PreGE2025 Elimu ya Shigongo inatia mashaka. Aliyeelewa kipengele hiki kwenye elimu ya Mbunge Eric Shigongo naomba anieleweshe!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Tuelezee kwanza mafanikio yako kabla ya kupekuwa elimu ya Shigongo.

Shigongo ana biashara iliyosajiliwa Brela na TRA.

Maana yake nini, kabla ya kuingia kwenye siasa.

Shigongo, ili kuanzisha biashara yake.
  • Kuna mtaji aliusaka.
  • Kuna vifaa aliagiza
  • Kuna office alilipia pango
  • Kuna watu aliajiri.
  • Baada ya biashara kuwa sawa kuna mishahara ya kulipa, kodi za PAYE, Pango la jengo, VAT na corporate tax.
Hilo lipo wazi kwa naturę ya biashara yake kabla ya kuwa mwanasiasa.

Hili uhalalishe uwezo mdogo wa Shigongo, elezea umefanya nini na shahada yako ya uzamili.

Haya mambo yetu ya kudharau watu wenye mafanikio kwa elimu zetu za kuunga-unga inabidi tuwekane sawe.

Kuwa na shahada hakukupi uhalali wa kujitapa kwenye maisha,

III kunanga watu kwanza uwe umewazidi kwenye maisha na kila kitu (vinginevyo ni wivu tu).

Sasa unamzidi vipi mtu kwenye maisha, wakati kuna watu mnapishana tafsiri yenu ya mafanikio kwenye maisha.

Tuache hizi dharau za watu wengine (kwa kigezo dhaifu kama elimu).

Shigongo ni successful, mengine pambana na hali yako.


​


 
A
Tumaini University ilikuwa na program maalum ya kuwaruhusu wahitimu wa darasa la 7 kujiunga na Bachelor. Shigongo ni mnufaika wa huo mpango. Kwa sasa Shigongo ni mwanafunzi wa PhD pale Mlimani UDSM. Kama uliuliza kwa nia ovu shindwa pepo.
Alidhan mchongo.... Vyuo vikuu vyote vina hio program mleta Mada akafanye research kwanza badala ya kuja kushangaa jf
 
Haya ndo yalee "Do you have any Evil or Talent" Despicable Me
 
Newton ambaye formula yake inatumika mpaka sasa hivi aligundua formula hiyo akiwa na elimu ya kufundishwa na baba yake tu.

Huyo mbunge anauelewa mkubwa sana kuwazidi hata wenye Phd aliweza kuanzisha magazeti ya udaku na akapiga pesa ya kutosha hata wenye Phd waliyasoma. Achana na kuhangaika na mawazo ya ki-academically hutaendelea, kama una elimu ya awali uliofundishwa na wazazi wako tu inatosha sana kujitambua ikichangiwa na exposure ya dunia.
 
Elimu za wabunge (watunga sheria wa tz) ni vichekesho walah
 
Hayo ni mambo ya kawaida Tanzania

Sio tu Tanzania, Kuna vyuo vinaheshimika vipo nje ya nchi wanataratibu zao.

Mfano unaweza kukuta mtu akaruhusiwa kufanya Masters bila kuwa na Bachelor. Japo wanaweka wazi ni case by case na at their own discretion au wanasema exceptional case.

Unaweza kupata admission unconditional au ikawa na condition za kukidhi ili uendelee na Masters.
 
Inawezekana mbona
 
Ila Shigongo ni mpambanaji sana
Hata kama amesoma kwa janjajanja bado uwezo wake ni mkubwa sana.
 
Duh aisee
 
Tumaini University ilikuwa na program maalum ya kuwaruhusu wahitimu wa darasa la 7 kujiunga na Bachelor. Shigongo ni mnufaika wa huo mpango. Kwa sasa Shigongo ni mwanafunzi wa PhD pale Mlimani UDSM. Kama uliuliza kwa nia ovu shindwa pepo.
Wivu tu unamsumbua
 
Miaka ya 70, wakati UDSM ndicho chuo kikuu pekee, kulikuwa na Mature Age Entry Program. Tulisoma na walimu wetu ambao walikuwa wameishia darasa la saba.
 
Ways of acquiring education or knowledge
1.formal
2.informal
3. Non-formal

Ni kweli Eric James Shigongo Bukumbi ana cheti cha darasa la 7.

Na hili hata yeye mwenyewe huwa amekuwa akiliweka wazi....ikiwa ni kama justification ya kuhamisisha vijana waliotoka kwny kaya fukara kama aliyetoka yeye.

Huyu aliwahi kuja Udsm kuzungumza na sisi wanachuo wa wakati huo..

Atakuwa alijiendeleza baadae.
Sio kwa dhumuni la kupata ajira...ila ni kutengeneza status tu..

Na mara nyingi Serikali na jamii yetu kwa ujumla probably na mimi nikiwemo, huwa hatuwapi heshima sana watu walio- aquire elimu zao nje ya mifumo rasmi;

Nii kasumba ya kipuuzi kuamini kwamba kupata Elimu mpaka upitie msoto kama uliokutana nao wewe... eti vinginevyo ni ujanja ujanja.
 
This is neither here nor there...; Sheria ya kuwa Mbunge ni Ipi ? Kwani wananchi wakiamua mtu ambaye hana Cheki kuwawakilisha kuna shida ?!!! Shigongo anaweza akawawakilisha watu kwa moyo na kufikisha mawazo yao na matakwa yao kuliko nafasi hio angepewa hata Bwana Einstein sababu ningesema Faraday lakini hata Faraday nae ni self taught (no formal education)

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…