Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,786
- 1,715
'Mwosha huoshwa'.
Nape Nnauye ulianzisha mjadala juu ya elimu ya Mheshimiwa John Mnyika na mwenyewe ameshajitokeza kujibu.
Katika uzi huo wa Mheshimiwa Mnyika wachangiaji wengi wamegusia kuhusu details za elimu yako.
Swali la msingi: Matokeo yako ya Form 6 yana mashaka, wengine wanasema ulipata Division IV wengine Division 0. Uliwezaje kwenda chuo kikuu na Division IV ya Form 6?
Ona duku duku la wengi kujua matokeo yako.
Watu hawa wote, pamoja na mimi mwenyewe tunaomba majibu.
Kama kuna waliosoma na Nape pia, mnaweza kutueleza mnavyomfahamu.
Nape Nnauye ulianzisha mjadala juu ya elimu ya Mheshimiwa John Mnyika na mwenyewe ameshajitokeza kujibu.
Katika uzi huo wa Mheshimiwa Mnyika wachangiaji wengi wamegusia kuhusu details za elimu yako.
Swali la msingi: Matokeo yako ya Form 6 yana mashaka, wengine wanasema ulipata Division IV wengine Division 0. Uliwezaje kwenda chuo kikuu na Division IV ya Form 6?
Ona duku duku la wengi kujua matokeo yako.
Nafikiri atakuwaNape Nnauye ameelewa sasa ingawa alikuwa anajifanya haijui elimu ya John Mnyika. Nape Nnauye Haya tuwekee na wewe elimu yako ya kuungaunga pamoja na mwenzako fisadi mtoto wa the pilot au Vasco da Gama
Haya sasa napie nawe weka tokeo la form 4
Ningependa sana baada ya majibu ya Mnyika (aliyepata A-9 straight), sasa nape atupe grades zake, na Ridhwani (who has always been insignificant person ukiondoa kuwa mtoto wa rais nao wawe grades zao humu)
tuleteeni ya Nape
Habari zilizoenea mitaani ni kuwa Nape alipata Division 0 mtihani wa Kidato cha 6, mwenye uhakika au yeye mwenyewe atuhakikishie. Na aeleze aliwezaje kwenda Chuo Kikuu baada ya kupata Division 0 mithani wa kidato cha 6.
Haya Nape na wewe tuwekee matokeo ya elimu yako ya awali yaani Drs. la 7, Form IV, na Form VI hapa jamvini. Tuanzie hapo kwanza.
Vinginevyo tukisema huko vyuo vikuu uliingia kwa favour fulani tutakuwa hatukosei. Mnyika kwa matokeo yake anaweza kwenda chuo kikuu chochote dunani hata baada ya miaka 20 ijayo. Tunaomba grades zako tujiridhishe jinsi ulivyoingia Chuo. Hilo tu kwa sasa mheshimiwa.
Nape na masters yake ya kuchakachua uwezo wake ni sawa na mwanangu aliye chekechea ni kiwango duni kuliko maelezo kitu kikubwa anachotakiwa kushukuru ni mfumo sultani uliombeba lakini jamaa ni mbulula zero kilaza na ndiyo maana anakubali kutumika bila kufikiria.
Ndugu wanajamvi nasikitika tu kueleza kuwa Nape kaanzisha suala la elimu ilihali yeye akijua kabisa kuwa hana uwezo na hatokuwa na uwezo kielimu kama aliokuwa nao Mnyika.
Nape alihamia Nsumba Sekondari iliyoko Mwanza Mwaka 1995 akitokea Ngudu Sekondari iliyoko wilayani Kwimba na kunikuta mimi nikiwa kidato cha kwanza yeye akiwa kidato cha pili.
Nape alifikia kuishi bweni lijulikanalo kwa jina la Mondlane room 3. Kijana Nape alikuwa mcha Mungu sana maarufu kama mlokole.
Nape baada ya kuhitimu form four alipata division four ya point 29. Sasa mimi sijui alifikaje huko form six. baada ya hapo sikuelewa tena nini kiliendelea kwa Nape kwa elimu ya bachelor lakini kwa masters yake amehangaika sana kukamilisha dessertation yake pale Mzumbe kwa habari niliyoipata kutoka kwa Lecturer mmoja ambaye ni jamaa yangu wa karibu na aliyemfahamu tangia akiwa form two.
Baada na hata kala ya kubuni na kusambaza tuhuma za uongo dhidi ya Ndugu John Mnyika,historia ya elimu ya Ndugu Nape Nnaye imekuwa, mara kwa mara, ikihojiwa na wafuatiliaji wa masuala ya mambo, hasa wanaojali na kuamini katika weledi, umahiri na umakini wa watekelezaji na wasimamizi wa majukumu mbalimbali katika ngazi na maeneo mbalimbali ya kiutawala..
Kwa kadiri ya ufahamu wangu,ningependa kuweka wazi kabisa kuwa Ndugu Nape amepata kusoma katika ngazi ya Kidato cha Sita na hatimaye kupata daraja sifuri. Kwa matokeo hayo, ni dhahiri kuwa Nape hana Elimu ya Kidato cha Sita.Kwa kuwa inafahamika kuwa Nape alipata daraja la Nne (IV) la pointi 29 katika mtihani wa Kidato cha Nne na kwa kuwa mantiki ya kawaida inaweka sharti la mtahiniwa yeyote wa Kidato cha Sita kuwa na angalau credits tatu katika matokeo ya Kidato cha Nne; basi, inafuata kimantiki, kuwa, Ndugu Nape amepata kufanya Mtihani wa marudio kwa minajili ya kupata alama ambazo zingemwezesha kuweza kumpa sifa ya kuweza kufanya mtihani wa Kidato cha Sita.
Katika hali ya isiyojulikana msingi wala nia yake, Ndugu Nape amekuwa si muwazi na mkweli hata kidogo katika historia yake ya kielimu na kitaaluma ingawa yeye mwenyewe amejivika jukumu la kuhoji viwango vya Elimu vya wananchi wengine. Kutokana na hali hiyo, wafuatiliaji wa elimu yake wamekosa majibu sahihi na yenye kujitosheleza.
Aidha mtu huyu amethubutu hata kudanganya umma mara kadhaa kuwa amepata kusoma katika Shule ya Sekondari Mwenge iliyopo iliyopo Singida, na kuhitimu Kidato cha Sita mwaka 2000. Hii si kweli. Baadhi yetu tunajua ,yeye mwenyewe anajua, ndugu zake wanajua na hata Utawala wa Shule kuwa huu ni uongo wa wazi. Nape, ingawa anaijua vema shule hiyo kongwe kabisa iliyopo Mjini hapo, hakupata kuwa mwanafunzi katika shule hiyo. Ukweli ni kuwa alifanya mtihani wa kidato cha Sita,kama mtahiniwa wa kujitegemea katika shule hiyo na kupata daraja sifuri.
Aidha, Nape katika miaka ya mwanzoni mwa 2000 alikuwa na kawaida ya kwenda katika shule hiyo kwa shughuli za Uinjilisti, akiwekeza katika kuwalea wanafunzi kiroho wa kikundi cha CASFETA shuleni hapo. Sasa, kama kufundisha dini tu mara moja kunampatia mhusika hadhi ya uanafunzi katika shule basi tunao wanafunzi na wahitimu wengi katika nchi hii kuliko tunaowajuai!
Mwisho kabisa ningependa kumsihi Nape ajenge utamaduni na tabia ya kusema ukweli maana ukweli, daima, utamuweka huru. Hii ni muhimu kwa kuwa haiwezekani kuwa mtu mwenye hadhi ya mtumwa katika kasri la Mfalme kupanga na kuratibu mkakati na mbinu za kuwatoa watumwa wengine wa kweli na wa uongo kutoka katika vifungo vya utumwa.
MUZEEZAIDI said:Nimeamua kueleza ukweli huu baada ya kuona upotoshaji wa makusudi unaoendelea humu.
Kuna mtu kajitokeza kujibu elimu ya Nape wengi wakahoji kwani Nape yuko wapi asijitokeze mwenyewe kujibu kama alivyofanya Mnyika?
Naomba mfahamu aliyejibu ni Nape mwenyewe kwa kutumia ID ya bandia, lakini amekuwa mno too radical hadi watu wakamshtukia.
Lakini hoja sio kuwa radical, au kutumia ID bandia, hoja ni kuwa amefanya upotoshaji wa makusudi uliotuacha mdomnd wazi wale tunaomfahamu. Sasa ukweli kuhusu elimu ya Nape huu hapa.
Mwaka 1993 alifeli darasa la saba. Wakati ule jina halali la Nape akiitwa Nahum Nnauye. Waliosoma nae wanakumbuka. Bt akafanyiwa mpango na kupewa jina la Nape Mkumbo Nyagicha mtoto masikini wa Kinyiramba, aliyefaulu lakini familia yake haikuwa na uwezo wa kumsomesha.
Mwaka 1994 Nahum Nnauye akajiunga na shule ya sekondari ya kutwa Ndugu wilayani Kwimba akiwa na jina kaiba jina jipya la Nape. Mwaka 1995 akahamishiwa shule ya Sekondari Nsumba kwa kutumia title ya baba yake Mzee Moses Nnauye.
Mwal 1997 akafeli form four kwa kupata division four ya point 29 akiwa na D 4, c 1 na F 5. Akareseat mara 2 bila mafanikio pale Butimc TTC ambacho ni kituo cha watahiniwa binafsi. Mwaka 1999 na mwaka 2000.
Akakata tamaa na hatimaye mwaka 2001 akaamua kwenda kusoma cheti cha Uhazili (cert of secretarial services) katika chuo cha Kivukoni. So kabla sijaendelea naomba ieleweke kuwa Nahum Moses Nnauye (Nape) hajawahi kusoma form 5 shule yoyote duniani. Kama anabisha aje hapa tumuulize maswali ya Geography 1 au Ecomics 2 uone atakavyochanganyikiwa. Kwanza hajui kama kuna paper 1 na 2 A.level, atasemaje amesoma A.level?
So uhazili mwaka akatumia cheti chake cha uhazili kuomba diploma pale chuo cha Diplomasia kurasini. akapata na akaanza kusoma. Mwaka mwaka 2002 akafeli kuendelea na 2nd year baada ya kupata suplimentary 4 ktk masomo 6 aliyokuwa akisoma. So kwa kifupi akadsco. Hivyo naomba ieleweke kuwa huyu jamaa anayejiita Nape hajawahi kutunukiwa diplmoma yoyote kutoka Chuo cha Diplomasia Kurasini. Kwanza asikidhalilishe chuo maana pale hakuna Diploma ya mwaka mmoja. kama anabisha aupoad picha yoyote hapa alipokuwa anatunukiwa hiyo diploma.
Grace Mwasonge unamkumbuka Nape vzr maana alikuwa classmate wako wakati huo. So najua uko humu japo kwa ID tofauti naomba ujitokeze kudhibitisha ili isionekane nafanya defamation.
Mwaka 2004 akatumia cheti chake form four kuomba degree India kwa kusaidiwa na mwandishi mmoja mashuhuri nchini kwa kuwatafutia vyuo vya nje watu waliofeli.
Na akapata kwa masharti ya kusoma miaka minne. Ikumbukwe India ni nchi yenye vyuo vya hovyo sana duniani, na ni miongoni mwa nchi ambazo hata kama una zero unaweza kusoma Bachelor bila matatizo yoyote hadi ukahitimu. Reffer kesi ya Mr.Andekisye, Lecturer aliyefukuzwa kazi Arusha University kwa kusoma elimu feki India. Andekisye aliajiriwa kama mhadhiri wa Marketing na Business Mathematics akidai ana MBA kutoka India. Bt ilipofuatiliwa ikagundulika ni kweli ana Masters bt hajawahi kusoma Bachelor. Alichomoka na Diploma yake ya Ualimu (Mathematics & Physics) kutoka Monduli TTC akaaply Masters India akapata akaenda kujoin. Sasa imagine mtu anatoka Diploma anakwenda Masters sembuse Nape kusoma bachelor?
So akapata degree yake fake ya psychology ambayo ndiyo aliyoitumia kuomba masters mzumbe. Na mzumbe hakukabidhi cheti zaidi ya kile cha degree yake ya India.
Kama anabisha aweke vyeti vyake vya o.lel na a.level hapa.
Huyo ndiye Nahum Moses Nnauye anayejiita Nape. Katibu mwenzezi wa Chama cha Mapinduzi CCM na mgombe ubunge ubungo mwaka 2010, wakati ule akijaribu kushindana na genious aliyepata A 9 O.Level yeye akiwa na D 4 tu.
Watu hawa wote, pamoja na mimi mwenyewe tunaomba majibu.
Kama kuna waliosoma na Nape pia, mnaweza kutueleza mnavyomfahamu.