisha na O level

Hio point ya A level haina faida ni kwa ajili ya kada za biashara, au arts sababu huko ni rahisi ukasoma ili upate cheti

Ila ukija kwenye science hausomi tu upate cheti bali uelemike ndo maana kwa scince A level ina umuhimu kupita maelezo
 
Mfano kipindi nipo A level na chuo tulikua hatupendi vitabu vya marekani na uk kwa sababu vile vitabu huwezi kuta wamelist point yaani point imejificha huko katikati tukawa tunapenda kusoma vitabu vya india sababu wale point wamezi list kwa hiyo hupati shida ya kusoma kwa sababu ukweli ni kwamba sisi watanzania ni wavivu sana kusoma

Hata ukiangalia vitabu walivyoandika kutoka western phds holders na vitabu vyetu vya phd holders wa tanzania na afrika ni mbingu na ardhi hii ni sababu sisi tunasoma ili kupata cheti na sio kuelemika

Wote wanaopigia chapuo diploma na kuponda A level ni wanaogopa mziki wa A level na wanapenda shortcut na wao wanadhani elimu ni vyeti au makaratasi wanasahau lengo la elimu ni upate maarifa na sio vyeti

Mtu yeyote aliyesoma ili aelemike huwezi mkuta hana kazi sababu kamwe hatategemea vyeti ili aishi sababu sehemu ya vyeti ni ndogo sana kwenye maisha yetu ya kila siku
 
Nakumbuka sana vitabu kama University physics, nelkon na ramsden, rogermancaster, Tom Duncan ulikua huwizi kuvikosa watu walikua hawavisomi kabisa. Wao ulikuwa ni mwendo wa mapamu yakina kitedy sijui challange yaani hayo watu walithubutu Hadi kuyaficha
 
Huku Afrika kipaumbele ni ufaulu upate cheti na sio uelimike ndo maana leo hii ni kawaida kuona ufaulu mkubwa sana form six tofauti na miaka ya nyuma point ni kwamba shule nyingin Tanzania zinampa-mbinu mwanafunzi afaulu tu kama kipaumbele na sio kuelimika

Ni rahis sana mtu kukwambia A level ifutwe ukweli ni kwamba sisi ni watu ambao tunatafuta short-cut always ndo maana tuko kama tulivyo maskin sana wanatu ni ma-proffesor ila hawana maajabu au output yeyote

Dhana ya elimu kwa mwafrika na mzungu ni vitu viwili tofauti
 
Back
Top Bottom