Elimu ya Tanzania na elimu ya Marekani,mbona sisi tunatumia nguvu nyingi?

Sir Khan

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
5,730
Reaction score
11,576
"Elimu ni kile kinachobaki kichwani baada ya kusahau yale uliyofundishwa darasani" by Albert Einsten.
Wakuu wasalaam,bila kupoteza muda twende na mada.Nianze kwa kuelezea mambo ya tofauti kati ya elimu ya Marekani na Tanzania:-
1.wanafunzi wa marekani hawachapwi viboko,lakini wanafunzi wa Tz wanachapwa hasa wakifeli,kwa wastani kuanzia darasa la kwanza hadi form six mwanafunzi wa Tz anakuwa amechapwa fimbo 1200 jumlisha dazeni za makofi na adhabu ngumu.
2.Marekani wanasoma siku 200 kwa mwaka,lakini Tz wanasoma siku 280 hadi 300 kwa mwaka.
3.Marekani wanafunzi wanatumia simu na hakuna upuuzi wa kuvaa sare(uniform),sisi huku simu ni haramu kwa mwanafunzi zaidi ya viroba,halafu kuvaa sare ni lazima eti wote tuonekane tuko sawa kiuchumi upuuzi mtupu.
Inaendelea......
 
Inaendelea.......
4.Marekani wanafunzi wanakula chakula kizuri,lakini TZ wanafunzi wanalishwa maharage mabovu yaliyooza na wadudu wakutosha, ugali mbaya wenye harufu mbaya halafu walimu na wazazi wanakuambia eti chakula hicho kibaya kinamfanya mwanafunzi awe na akili na kupata afya bora huu ni ubutu wa fikra.
Mambo hayo manne yanaonesha sisi tunatumia nguvu nyingi ila tunaishia kuzalisha ziro nyingi na elimu yetu inazidi kuwa mbovu, wakati hawa wamarekani wasiotumia nguvu sana elimu yao ipo juu sana.
Unaweza kusingizia uhaba wa walimu na vitabu sawa,ila hii sio sababu ya kusingizia,kwa mfano mimi nimesoma o-level shule ilikuwa na walimu wa kutosha,vitabu vya kutosha na fimbo za kutosha lakini 2014 shule ilipata ziro 42 kwenye mtihani wa kidato cha nne.
Je sisi tunakosea wapi? ,je kuvaa sare,chakula kibaya kuzuia simu na kuchapa wanafunzi fimbo ma adhabu kali inasaidia chochote kwenye elimu yetu? kipi kifanyike kukuza elimu yetu?Karibu wakuu
%by Sir Khan.Born 2 win%
 
hasheem thabeet amesoma university of connecticut... chuo kipo 100 bora duniani... sitaki kuamini kama angekuwa bongo hata udsm angepewa nafasi
unamaanisha kichwani hana kitu au sijakuelewa mkuu
 
"Elimu ni kile kinachobaki kichwani baada ya kusahau yale uliyofundishwa darasani" by Albert Einsten.
Wakuu wasalaam,bila kupoteza muda twende na mada.Nianze kwa kuelezea mambo ya tofauti kati ya elimu ya Marekani na Tanzania:-
1.wanafunzi wa marekani hawachapwi viboko,lakini wanafunzi wa Tz wanachapwa hasa wakifeli,kwa wastani kuanzia darasa la kwanza hadi form six mwanafunzi wa Tz anakuwa amechapwa fimbo 1200 jumlisha dazeni za makofi na adhabu ngumu.
2.Marekani wanasoma siku 200 kwa mwaka,lakini Tz wanasoma siku 280 hadi 300 kwa mwaka.
3.Marekani wanafunzi wanatumia simu na hakuna upuuzi wa kuvaa sare(uniform),sisi huku simu ni haramu kwa mwanafunzi zaidi ya viroba,halafu kuvaa sare ni lazima eti wote tuonekane tuko sawa kiuchumi upuuzi mtupu.
Inaendelea......
Hatuna akili
 
Mkuu acha kufananisha marekani na vitu vya ajabu sisi wenzetu wakutufananisha labda Rwanda au kenya mkuu marekani mbali utakuwa unabaka mfananisho
 
Hivi kwa hali ilivyo saizi wanafunzi wanatumia simu nyumbani zero zinakuwa nyingi je wakiruhusiwa kutumia na huko shule itakuaje?
 
Ni Tanzania pekee duniani ambayo mtoto anapewa elimu ya msingi kwa kiswahili kwa miaka saba hadi nane (ukijumlishia na chekechea) kisha anabadilishiwa gear angani anaanza kupewa elimu ya sekondari kwa lugha ya kiingereza kwa miaka minne na anategemewa afaulu.

Tutasubiri sana.
 
swali la kujiuliza kwanini wa ughaibuni wanatumia na elimu yao ipo juu,au wanafunzi wa bongo hawana akili ya kujitawala hasa katika kutumia simu?
 
Mkuu acha kufananisha marekani na vitu vya ajabu sisi wenzetu wakutufananisha labda Rwanda au kenya mkuu marekani mbali utakuwa unabaka mfananisho
Mkuu najua kweli wametuacha mbali,lengo langu ni kutaka kujua wamefikaje uko?
 
fanya kautafiti kidogo mambo yanayofanyika kwenye shule za kitanzania wao waliyaacha lini?
kitambo sana,tatizo umaskini unatufanya tunakuwa na mawazo mgando eti maharage yenye wadudu yanakufanya uwe na akili na afya njema,hivi kweli hii inaingia akilini?
 
Ni Tanzania pekee duniani ambayo mtoto anapewa elimu ya msingi kwa kiswahili kwa miaka saba hadi nane (ukijumlishia na chekechea) kisha anabadilishiwa gear angani anaanza kupewa elimu ya sekondari kwa lugha ya kiingereza kwa miaka minne na anategemewa afaulu.

Tutasubiri sana.
yaaani hapo ndio huwaga nacheka sana
 
Back
Top Bottom