Inaendelea.......
4.Marekani wanafunzi wanakula chakula kizuri,lakini TZ wanafunzi wanalishwa maharage mabovu yaliyooza na wadudu wakutosha, ugali mbaya wenye harufu mbaya halafu walimu na wazazi wanakuambia eti chakula hicho kibaya kinamfanya mwanafunzi awe na akili na kupata afya bora huu ni ubutu wa fikra.
Mambo hayo manne yanaonesha sisi tunatumia nguvu nyingi ila tunaishia kuzalisha ziro nyingi na elimu yetu inazidi kuwa mbovu, wakati hawa wamarekani wasiotumia nguvu sana elimu yao ipo juu sana.
Unaweza kusingizia uhaba wa walimu na vitabu sawa,ila hii sio sababu ya kusingizia,kwa mfano mimi nimesoma o-level shule ilikuwa na walimu wa kutosha,vitabu vya kutosha na fimbo za kutosha lakini 2014 shule ilipata ziro 42 kwenye mtihani wa kidato cha nne.
Je sisi tunakosea wapi? ,je kuvaa sare,chakula kibaya kuzuia simu na kuchapa wanafunzi fimbo ma adhabu kali inasaidia chochote kwenye elimu yetu? kipi kifanyike kukuza elimu yetu?Karibu wakuu
%by Sir Khan.Born 2 win%