Unaongelea cooperatives yaani ushirika? Hilo liliishafeli. Cooporations kama Amazon siyo ushirika.
Naanza kupata shaka kama unanielewa wako mkuu..., rudia kusoma kuanzia mwanzo nimeongelea nini ili niepuke kujirudia..., Kwanini nimeongelea Amazon (sababu tunakoelekea generation ya sasa ni tofauti na wao kununua Insta na Facebook ndio mpango mzima, ingawa utapeli unafanya movement iwe ngumu) convinience ni muhimu, mtu anakwenda kwenye duka la Mangi kupata mahitaji, na kama hayo mahitaji anaweza kuyapata kwake kwa bei nafuu kuliko Mangi atafanya hivyo...., Nilivyoongelea Amazon (ambayo ni business model) ukasema inapunguza uchumi kwa watu wachache kufaya kitu nikakwambia unajua cooperatives..., chama chochote cha ushirika kinaweza kikatumia business model ya Amazon..., kuna maduka makubwa na corporations world wide ambazo ni Ushirika..., if am not mistaken hata Tanga Fresh Maziwa ilikuwa ni ushirika..., Kwahio ku-fail au kushamiri kwa Amazon sio sababu ya kutokuwa ushirika au la ni business model yake na how the business is run...., kuwa na maduka yameongozana kila mlango yanauza kilekile sio efficiency ni kama uchafu..., zamani duka moja labda mtaa hata mwenye duka anapata cha kueleweka sasa hivi kila ukipiga tambo ni duka (kugawana umasikini) bora muda huo watu wangetumia hata kutunga singeli watu waburudike....
Na ili kuepuka kujirudia huko mbele naomba uelewe kwamba ninapoongelea AMAZON ni kile anachofanya sio necessarily Business Model nzima (Mtu kupata kitu Conveniently) Ninapoongelea Cooperatives naongelea Umiliki (Ownership) Hence badala ya Amazon kuwa owned na Bezos na jamaa wachache ingeweza kuwa owned na Cooperation ya Singasinga wote huko Saskatchewan au Gamboshi....
Kama tunatafuta Efficiency kwa nini tusiwape watu 100? Kama tunatafuta efficiency zaidi kwa nini tusimpe mtu mmoja? Unachanganyachanganya logic.
Tusiwape wewe ni nani unawapa ? Binadamu haifai apangiwe anafanya anachofanya na kwenye biashara ambayo ni ushindani akija mtu mwenye better business model wewe unakufa kifo cha kawaida...., Amazon alianza kwa kuuza vitabu ambavyo yeye sio publisher wala hana publishing company wala duka..., ukinunua anaenda madukani anachukua na kukuletea matokeo yake alipata soko kwa overheads ndogo mpaka publishing companies zikamgongea mlango sababu alichukua soko lao na yeye ni efficient kuliko wao.., kwahio maisha haupewi bali unakuwa squeezed nje ya market na kuwa obsolete IBM alikuwa ndio Baba wa Computer (Mainframes) hakutaka kuingia kwenye PC (Personal Computers) akiona kwamba yeye soko lake ni maintance kuja kushituka ni too late ikabidi atengeneza haraka haraka na kujiunga na kina Gates kwa kutumia OS yao ama sivyo angepotea kwenye ramani....
Kwahio kwa kukurahisishia ni kwamba maisha yanabadilika na yakibadilika inabidi ku-adapt na hapa issue ni mgawanyiko wa faida.., sasa kama issue ni mgawanyiko inabidi cooperative ichukue modal which works sababu zisipofanya hivyo wachache au mmoja atafanya kwa faida yake na itabidi watu waanze kulia Monopoly na kumzuia mtu (sababu anachofanya ni bora kwanini kisifanyike kwa manufaa ya wengi after all hapo which matters ni ownership) hata hii Voda ingeweza kuwa owned na wakazi wote wa Temeke kwa kupewa (shares) lakini wafanyakazi na management bado ikabakia ambavyo ilivyo sasa....
Mazingira yanayofanya wenzetu malls ziflourish ndiyo yanafanya online business/ na delivery ziflourish. Hapa kwetu hayapo.
Tofauti ya malls na soko la Kariakoo au genge au mnadani au gulio ni nini zaidi ya miundombinu ? Kwa taarifa yako hizo malls ndio minada ya huku..., ni kwamba tu kuna mpangilio..., online business huku ni ngumu ku-take another step sababu ya utapeli na uongo uongo..., leo Mangi akisema ukitaka kitu nakuletea kwako utakataa.., unacho-suggest badala ya kuwa na Duka la Mangi kila duka la tatu kila nyumba iwe na Duka la Mangi..., sasa mimi nakwambia kwa kuwaza future ni kuwa na more efficient ways na mipangilio.....
Umesema haya mambo kwetu hayapo kwahio tuwekeze yawepo sio kuwekeza kuendelea kuwa na mediocrity....
Duka la mangi ni biashara ya kale sana duniani. Haiwezi kusemwa ilianzishwa na watu fulani. Toka enzi za kabla ya Yesu yapo. Na kwa nchi yetu ambayo hakuna habari ya zoning zinazokataza biashara kwenye makazi, duka la mangi litaendelea kuwepo na kuwa muajiri mkubwa.
Ndio hapo nasema najikuta ninajirudiarudia nimekwambia haya maduka hata nje yapo yaani corner shops au convenient shops..., sababu kwa wenzetu kuliko kwenda malls ambapo huenda ni cheaper unachukua kitu karibu yako kwa rejareja hence inakusaidia kwenye muda lakini kwa giants kutaka biashara zaidi wameanza hadi kureach kwenye nyumba za watu kwa delivery (ndio hapo ukasema inaharibu uchumi local) mimi nakwambia hio ndio future na sio lazima Mangi aendelee kuwa Mangi kama biashara yake ikifa kwa kupata kitu bora maybe bore aanze kuuza mbege au kutumia muda wake kwa kitu ambacho atafanya more efficiently..., Mangi hakatazwi kuwepo ila wewe unataka hii shughuli hadi tuweke kwenye mitaala kwamba tuendelee kuwepo hapa ambapo maybe badala ya kuwepo hapa tungeinvest kwenye kutoka hapa na kwenda pale sababu teknolojia ipo.....
Unataka turudi kwenye ujamaa!!?
Ujamaa ni nini ? Au unaongelea duka la Kaya ? Nadhani wewe ndio unataka tubaki kwenye maduka ya Kaya kwamba Mangi lazima awepo ili apate Pesa mimi nakwambia Mangi awepo ila kama Azam anaweza kufanya kazi kwa gharama ndogo na bei ndogo basi aje hata kama kina Mangi wakifa kifo cha kawaida so be it.... (sio lazima owner awe Azam wanaweza kuwa Mangi wote wa Kibosho)
Kusoma bookkeeping na kusoma uhalisia wa kuendesha duka la mangi ni vitu viwili tofauti. Waendeshaji wengi hawajapitia bookkeeping.
Ndio hapo unakosea tena..., Ujasiriamali haufudishwi shule pekee its way of life..., wahindi tangia mtoto anazaliwa anakaa dukani na mama yake huku mama yake anauza (anfanya practicals since day one) huenda mimi ninajua theory zaidi kuliko Mangi na nikizi-apply huenda nikafanikiwa kuliko Mangi ila sina discipline ya pesa wala muda na uvumilivu wa kukaa dukani masaa na masaa wala customer care...., hayo hayafundishwi kwenye makabrasha ni maisha ya mtu anayoyaishi kila siku hence kuboresha (na huenda kuboresha huko ni kuongeza reach na kuwa kama kina Amazon na sio kubakia nyuma sababu wakati utakupita)
Au kama vipi basi shule wapeani zamu ya kila mwanafunzi kuuza maandazi na pipi za mwalimu mkuu kwa mwaka kila watu 100 kwa mwezi mmojamoja..., hio itakuwa more practically ingawa huenda tukapelekea watoto kuiba chenji za kutoa sadaka kanisani sababu mwalimu kanuna fulani hanunui maandazi yangu....