Moja je ni Vizuri kuwa na Duka kila Mlango: Ulishawahi kuwa na Duka au umeshaongea na mtu mwenye duka mitaa ya Bongo ? Kwa taarifa yako zamani walikuwa wanafurahia sababu wanapata wateja wa kutosha sasa hivi supply ni kubwa kuliko demand (hawana alternative cha kufanya ni mwendo wa kugawana umasikini utasikia wanasema riziki analeta Mungu) Nikupe case study ndogo unayoweza ukarelate.., hapo mwanzo Bodaboda walikuwepo hatua hata ishirini na watu kwa siku walikuwa wanaweza kulala na hata elfu sitini sasa hivi ukitoka tu getini kwako kuna Boda hence watu hata kupata elfu kumi kwa siku imekuwa shughuli.., kwahio supply inabidi iendani na demand na Mipango miji haikupanga kila nyumba ya barabarani iwe frame imetokea tu kwa kuwa na sera mbovu hence watu kudhani tujaribu labda tuuze duka (fanya research ni biashara ngapi zinakufa baada ya mwaka kuanzishwa) au muulize mwenye nyumba kwa mwaka anapangisha watu tofauti wangapi huyu anakuja anajaribu kuuza pombe, mwingine anakuja anaweka betting kesho anakuja anaweza game la watoto ili mradi ni mzunguko usio na tija....
Kwa logic yako tuongeze hata vituo vya taksi, daladala na hata ikibidi kila mtu awe na duka sebuleni kwake ili asiende mbali... (ooh thinking about it kuna alternative ambayo ni simu yake aliyonayo mkononi)
Hivi unadhani wapanga miji huko wanapanga wakiwa under influence au wakiwa na kilevi kichwani ? Kwa taarifa yako wakipanga miji wanaona na kuweka huduma zote muhimu kwa wakazi ili kuleta convinience tena kipindi cha Post Office kulikuwa karibia na kila sehemu ya Makazi (mfano UK) kuna post office..., kila mitaa miwili kuna Corner shops n.k. (Lakini zote hizo zimekufa kifo cha kawaida kutokana na wakati; nani anatuma barua ?, Pia Supermarkets zinaweza zikaleta mpaka delivery though corner shops bado zipo.....
Wangekuwa wanaangalia urahisi wa huduma watu wasingehitajika kuendesha kwenda kufuata groceries. Sehemu kubwa, hasa Marekani, watu wanafanya hivyo. Ulaya si sana. Sisi huku kuwa na duka kila kona kila sehemu ni jambo zuri sana.
Unajua kitu kinaitwa A Broken Windows Fallacy ?!!!! Wewe unaweza kudhani mtoto kuvunja kioo anakuza uchumi sababu muuza mwenye kioo atanunua kipya ambacho kiwanda kitatengeneza kipya n.k. unasahau kwamba mwenye kioo huenda hizo pesa angenunulia viatu jambo ambalo hataacha kununua....
Hence mahitaji ya Binadamu ni Chakula, Malazi na Mavazi kama Chakula kitakuwa bei ndogo sana watu watapata disposable income ambayo huenda wakapeleka kwenye luxuries na vitu vingine...,
Chakula kikiwa bei ndogo sana wazalishaji wanaathirika. Kama jinsi wakulima nchini wanavyoathirika. Marekani na nchi za magharibi leo hii hazizalishi na watu wanakosa ajira sababu ya bidhaa za bei ndogo ambazo makampuni makubwa kama Amazon, Walmart na nk wanaingiza kutoka China nk. Bei ndogo inaweza kuwa hatari kubwa kwa uchumi.
Kama tumeongeza ufanisi kwenye maduka kwa kuweka wauzaji wachache wenye ufanisi, kwa nini tusifanye hivyo kwenye kilimo na sekta zingine unazotaka hao wauza mafukw waende!!? Mwisho wa siku tuwe na kama asilimia 10 hivi ya watu wanaofanya kazi na wengine watulie!!!!?
Lakini sijasikia mtu anasema tufundishe watu kuuza mitumba au Kuendesha Bodaboda sababu ndio ajira kubwa..., Au uchimbaji mdogo wa madini au Kuwa Makondakta kwenye Daladala.....
And ?!!!! Sijasema Mafunzo ya Bishara yafutwe kwenye mashule au itabidi nirudie nilichoandika sababu ninachoandika na unachojibu naona ni kama mbingu na ardhi !!!!
Wangekuwa wanaangalia urahisi wa huduma watu wasingehitajika kuendesha kwenda kufuata groceries. Sehemu kubwa, hasa Marekani, watu wanafanya hivyo. Ulaya si sana. Sisi huku kuwa na duka kila kona kila sehemu ni jambo zuri sana.
Kuwa na duka kila kona ni tofauti na kuwa na duka kila nyumba (hence corner shops).., Pili inategemea na sehemu kama mtu watu wanaishi kwenye mageti na wana magari na watu wapo nyumba kila baada ya masaa huenda ndio maana hata hakuna watu wanahangaika kuweka maduka (hakuna market).., By the way kama kuna uhaba wa maduka kwanini huko mtaani kwenu unakoishi USA usishauri kina Mangi wapeleke hao maduka huko.., Na kama Sheria ipo mtaa huo kusiwe na duka unaweza kuniambia kwanini ? (lazima hio sababu ina-make sense huwezi kuvunja nyumba ya kuishi ambazo zipo uniform uweke duka ila kama kuna need am sure unaweza kuongea na watu wa planning kwenye kona ya huo mtaa wako ukaweka duka....
Chakula kikiwa bei ndogo sana wazalishaji wanaathirika. Kama jinsi wakulima nchini wanavyoathirika. Marekani na nchi za magharibi leo hii hazizalishi na watu wanakosa ajira sababu ya bidhaa za bei ndogo ambazo makampuni makubwa kama Amazon, Walmart na nk wanaingiza kutoka China nk. Bei ndogo inaweza kuwa hatari kubwa kwa uchumi.
Kwahio ndio hapo tunakuja with machinery and automation soon human labor itakuwa haiitajiki..., kwahio cha kufanya ni vipi watu wanaweza kunufaika na faida ya uzalishaji huo ili wapate ujira (kuna watu hadi walisuggest universal pay which to me did not make sense sababu they more people are paid without working wazalishaji wangeongeza bei...; to me the only way forward ni sustainability make according to demand and work according to need na sio work for the sake of working.... Unaweza kupitia hii Riwaya inagusa Tatizo hili ambalo kwa sasa lipo Ulimwenguni due to automation....
Utangulizi Maisha matamu sana, haya ni maneno ambayo nisingeweza kuyatamka miaka ishirini iliyopita, sikujua cha maisha wala uzuri…, na si mimi tu wengi tulikuwa kwenye dhahama hizo… Nasogea kwenye bustani na kuketi napigwa na upepo mzuri naona wanafamilia wakitembea kutoka makwao kuelekea...
Kama tumeongeza ufanisi kwenye maduka kwa kuweka wauzaji wachache wenye ufanisi, kwa nini tusifanye hivyo kwenye kilimo na sekta zingine unazotaka hao wauza mafukw waende!!? Mwisho wa siku tuwe na kama asilimia 10 hivi ya watu wanaofanya kazi na wengine watulie!!!!?
Again huwezi ukasema tufanye au ufanye (human being sio Chess Pieces kwamba utawapeleka pale au hapa bali necessity, demand na circumstances zitafanya hivyo automatically, kusipokuwepo na infrastructure ya kuwasaidia wengi kwa faida ya wengi wachache watachukua opportunity ya kufanya kitu kwa ufanisi ambapo hii gap ya wealthy itaendelea kuongezeka na mwisho wa siku kuwa a Threat to Human Civilization (Extreme Poverty Anywhere is a Threat to Humankind Everywhere)....
Unaongelea kwenye Kilimo ofcourse na kule kuna machinery na combined harvester hatuhitaji wote kushika jembe la mkono (nimesema waende kule sababu kwa sasa huenda kuna more need; Chakula bado bei ya juu kuliko kipato cha watu)..., ila mwisho wa siku kazi ambazo binadamu anaweza kuzifanya vizuri ni hospitality, care na creativity (huku pengine sababu ingekuwa kufanya tu jambo ili watu walipwe basi tungekuwa tunachimba shimo jtatu watu walipwe jnne walizibe walipwe na jtano wachimbe walipwe and so forth....
Ulishawahi kujiuliza kwanini tunafanya kazi ? Kwamba sababu huenda jembe la mkono linasaidia wau wengi zaidi kufanya kazi tusitumie tractor au combined harvester ?
Huo muda wa Mom & Pop kuuza kitu ambacho Supermarket pia kipo (economy of scale) wangetumia muda huo labda kutengeneza home made (sababu kama wanatoa convinience, kina amazon do it better)...., The tide is coming Gen Z hawana muda wa shopping ni mwendo wa online...,. Ingawa huku hatujafika sawa lakini sio tuwekeze kwenye jambo ambalo kesho halina tija....; Ni sawasawa leo unamfundisha mtoto kutumia Four Figure Table au kujumlisha na kutoa kwa kutumia Roman Numerals....; unless unafanya kama hobbie
Ndio hapo kaka mtaani noma na pataendelea kuwa Noma..., Na hii sio kwa Sera mbovu tu bali ji mabadiliko ya Kimfumo / Kidunia ni kama enzi za Industrial Revolution zilivyomaliza Utumwa ndio sasa hivi Technology na Automation imefanya nguvu kazi kutokuhitajika kabisa..., Kwahio Sio Bongo tu kama Dunia inabidi mfumo ubadilike sababu Capitalism na Accumulation of Wealth inatengeneza Matabaka makubwa ya Matajiri wachache sana na Mafukara wengi sana hence Civilization Stability ipo kwenye Mashaka..... Tutegemee things will get worse before they get better...
Tusi-justify bad planning na un-sustainability na divinity ya aina yoyote ile kama tungejifunza kutoka Nature au Viumbe kama Nyuki sidhani kama tungekuwa na hii inefficiency....
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.