SoC02 Elimu ya Mahusiano ianze kutolewa shuleni

Stories of Change - 2022 Competition

ReTHMI

Senior Member
Joined
Jul 17, 2022
Posts
181
Reaction score
323
Wengi watapigwa na butwaa kwanini natamani elimu ya mahusiano itolewe mashuleni tena mahusiano ya kimapenzi. Nitabaki kusimamia kwamba elimu ya mahusiano ya kimapenzi itolewe mashuleni, ikiwezekana kama somo la lazima kuanzia ngazi ya elimu ya msingi mpaka elimu ya sekondari.

Elimu inatakiwa isaidie katika kupambana na matatizo yanayoikumba jamii. Katika jamii zetu mahusiano yanasababisha madhara kila uchwao na kuvipamba vichwa vya habari kwenye vyombo vya habari na mitandao. Imefikia hatua watu wanaweka mzaha kwenye matukio ambayo yamegharimu maisha ya watu. Ila cha kusikitisha hakuna nguvu inayoelekezwa katika kulitafutia ufumbuzi tatizo hili.

Zama zilizopita vijana walifunzwa jinsi ya kuishi kwenye ndoa na kutimiza majukumu yao kwenye familia kupitia jando na unyago. Zama hizi utamaduni huu umekufa, tumeshindwa kuendeleza kwa kuboresha mazuri na kuyaacha mabaya yaliyokua yanafanyika kwenye jando na unyago.

Ukosefu wa elimu ya mahusiano unapelekea jamii kukumbana na athari nyingi zitokanazo na mahusiano;
Watu wanakufa, wanauwawa na wenza wao au watu wengine kutokana na wivu wa mapenzi.

Ukatili wa kijinsia umeongezeka maradufu kwenye ndoa na mahusiano. Watu wanapata ulemavu kutokana na vipigo na kushambuliwa na wenza wao.

Magonjwa ya ngono, watoto wa mitaani, utoaji wa mimba, mimba katika umri mdogo, watoto kulelewa na mzazi mmoja (single mother) yote haya yanaongezeka kila uchwao.

Afya ya akili imedorora miongoni mwa watu wengi, wameathirika kisaikolojia kutokana na maumivu waliyopitia/wanayopitia kwenye mahusiano hali inayopelekea wengine kuwehuka kabisa.

Takwimu za kwenye chapisho la BBC la tarehe 1 Juni 2022 zinabainisha;
Kituo cha Sheria na haki za binadamu nchini Tanzania, LHRC, kwa mwaka 2017, kilikusanya matukio makubwa 13 na mwaka 2020 matukio yaliongezeka mpaka 39 yaliyotokana na wivu wa kimapenzi. Lakini kituo hicho kinasema mwezi Mei pekee mwaka huu (2022), kumeripotiwa matukio 7 ya mauaji yatokanayo na wivu wa kimapenzi huku mwaka 2021 kuliripotiwa kuwa na mauaji ya ina hiyo 35, ambapo wanaume waliouawa walikuwa 4 na wanawake 31 sawa na asilimia 89%.
Pia katika chapisho la DW la tarehe 24/01/2022, linalozungumzia kuhusiana na ukatili wa kijinsia linaonyesha;
Ripoti iliyotolewa Septemba 2021 na Jarida la Afrika kuhusu hali ya ukatili wa kijinsia Tanzania miongoni mwa wanandoa, imeonyesha kuwa, asilimia 46 ya wanandoa hufanyiwa ukatili wa kijinsia, ambapo asilimia 36 walifanyiwa ukatili wa kimwili na asilimia 32 walifanyiwa ukatili wa kisaikolojia na asilimia 13 walifanyiwa ukatili wa kingono.
Kwenye suala la mimba na ndoa za utotoni zinashuhudiwa pia katika jamii zetu ikiwemo kupelekea watoto kukatiza masomo yao. Kwa mujibu wa takwimu za Unicef za kati ya mwaka 2010 na 2017;
Tanzania ni ya tatu kwa kuwa na viwango vya juu vya ndoa za utotoni baada ya Sudan Kusini na Uganda. Sudan Kusini kiwango cha watoto wa chini ya miaka 18 wanaoozwa ni asilimia 52 na nchini Uganda ni asilimia 40 na Tanzania ni asilimia 31.
Kwa upande wa maambukizi ya UKIMWI Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS), Dk. Leonard Maboko mei 19,2022 alibainisha kuwa,
“Hali ya maambukizi ya UKIMWI nchini Tanzania inaonyesha kuwa kama nchi tunapiga hatua kubwa, makadirio ya takwimu kwa mwaka 2021 yanaonyesha kwamba maambukizi mapya ni watu 54,000 kwa mwaka huku, upande wa vifo vimeshuka kutoka watu 32,000 mwaka 2020 hadi watu 29,000 mwaka 2021” (Chanzo cha habari, Mtanzania digital).
Inaonekana maambukizi mapya ya UKIMWI yameshuka ila bado ni mengi. Kwa asilimia kubwa maambukizi ya UKIMWI yanatokana kushiriki ngono zembe mbali na njia nyingize zinachochangia maambukizi kwa asilimia chache.

Kupitia takwimu hizi chache inaonyesha ni jinsi gani jamii inahitaji msaada wa dharura na wa muda mrefu ili kutengeneza msingi imara utakaosaidia kuimarisha mahusiano ya mapenzi. Wengi huchukulia kawaida na hata kuweka utani pale wengine wanapokumbana na madhara yatokanayo na mahusiano ya mapenzi. Ila wanashindwa kuyakwepa yanapowafika wao kutokana na ukosefu wa elimu ya mahusiano.

Hivyo basi, kutolewa kwa elimu ya mahusiano shuleni itasaidia kwa kiasi kikubwa kupambana na tatizo hili. Hii ni kutokana na watu wengi pindi wanapomaliza elimu yao hupuuzia kujifunza mambo mapya, hata zinapoandaliwa semina mbalimbali ushiriki ni hafifu sana.

Wapo wanaochukulia kumfundisha mtoto juu ya mahusiano ya kimapenzi ni kumharibu kabisa mtoto. Zipo njia nzuri na zinazofaa kumfundisha mtoto juu ya mahusiano ya kimapenzi ambazo ni tofauti na zile zitakazotumiaka kumfundisha mtu mzima. Watoto pia wanahitaji elimu hii kwasababu nao pia ni waathiriwa wakubwa wa mahusiano ya kimapenzi. Ikiwemo kukatiziwa masomo yao kutokana na mimba na ndoa za utotoni. Ila pia kupitia michezo yao watoto hucheza michezo ambayo huigiza kama familia inadhihirisha ni jinsi gani nao wanahitaji elimu hii ya mahusiano kwakua nao wanayashuudia yanayotendeka kwenye jamii zao hali inayopelekea kuyaakisi wanapokua watu wazima.

Elimu ya mahusiano ikitolewa mashuleni itapunguza vifo vitokanavyo na wivu wa kimapenzi na ukatili wa kijinsia. Hii ni kwasababu watu watafundishwa uaminifu kwenye mahusiano, na uaminifu utapunguza migogoro kwenye mahusiano. Ila pia wataweza kutambua yapi ni mahusiano sahihi na yapi sio sahihi. Watatambua njia za kutumia kutatua migogoro kwenye mahusiano bila kumuumiza mwingine.

Itasaidia kupunguza maambukizi wa UKIMWI kutokana na ngono zembe. Watu wengi wanaingia kwenye mahusiano bila kupima virusi vya UKIMWI, wakiamini kwamba kua na afya nzuri basi mtu hana maambukizi ya UKIMWI. Elimu hii itawasaidia kutambua kwamba UKIMWI haupimwi kwa macho, mtu anaweza akaonekana mzuri kiafya ila ana maambukizi hivyo ni vyema kutumia njia zitakazomkinga. Pia itasaidia watu kuwa waaminifu kwenye mahusiano ikiwemo kutokua na michepuko.

Elimu ya mahusiano ikitolewa vizuri shuleni itawasaidia pia wanafunzi kutimiza malengo yao ya kimasomo. Hasahasa kwa upande wa wanafunzi wa kike wanaokatiza masomo yao kutokana na mimba na ndoa za utotoni. Hii ni kwa sababu wanafunzi watatambua ni kwa namna gani mahusiano ya kimapenzi yanavyoweza kuathiri masomo. Pia wataelekezwa ni wakati upi sahihi wa kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Mwisho kabisa, nipende kusema ni bora kutatua tatizo kwa kulishughulikia kuliko kuacha tatizo litutafune kwa kulionea aibu. Ni dhairi kua japokua mahusiano ya kimapenzi yanachangamoto nyingi sana ila hakuna maisha bila mahusiano ya kimapenzi. Ili kupunguza changamoto hizi basi serikali ikae na itafakari kwa kina ni kwa namna gani iliyo bora wanaweza kuandaa somo kuhusu mahusiano litakalofundishwa shuleni. Hii ni kwa minajili tu ya kulikomboa taifa kutokana na nguvu kazi zinazopotea kutokana na mahusiano ya kimapenzi.
 
Upvote 341
Wengi watapigwa na butwaa kwanini natamani elimu ya mahusiano itolewe mashuleni tena mahusiano ya kimapenzi. Nitabaki kusimamia kwamba elimu ya mahusiano ya kimapenzi itolewe mashuleni, ikiwezekana kama somo la lazima kuanzia ngazi ya elimu ya msingi mpaka elimu ya sekondari.

Elimu inatakiwa isaidie katika kupambana na matatizo yanayoikumba jamii. Katika jamii zetu mahusiano yanasababisha madhara kila uchwao na kuvipamba vichwa vya habari kwenye vyombo vya habari na mitandao. Imefikia hatua watu wanaweka mzaha kwenye matukio ambayo yamegharimu maisha ya watu. Ila cha kusikitisha hakuna nguvu inayoelekezwa katika kulitafutia ufumbuzi tatizo hili.

Zama zilizopita vijana walifunzwa jinsi ya kuishi kwenye ndoa na kutimiza majukumu yao kwenye familia kupitia jando na unyago. Zama hizi utamaduni huu umekufa, tumeshindwa kuendeleza kwa kuboresha mazuri na kuyaacha mabaya yaliyokua yanafanyika kwenye jando na unyago.

Ukosefu wa elimu ya mahusiano unapelekea jamii kukumbana na athari nyingi zitokanazo na mahusiano;
Watu wanakufa, wanauwawa na wenza wao au watu wengine kutokana na wivu wa mapenzi.

Ukatili wa kijinsia umeongezeka maradufu kwenye ndoa na mahusiano. Watu wanapata ulemavu kutokana na vipigo na kushambuliwa na wenza wao.

Magonjwa ya ngono, watoto wa mitaani, utoaji wa mimba, mimba katika umri mdogo, watoto kulelewa na mzazi mmoja (single mother) yote haya yanaongezeka kila uchwao.

Afya ya akili imedorora miongoni mwa watu wengi, wameathirika kisaikolojia kutokana na maumivu waliyopitia/wanayopitia kwenye mahusiano hali inayopelekea wengine kuwehuka kabisa.

Takwimu za kwenye chapisho la BBC la tarehe 1 Juni 2022 zinabainisha;

Pia katika chapisho la DW la tarehe 24/01/2022, linalozungumzia kuhusiana na ukatili wa kijinsia linaonyesha;

Kwenye suala la mimba na ndoa za utotoni zinashuhudiwa pia katika jamii zetu ikiwemo kupelekea watoto kukatiza masomo yao. Kwa mujibu wa takwimu za Unicef za kati ya mwaka 2010 na 2017;

Kwa upande wa maambukizi ya UKIMWI Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS), Dk. Leonard Maboko mei 19,2022 alibainisha kuwa,

Inaonekana maambukizi mapya ya UKIMWI yameshuka ila bado ni mengi. Kwa asilimia kubwa maambukizi ya UKIMWI yanatokana kushiriki ngono zembe mbali na njia nyingize zinachochangia maambukizi kwa asilimia chache.

Kupitia takwimu hizi chache inaonyesha ni jinsi gani jamii inahitaji msaada wa dharura na wa muda mrefu ili kutengeneza msingi imara utakaosaidia kuimarisha mahusiano ya mapenzi. Wengi huchukulia kawaida na hata kuweka utani pale wengine wanapokumbana na madhara yatokanayo na mahusiano ya mapenzi. Ila wanashindwa kuyakwepa yanapowafika wao kutokana na ukosefu wa elimu ya mahusiano.

Hivyo basi, kutolewa kwa elimu ya mahusiano shuleni itasaidia kwa kiasi kikubwa kupambana na tatizo hili. Hii ni kutokana na watu wengi pindi wanapomaliza elimu yao hupuuzia kujifunza mambo mapya, hata zinapoandaliwa semina mbalimbali ushiriki ni hafifu sana.

Wapo wanaochukulia kumfundisha mtoto juu ya mahusiano ya kimapenzi ni kumharibu kabisa mtoto. Zipo njia nzuri na zinazofaa kumfundisha mtoto juu ya mahusiano ya kimapenzi ambazo ni tofauti na zile zitakazotumiaka kumfundisha mtu mzima. Watoto pia wanahitaji elimu hii kwasababu nao pia ni waathiriwa wakubwa wa mahusiano ya kimapenzi. Ikiwemo kukatiziwa masomo yao kutokana na mimba na ndoa za utotoni. Ila pia kupitia michezo yao watoto hucheza michezo ambayo huigiza kama familia inadhihirisha ni jinsi gani nao wanahitaji elimu hii ya mahusiano kwakua nao wanayashuudia yanayotendeka kwenye jamii zao hali inayopelekea kuyaakisi wanapokua watu wazima.

Elimu ya mahusiano ikitolewa mashuleni itapunguza vifo vitokanavyo na wivu wa kimapenzi na ukatili wa kijinsia. Hii ni kwasababu watu watafundishwa uaminifu kwenye mahusiano, na uaminifu utapunguza migogoro kwenye mahusiano. Ila pia wataweza kutambua yapi ni mahusiano sahihi na yapi sio sahihi. Watatambua njia za kutumia kutatua migogoro kwenye mahusiano bila kumuumiza mwingine.

Itasaidia kupunguza maambukizi wa UKIMWI kutokana na ngono zembe. Watu wengi wanaingia kwenye mahusiano bila kupima virusi vya UKIMWI, wakiamini kwamba kua na afya nzuri basi mtu hana maambukizi ya UKIMWI. Elimu hii itawasaidia kutambua kwamba UKIMWI haupimwi kwa macho, mtu anaweza akaonekana mzuri kiafya ila ana maambukizi hivyo ni vyema kutumia njia zitakazomkinga. Pia itasaidia watu kuwa waaminifu kwenye mahusiano ikiwemo kutokua na michepuko.

Elimu ya mahusiano ikitolewa vizuri shuleni itawasaidia pia wanafunzi kutimiza malengo yao ya kimasomo. Hasahasa kwa upande wa wanafunzi wa kike wanaokatiza masomo yao kutokana na mimba na ndoa za utotoni. Hii ni kwa sababu wanafunzi watatambua ni kwa namna gani mahusiano ya kimapenzi yanavyoweza kuathiri masomo. Pia wataelekezwa ni wakati upi sahihi wa kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Mwisho kabisa, nipende kusema ni bora kutatua tatizo kwa kulishughulikia kuliko kuacha tatizo litutafune kwa kulionea aibu. Ni dhairi kua japokua mahusiano ya kimapenzi yanachangamoto nyingi sana ila hakuna maisha bila mahusiano ya kimapenzi. Ili kupunguza changamoto hizi basi serikali ikae na itafakari kwa kina ni kwa namna gani iliyo bora wanaweza kuandaa somo kuhusu mahusiano litakalofundishwa shuleni. Hii ni kwa minajili tu ya kulikomboa taifa kutokana na nguvu kazi zinazopotea kutokana na mahusiano ya kimapenzi.
Wenye kuelewa tumeelewa, naungana na wewe kwenye hili
 
Hongera ReTHMI kwa andiko lako..naomba nikuulize, unadhani kila tatizo linalotokea kwenye jamii ni matokeo ya kutokuwa na mafunzo? Lengo hasa la elimu ni nini, kwa mfano hesabu anazofundishwa mtoto kutoka darasa la kwanza hadi la Saba lengo lake ni nini? Je sheria za shule zinazomkataza mtoto kujihusisha na mahusiano ya mapenzi lakini hata maonyo ya wazazi, viongozi wa kiimani na walezi juu ya jambo hili hayatoshi? Tena yana adhabu pale mtoto anapokiuka alichoelekezwa..ni sawa kila linalotokea kwenye jamii lenye madhara ya kifo au kuumizwa lazima liwe na mafunzo?
 
Shukrani kwa mchango wako wa maswali, naomba nikujibu kama ifuatavyo;
1. Sio kila tatizo linalotokea kwenye jamii ni matokeo ya kutokua na mafunzo, ila matatizo mengi yanayoikumba jamii yanatokana na jamii kukosa uelewa mzuri juu ya jambo husika

2. Lengo la elimu ni kumpa uelewa mtu kuhusiana na jambo fulani, kama ni hesabu basi ni kwaajili ya kumpa mtoto uelewa wa hesabu. Lakini pia kwa baadhi ya nchi elimu inatumika katika kutatua changamoto mbalimbali kwenye jamii, tofauti na Tanzania ambapo kwa kiasi kikubwa elimu inaonekana kama ni kwaajili ya kumsaidia mtu kupata kazi nzuri kwa maisha ya baadae.

3. Kwenye upande wa sheria, hapo mtoto anakatazwa tu ila hapewi elimu ya mahusiano, kwaiyo ataogoga kujihusisha na mahusiano kwa sababu ya uoga wa kuadhibiwa na sio kutokana na uelewa wa madhara ya mahusiano kwa wakati huo. Pia atafanya kwa siri kwakua anajua asipogundulika hataadhibiwa mwisho wake anapata madhara kama ujauzito akiwa bado shuleni na magonjwa ya zinaa. Kwa maana hiyo basi adhabu na sheria hizo hazitoshi kuepusha madhara yatokanayo na mahusiano.

Na hili linathibitika hasa pale mwanafunzi anapohitimu elimu yake ya sekondari ama msingi na kuingia mtaani au vyuoni. Vyuoni wanapata uhuru, hakuna tena wa kumkataza, hakuna tena adhabu hata ikigundulika ana mahusiano ya kimapenzi. Hapa sasa ndipo wanapofungulia koki, basi ataingia mzimamzima kwenye mahusiano bila kujali mimba zisizotarajiwa wala magonjwa ya zinaa.

Ukiangalia wanawake wanaoenda vyuoni wengi wao hurudi na watoto au ujauzito, ukiachana na magonjwa ya zinaa na waliotoa mimba vyuoni ambavyo hufanywa siri. Hapa nadhani utakubaliana na mimi hili limetokana na ukosefu wa uelewa kwenye suala zima la mahusiano.

Madhara ya kukosa uelewa wa mahusiano yapo mengi sana ikiwemo watoto wadogo wa kiume na wa kike kurubuniwa na kupelekea kunajisiwa. Lakini kama mtoto huyo angefundishwa kwamba kitu hiki sio sawa kwa sababu hii na hii, ikitokea mtu akakushawishi kufanya basi chukua hatua hizi, naamini visa hivi vingepungua kwa kiasi kikubwa.
Natumaini utakua umenielewa, ila pia ambapo hujaelewa usisite kusema pia ningependa kupata maoni yako juu ya hili.
 
Andiko zuri serikali kweli inatakiwa kutazama mtahala wa elimu kwa mara nyingine tena sasaivi mabadiliko ni makubwa na elimu hii ni muhimu kama tunakusudia kuwa na vijana wenye afya ya akili na mwili pia. kura yangu nakupa
 
Nafikiri mafunzo ni muhimu kwani bado wengi wanafanya kwa kutokuelewa mambo kwa undani. Watoto wakati mwingine wanaona maelekezo ya wazazi ni kama kuwazuia tuu na kitu kisicho na madhara yoyote kutokana na hofu na hivyo wengi hupuuzia lakini elimu ya undani na usahihi zaidi inaweza kutolewa shuleni. Ninafikiri kila kinacholeta hatima mbaya kwenye jamii kinahitaji kufundishwa angalau kutakua na kiasi cha watakaojilinda kutokana na elimu walio ipata japo lazima tutaendela kuwa na kundi la wakaidi au wajinga lakni haitakuwa kama wakati huu elimu ikiwa bado inahitajika. Karibu pia kwenye andiko nitafurahi kuona maoni yako
 
Andiko zuri serikali kweli inatakiwa kutazama mtahala wa elimu kwa mara nyingine tena sasaivi mabadiliko ni makubwa na elimu hii ni muhimu kama tunakusudia kuwa na vijana wenye afya ya akili na mwili pia. kura yangu nakupa
Shukrani sana
 
Shukrani kwa mchango wako wa maswali, naomba nikujibu kama ifuatavyo;
1. Sio kila tatizo linalotokea kwenye jamii ni matokeo ya kutokua na mafunzo, ila matatizo mengi yanayoikumba jamii yanatokana na jamii kukosa uelewa mzuri juu ya jambo husika

2. Lengo la elimu ni kumpa uelewa mtu kuhusiana na jambo fulani, kama ni hesabu basi ni kwaajili ya kumpa mtoto uelewa wa hesabu. Lakini pia kwa baadhi ya nchi elimu inatumika katika kutatua changamoto mbalimbali kwenye jamii, tofauti na Tanzania ambapo kwa kiasi kikubwa elimu inaonekana kama ni kwaajili ya kumsaidia mtu kupata kazi nzuri kwa maisha ya baadae.

3. Kwenye upande wa sheria, hapo mtoto anakatazwa tu ila hapewi elimu ya mahusiano, kwaiyo ataogoga kujihusisha na mahusiano kwa sababu ya uoga wa kuadhibiwa na sio kutokana na uelewa wa madhara ya mahusiano kwa wakati huo. Pia atafanya kwa siri kwakua anajua asipogundulika hataadhibiwa mwisho wake anapata madhara kama ujauzito akiwa bado shuleni na magonjwa ya zinaa. Kwa maana hiyo basi adhabu na sheria hizo hazitoshi kuepusha madhara yatokanayo na mahusiano.

Na hili linathibitika hasa pale mwanafunzi anapohitimu elimu yake ya sekondari ama msingi na kuingia mtaani au vyuoni. Vyuoni wanapata uhuru, hakuna tena wa kumkataza, hakuna tena adhabu hata ikigundulika ana mahusiano ya kimapenzi. Hapa sasa ndipo wanapofungulia koki, basi ataingia mzimamzima kwenye mahusiano bila kujali mimba zisizotarajiwa wala magonjwa ya zinaa.

Ukiangalia wanawake wanaoenda vyuoni wengi wao hurudi na watoto au ujauzito, ukiachana na magonjwa ya zinaa na waliotoa mimba vyuoni ambavyo hufanywa siri. Hapa nadhani utakubaliana na mimi hili limetokana na ukosefu wa uelewa kwenye suala zima la mahusiano.

Madhara ya kukosa uelewa wa mahusiano yapo mengi sana ikiwemo watoto wadogo wa kiume na wa kike kurubuniwa na kupelekea kunajisiwa. Lakini kama mtoto huyo angefundishwa kwamba kitu hiki sio sawa kwa sababu hii na hii, ikitokea mtu akakushawishi kufanya basi chukua hatua hizi, naamini visa hivi vingepungua kwa kiasi kikubwa.
Natumaini utakua umenielewa, ila pia ambapo hujaelewa usisite kusema pia ningependa kupata maoni yako juu ya hili.
Asante ReTHMI kwanza kujali sana suala la malezi kwa vijana, ninaliona hili between the lines..labda niongeze kdg, mimi ninaona shida iko kwa sisi wazazi na walezi na tusihamishe jukumu letu la msingi kwenda kwa walimu, wajibu walio nao unatosha pengine hata umewazidi, suala la tabia na mwenendo wa watoto na vijana ni jukumu la wazazi na walezi, mwalimu hapaswi kutumia muda mwingi kufundisha watoto au vijana kuhusu tabia zao..mwalimu anajenga kwenye msingi ambao mzazi/mlezi ameweka tayari kwa mtoto, shule ya kwanza kwa mtoto ni nyumbani anapoishi..niseme kitu hapa, zawadi pekee ya thamani ambayo mzazi/mlezi anapaswa kumpa mtoto au kijana wake..si elimu au pesa au urithi, ni jinsi yeye mzazi/mlezi alivyo..upendo, nidhamu, wajibu, huruma nk haya ndio yanaumba kitu ndani ya mtoto au kijana vile ataishi na jamii mbali na wazazi/walezi wake..na kwa upande wa elimu lengo ni kumpa mtoto MAARIFA/KNOWLEDGE ili imsaidie kukabiliana na yanayokuja mbele yake ikiwamo namna ya kutatua migogoro yoyote hata ya mahusiano! mwenye maarifa anajua pa kwenda kupata ushauri anapolemewa na tatizo, anajua wapo wakumsaidia kwa lolote akitaka, viongozi wa imani, walimu, watu waliomzidi umri nk..wapo hivyo haihitaji mafunzo maalum kwa ajili ya mahusiano!
Pengine serikali inapaswa kuwa bunifu wasiunde wizara kwa mazoea tu kwamba kila serikali lazima wizara fulani fulani ziwepo hata kama ha,ina msaada kwa jamii kulingana na wakati ulivyo..kwa mfano kwa sasa inahitajika kabisa iwepo wizara ya mambo ya familia na malezi ili ziwepo sheria na kanuni na miongozo vile tunataka jamii yetu ikae kwa amani na umoja kama ndugu..mfano ziwepo sheria kijana akipata mtoto nje ya ndoa vyovyote iwavyo anawajibika 100% kwa malezi ya mtoto be it ana kazi au hana kazi, sheria itamlazimisha atunze mtoto hata kwa kifungo cha nje kupitia kufanya kazi kwa kulipwa ujira nk hatuwezi kuwa taifa lenye mwelekeo kama kila mmoja anafanya atakavyo na hakuna uwajibikaji wa hayo anayofanya..lazima kuwe na order katika kila hatua ya maisha yetu kama jamii..nadhani unaelewa ninachojaribu kujenga, yapo mengi..lakini hongera kwa hicho ulichotushirikisha ReTHMI.
 
Umegusia mengi, ila nikujibu tu kwa uchache,
Unaposema sheria ziwepo (kwa nijuavyo sheria zipo juu ya hili) zitakazombana kijana akipata mtoto nje ya ndoa kwanini tusifikirie kuepusha kijana kupata mtoto nje ya ndoa, kwa kumpa elimu mapema ili kuzuia mtoto kuja kulelewa na mzazi mmoja.

Lengo langu ni tuepushe hiyo migogoro kwenye mahusiano kabla ya kufikiria kwenda kuitatua kupitia watu wengine pindi inapotokea, tupambana kuzuia tatizo lisitokee na sio kusubiria litokee ndio tupambane kulitatua.

Ninaposema elimu itolewe shuleni simaanishi labda mwalimu anayefundisha hesabu akafundishe suala la mahusiano, hapana! Namaanisha waalimu watakaohusika kutoa hii elimu watakua ni wataalamu wa jambo husika, waliosomea na wenye maarifa ya kutosha juu ya mahusiano ya mapenzi.

Pia napenda kukufahamisha tu, watoto wengi wa kitanzania wanatumia muda mwingi shuleni kuliko nyumbani, nyumbani sana sana muda mwingi ni kulala (usiku). Pia wapo watoto wanaoanza shule za bweni kuanzia chekechea (na huku ndipo wanapokumbana na majanga kutokana na hawana ufahamu wowote juu ya mahusiano). Wazazi wengine hawana muda kabisa wa kukaa na watoto wao, kutokana na kubanwa na kazi au sababu nyinginezo zisizo na msingi. Ni kwanini suala hili lisiingizwe shuleni kusaidia haya.

Pia unaposema wazazi waachiwe jukumu hili, nadhani hata sasa hivi wao ndio wenye jukumu lakini bado tunashuhudia matatizo lukuki yanayotokana na mahusiano ya mapenzi. Huenda nao hawana uelewa, kwanini wasisaidiwe na shule zilizopo?

Pia unapowaongelea wazazi, nikufahamishe pia unaongelea aina hii ya wazazi
1. Wazazi wanaopiga au kupigwa na mke/mume wake mbele ya watoto wake
2. Wazazi wanaoonyesha dharau kwa mke/mume wake mbele ya watoto wake
3. Wazazi wenye michepuko wengine zaidi hata ya michepuko watatu
4. Wazazi wanaoshinda baa hawajui mtoto anavaa nini au anakula nini
5. Masingle mother na masingle father ilihali wazazi wenza wapo hai
6. Wazazi wanaoozesha watoto wao wa kike wakiwa bado wadogo kwa tamaa ya pesa au ng'ombe
7.Wazazi wanaowashawishi mtoto wao atoe ujauzito
8. Wazazi wanaoanika picha zao za utupu mitandaoni (Uhalisia tizama wanaojiita masupa star)
9. Wazazi (baba) waliokana ujauzito wao na wazazi (mama) waliobambikia watoto kwa baba wasio halisi.
10. Wazazi wanaotelekeza watoto wao na hata familia

Kwa ufupi tu ni kwamba wazazi kama hao wataweza vipi kuelimisha watoto wao juu ya suala nyeti kama hili kama sio kumdidimizia mtoto shimoni kabisa, ndio maana tunazidi kushuhudia matatizo kila siku.

Na ndio maana hata zamani waliliona hili wakaweka wataalamu waliokua wanafundisha jando na unyago na sio kuwaachia wazazi. Na hii ilisaidia sana japo kuna mambo machache yasiyofaa yalikua yanatendeka. Ila mke alijua kumuheshimu mume na mume alijua kumuheshimu mke wake.

Ukiangalia pia nchi kama Marekani, baadhi ya nchi za ulaya na asia wanafundisha 'sex education' shuleni na ipo kisheria kabisa, wameona tatizo lilipo kwaiyo wanajitahidi kuliepuka kwa namna hiyo.

Kuendelea kuchukulia poa haya mambo ndivyo tunavyozidi kushuhudia mambo ya ajabu kila kukicha kwenye jamii zetu, kisababishi mahusiano ya mapenzi.

Nashukuru kwa mchango wako TrueVoter, lakini ni vyema tukalitilia mkazo zaidi ya hapa.
 
ReTHMI si kila jambo ili kuliepuka ni kutoa elimu, mwisho utasema hata wezi na vibaka au panyaroad wanahitaji elimu sijui ya namna gani ili wasifanye uhalifu..huko ni kupoteza muda na resources bure! nilisema awali elimu hii tunayopata kuanzia shule ya msingi, sekondari nk inampa mtu maarifa ya kukabiliana na mazingira yanayomzunguka ikiwemo migogoro ya mahusiano! Nikasema mwenye maarifa anafahamu nini cha kufanya anapopatwa na tatizo be it mwenza amemsaliti au kukosa kazi nk na watu wa kutoa msaada wa aina hiyo wapo, unasema sex education..ipi hiyo? sidhani tatizo ni kutokuwepo sex education, utatoaje elimu ya mahusiano kwa rika ambalo sheria zinawakataza kujihusisha na mambo ya mahusiano? Kinachotokea kwa wenza kudhuriana ni tabia ya mtu ni sawa tu na kusema huhitaji kufanya mafunzo ili watu waache kuiba..na suala la tabia linashughulikiwa vizuri nyumbani na wazazi au walezi, na sheria zipo kurekebisha mapungufu ya malezi, ndiyo maana nikashauri serikali ijaribu kuweka namna bora zaidi kupitia sheria na miongozo kwa wazazi na walezi kufanya wajibu wao ipasavyo..huwezi kutoa mafunzo kwa kila tatizo linaloiathiri jamii wakati sheria na miongozo sambamba na elimu tunayopata inatosha kabisa kumsaidia kijana au mtoto kufahamu lipi ni baya lipi ni zuri..imekuwa kama wimbo kila jambo linaloihusu jamii kisingizio ni hakuna mafunzo au watu wanaihitaji elimu ya jambo fulani, mbona kwa mfano husikii watu wanasema wanahitaji elimu juu ya kutumia simu, mbona ni rahisi kujifunza mwenyewe kuitumia hata kama hufahamu lugha ya maelekezo..tusiwe watu wa visingizio na kutwist mambo pasi na sababu, madhara ya kusalitiana ni uhalifu sawa na uhalifu mwingine na chanzo ni tabia wala si kukosa elimu ya mahusiano ReTHMI.
 
ReTHMI wazazi na walezi huwa wamesomea mambo ya mahusiano wanapoelekeza watoto au vijana wao mambo ya kuoa au kuolewa? au wanapompa angalizo mtoto asijihusishe na mahusiano katika umri mdogo? Ni kitu gani wanakuwa hawana wanapomweleza mtoto mambo haya, ila mtu mwingine anacho..
 
Kwenye uhalifu kuna vyombo vya ulinzi vinasimamia hilo, na adhabu stahiki zinatolewa. Lakini miongoni mwa kitu kigumu kuingilia ni mfarakano kwenye mahusiano. Mtua anakatwa mapanga au na kisu na mume au mke wake lakini akipona anagoma kutoa ushirikiano kwa polisi ili mwenza aliyefanya hilo achukuliwe hatua, wanayamaliza kifamilia ila mwisho wa siku yanajirudia mwenza anammaliza kabisa. Elimu ya mahusiano ni muhimu.

Yani naona unafananisha vitu visivyo na mantiki kabisa na jambo muhimu kama hili. Kutokujua kutumia simu kunagharimu maisha ya watu? Kuna mambo inabidi ufikirie kwa kina, na nimesharudia mara nyingi kwamba enzi hizo ilikua ni jambo la msingi na ndio maana kulikua na jando na unyago.

Unaposema mtoto asipewe hiyo elimu kwasababu sheria hazimruhusu kuwepo kwenye mahusiano. Hivi umefanya utafiti ni watoto wangapi wananajisiwa na watu wazima (kubakwa na kulawitia) kwa kurubuniwa tu? Hivi umefuatilia watoto wadogo kwenye kizazi hiki michezo wanayocheza?

Ni kutaarifu tu watoto wanaanza haya mambo mapema sana, na nyuma ya hili kuna mambo yanayopelekea hili. Ila wakielekezwa namna ya kujiepusha na hayo mambo nina uhakika mambo haya yatapungua.
 
Na nikujulishe tu ndoa nyingi zinavunjwa na wazazi. Unaongelea mzazi anayemtetea mtoto wake kabla hata ya kujua nani mwenye makosa. Ukitaka kujua hili fuatilia ndoa nyingi zenye mifarakano usipokuta nyingi wazazi pia wanachangia. Mitandaoni tu vipo visa vingi vya kuthibitisha hili.

Kuna njia nyingi za kumaliza matatizo kwenye jamii, Hivi unafikiri kwanini unakuta wazazi wote ni waalimu lakini anampeleka mtoto wake shule, kwanini asimfundishie nyumbani shuleni akafanye mitihani tu?
 
Chapisho lako sijasoma lote ila kura nimekupa. Cha kujazia ingewekwa level flan ya elimu ya kuanzia mafunzo hayo ili kuepuka kufundisha watoto.

Hongera kwa kuona mbali
 
Shukrani sana, Asante pia kwa maoni yako
 
Kwenye uhalifu kuna vyombo vya ulinzi vinasimamia hilo, na adhabu stahiki zinatolewa. Lakini miongoni mwa kitu kigumu kuingilia ni mfarakano kwenye mahusiano. Mtua anakatwa mapanga au na kisu na mume au mke wake lakini akipona anagoma kutoa ushirikiano kwa polisi ili mwenza aliyefanya hilo achukuliwe hatua, wanayamaliza kifamilia ila mwisho wa siku yanajirudia mwenza anammaliza kabisa. Elimu ya mahusiano ni muhimu.

Yani naona unafananisha vitu visivyo na mantiki kabisa na jambo muhimu kama hili. Kutokujua kutumia simu kunagharimu maisha ya watu? Kuna mambo inabidi ufikirie kwa kina, na nimesharudia mara nyingi kwamba enzi hizo ilikua ni jambo la msingi na ndio maana kulikua na jando na unyago.

Unaposema mtoto asipewe hiyo elimu kwasababu sheria hazimruhusu kuwepo kwenye mahusiano. Hivi umefanya utafiti ni watoto wangapi wananajisiwa na watu wazima (kubakwa na kulawitia) kwa kurubuniwa tu? Hivi umefuatilia watoto wadogo kwenye kizazi hiki michezo wanayocheza?

Ni kutaarifu tu watoto wanaanza haya mambo mapema sana, na nyuma ya hili kuna mambo yanayopelekea hili. Ila wakielekezwa namna ya kujiepusha na hayo mambo nina uhakika mambo haya yatapungua.
ReTHMI ni kama huelewi hata content ya ulichokiandika, unarudia rudia mambo yale yale, usidhani mafunzo unayosema kwa watoto na vijana ni kama kuandaa semina au warsha, mafunzo kwa watoto yanafanyika kulingana na mitaala, umri, malengo ya elimu kwa ujumla nk na hivyo kama si somo kamili mfano somo la uraia, basi mafunzo yanaweza kuwekwa kama topic au sub-topic kwenyr somo fulani, ndiyo maana nikakuuliza unadhani kila linalotokea kwenye jamii lazima liwe na mafunzo maalum kwa watoto? nikakuuliza wezi je nao uwe na mafunzo maalum kwa watoto ili wasiibe? huwezi kufanya hivyo, nikaeleza elimu tuliyo nayo inatosha kutoa maarifa kwa watoto na vijana kuwa na tabia njema na kujua namna ya kuishi na watu kwenye jamii including wenzi wao...sijui kama unafahamu kwenye somo la uraia kuanzia darasa la 3 hadi darasa la 7 watoto wanafundishwa maadili ndani yake yamo mambo ya tabia na mwenendo unaofaa kwa jamii, wajibu, nidhamu, upendo, ushirikiano nk wanafundishwa mambo hayo kuwasaidia sasa na badae..haiwezekani kufundisha watoto jambo maalum kama hilo unalopendekeza kama vile unafanya semina au kongamano kwa rika la watoto na vijana na ukadhani utafanikiwa, ni kupoteza muda na resources bure..na utafanya aina hiyo ya mafunzo kwa mambo mangapi? Mahusiano-mafunzo, matumizi ya madawa ya kulevya-mafunzo, ushirikina-mafunzo nk yote hayo yanafanyika na yana madhara kwa jamii..ukienda hivyo wapi utaishia? Kubali tu, si kila tatizo linaloikumba jamii linahitaji mafunzo..
 
Asante kwa mtazamo wako, naheshimu mawazo yako
 
1663502771226.png
 
Naunga mkono mahusiano siku yana dumu mwaka moja na yanakwisha. yapsua vijana wafundishiwe this ya kuwa romantic ata kama ni safari ama holiday ya mahusiana.
 
Back
Top Bottom