PreGE2025 Elimu ya Shigongo inatia mashaka. Aliyeelewa kipengele hiki kwenye elimu ya Mbunge Eric Shigongo naomba anieleweshe!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ni kweli. Kuna kipindi mfumo uliruhusu darasa la 7 kusoma degree
Yeye alipata fursa hiyo
Hakubahatika kupita elimu ya sekondari na mara nyingi ata yeye huwa anasema
 
Hujui kuna TCU? Kwanini usiende TCU au Chuo alichosoma ukajibiwa maswali yako? Kama wewe pia umesoma top universities si bora uchome moto hivyo vyeti vyako ili angalau tujue hujasoma?
😂😂😂 omce again haina haja ya maneno mengi, vijana wako chimbo data zitamwaga

And pls msilimbiane humu ndani
 
Huyo kafanya utapeli wa elimu , elimu ya janjajanja kama una hela unapewa vyeti bila hata kusoma
 
Huyo Degree yake halali kabisa.

Wewe una umri Gani?
nilitaka niulize swari kama hilo ana umri gani yeye
Mana jamaa maisha yaje yote alikuwa anayaandika
na siku zote alikuwa anasisitiza aliishia darasa la 7
Aende akamsone kwenye KITABU chaje au STORY ya maisha yaje ipo kwenye PAGE yake kama sikosei ile story
 
Mwaka 2017, nikiwa nafanya kazi Global Publisher, nimekaa nyuma ya kompyuta yangu, alitokea Shigongo akiwa mwenye furaha sana. alisema kwa furaha, nimeruhusiwa kusoma degree Tumaini! Wote tukawaza imewezekanaje? Nakumbuka mbele yangu alikaa Mzee Walusanga Ndaki, tukatazamana kwa mshangao tukihisi labda kuna kitu hakiko sawa!

Aliendelea kusema, "nilijaribu kulist kidato cha pili (QT) nikafaulu baada ya majaribio ya miaka kadhaa, nikaanza kidato cha nne, ambako nilifeli kwa kipindi cha miaka kadhaa, nilikata tamaa na niliahirisha kuendelea na elimu yangu kwa sababu mtihani wa kidato cha nne ulinishinda kufaulu... lakini akatokea mtu mmoja akaniambia upo mpango maalumu, wewe umeandika vitabu, leta vitabu vyako vyote ulivyoandika tutakuruhusu upate degree yako! Na sasa Tumaini wameniruhusu nikasome degree yangu!

Baada ya hapo, alituchukua wafanyakazi wote, akatupeleka katika hotel ambako alitununulia chakula, kisha akatugawia hela, mimi nilipewa Elfu Thelathini!
 
Wewe unaweza kuandika hata stori ya kurasa 2?
Acha ujinga ww alokuambia kuandika vitabu vya stori za mapenzi ndo IQ kubwa wote mtakua mataahira ww ulokubal ujinga huo na aliekuambia.

Mm elimu yake sna shda nayo kaipataje pataje hayo yake bnafs lakn mambo yakusema kuandika stori ni IQ kubwa huo n upumbavu WA kiwango Cha lami
 
Kwahiyo tukubali kuwa elimu yetu haina viwango, inakuwaje standard 7 anasomea degree haya ndio madhara ya rushwa na siasa kwenye elimu
 
Kwa vipimo vya huko kijijini kwenu hiyo sio IQ kubwa kwa sababu ya roho zenu za wivu na kichawi.
 
Tumaini University ilikuwa na program maalum ya kuwaruhusu wahitimu wa darasa la 7 kujiunga na Bachelor. Shigongo ni mnufaika wa huo mpango. Kwa sasa Shigongo ni mwanafunzi wa PhD pale Mlimani UDSM. Kama uliuliza kwa nia ovu shindwa pepo.
Hata raisi SAMIA NAE NI PhD holder? Basi kazi ipo
 
Elim ni biashara ukifika bei unaipata!na kwa bahati mbaya walimu tuliowengi njaa sana kwa level zote!!ukiweka mzigo mezani unateleza TU Hadi PHD!
 
Tarimba Abbas mbunge wa kinondoni, tafuta CV yake,utaishangaa Tanganyika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…