ELIMU YA MTAANI: Tusubiri mpaka Polisi wafike eneo la tukio au tumuwaishe hospitalini??

ELIMU YA MTAANI: Tusubiri mpaka Polisi wafike eneo la tukio au tumuwaishe hospitalini??

Retired Analyst

Senior Member
Joined
Apr 7, 2025
Posts
138
Reaction score
244
Eti wakuu, Jenga picha upo kijiweni saa 12 jioni baada ya kutoka kazini, mnapiga story mbili tatu, mara ghafla linatokea tukio la uhalifu, mtu mmoja anapigwa risasi barabarani/mtaani.

Ila baada ya kumtazama vizuri mnagundua kuwa huyo mtu anatiririka damu nyingi sana lakini hajafa. Sasa hapa busara ni nini?? Tumuache mpaka Polisi wafike eneo la tukio kwa maana tunaogopa fingerprints na nyayo zetu kuonekana na watu wa forensic au tumuwaishe hospital ili kuweza kuokoa maisha yake??

LENGO NI KUJIFUNZA MBINU ZA KIMAISHA NA UBINADAMU.
 
Fingerprint bongo?
Au mimi ndio sielewi?
Naomba kueleweshwa.
Anyway dunia ngumu sahivi unaweza kusaidia mtu wewe ukaenda kuozea jela upelelezi haujakamilika.
 
Mkuu, sio kwamba watakuchukua kwenda "kuisaidia Polisi"
ndio lazima ukatoe maelezo kwanini ulikuwepo pale so kama hukuwepo pale kwa nia mbaya na sababu ilikuwepo yakueleweka so what..?
Mkuu kukuta fingerprint za mtu mahali fulani huwa si kosa maana asiposhika binadamu ashike nani..? na ukumbuke fingerprint hazionyeshi muda mtu anaweza kuwa ulikuwepo eneo latukio hata kabla yatukio so wanapochukua hizo alama huwa hawakurupuki tu!.
 
Mkuu kukuta fingerprint za mtu mahali fulani huwa si kosa maana asiposhika binadamu ashike nani..?
Mkuu, if this is the case, mbona Polisi huvaa gloves wanapokuwa wanauonesha umma kupitia vyombo vya habari juu ya Silaha za wahalifu walizozikamata?? Lengo ni nini kama sio kuzuia finger marks zisionekane katika vizibiti husika??
 
ili asiongeze fingerprint nyengine zikazidi kuwa nyingi nakufanya uchunguzi utumie muda zaidi hiyo ndio mantiki
 
Back
Top Bottom