Waache watu waanzishe. Zitakazo kufa na zife. Waache bodaboda. Wakiona hazilipi wataacha.
Who said Otherwise ?!!!!!
Lakini sijasikia mtu anasema tufundishe watu kuuza mitumba au Kuendesha Bodaboda sababu ndio ajira kubwa..., Au uchimbaji mdogo wa madini au Kuwa Makondakta kwenye Daladala.....
Akiwa na anauza online bado atahitaji sehemu ya kuweka bidhaa. Usiongee kama vile bidhaa zinazouzwa mtandaoni zinapita kwenye mtandao!!
And ?!!!! Sijasema Mafunzo ya Bishara yafutwe kwenye mashule au itabidi nirudie nilichoandika sababu ninachoandika na unachojibu naona ni kama mbingu na ardhi !!!!
Wangekuwa wanaangalia urahisi wa huduma watu wasingehitajika kuendesha kwenda kufuata groceries. Sehemu kubwa, hasa Marekani, watu wanafanya hivyo. Ulaya si sana. Sisi huku kuwa na duka kila kona kila sehemu ni jambo zuri sana.
Kuwa na duka kila kona ni tofauti na kuwa na duka kila nyumba (hence corner shops).., Pili inategemea na sehemu kama mtu watu wanaishi kwenye mageti na wana magari na watu wapo nyumba kila baada ya masaa huenda ndio maana hata hakuna watu wanahangaika kuweka maduka (hakuna market).., By the way kama kuna uhaba wa maduka kwanini huko mtaani kwenu unakoishi USA usishauri kina Mangi wapeleke hao maduka huko.., Na kama Sheria ipo mtaa huo kusiwe na duka unaweza kuniambia kwanini ? (lazima hio sababu ina-make sense huwezi kuvunja nyumba ya kuishi ambazo zipo uniform uweke duka ila kama kuna need am sure unaweza kuongea na watu wa planning kwenye kona ya huo mtaa wako ukaweka duka....
Chakula kikiwa bei ndogo sana wazalishaji wanaathirika. Kama jinsi wakulima nchini wanavyoathirika. Marekani na nchi za magharibi leo hii hazizalishi na watu wanakosa ajira sababu ya bidhaa za bei ndogo ambazo makampuni makubwa kama Amazon, Walmart na nk wanaingiza kutoka China nk. Bei ndogo inaweza kuwa hatari kubwa kwa uchumi.
Kwahio ndio hapo tunakuja with machinery and automation soon human labor itakuwa haiitajiki..., kwahio cha kufanya ni vipi watu wanaweza kunufaika na faida ya uzalishaji huo ili wapate ujira (kuna watu hadi walisuggest universal pay which to me did not make sense sababu they more people are paid without working wazalishaji wangeongeza bei...; to me the only way forward ni sustainability make according to demand and work according to need na sio work for the sake of working.... Unaweza kupitia hii Riwaya inagusa Tatizo hili ambalo kwa sasa lipo Ulimwenguni due to automation....
Utangulizi Maisha matamu sana, haya ni maneno ambayo nisingeweza kuyatamka miaka ishirini iliyopita, sikujua cha maisha wala uzuri…, na si mimi tu wengi tulikuwa kwenye dhahama hizo… Nasogea kwenye bustani na kuketi napigwa na upepo mzuri naona wanafamilia wakitembea kutoka makwao kuelekea...
Kama tumeongeza ufanisi kwenye maduka kwa kuweka wauzaji wachache wenye ufanisi, kwa nini tusifanye hivyo kwenye kilimo na sekta zingine unazotaka hao wauza mafukw waende!!? Mwisho wa siku tuwe na kama asilimia 10 hivi ya watu wanaofanya kazi na wengine watulie!!!!?
Again huwezi ukasema tufanye au ufanye (human being sio Chess Pieces kwamba utawapeleka pale au hapa bali necessity, demand na circumstances zitafanya hivyo automatically, kusipokuwepo na infrastructure ya kuwasaidia wengi kwa faida ya wengi wachache watachukua opportunity ya kufanya kitu kwa ufanisi ambapo hii gap ya wealthy itaendelea kuongezeka na mwisho wa siku kuwa a Threat to Human Civilization (Extreme Poverty Anywhere is a Threat to Humankind Everywhere)....
Unaongelea kwenye Kilimo ofcourse na kule kuna machinery na combined harvester hatuhitaji wote kushika jembe la mkono (nimesema waende kule sababu kwa sasa huenda kuna more need; Chakula bado bei ya juu kuliko kipato cha watu)..., ila mwisho wa siku kazi ambazo binadamu anaweza kuzifanya vizuri ni hospitality, care na creativity (huku pengine sababu ingekuwa kufanya tu jambo ili watu walipwe basi tungekuwa tunachimba shimo jtatu watu walipwe jnne walizibe walipwe na jtano wachimbe walipwe and so forth....