Elimu ya Tanzania na elimu ya Marekani,mbona sisi tunatumia nguvu nyingi?

Angalau umejitahidi kujibu kisomi. Hizi ndiyo sababu haswaaa (70%).
 

ni kukremu kwa kwenda mbele lol
 
I think tujenge syllabus tailored to our environment.

pili,tuangalie structures za nje elimu yao ikoje,how can it be improved to suit our needs.

walimu wachaguliwe waliofaulu vizuri,sio waliofeli

mshahara wa walimu upandishwe uwe the same level as majaji etc
 
5. Wamarekani Wanatumia nguvu nyingi kuwekeza kwenye elimu, wakati CCM wanatumia nguvu nyingi kuwadanganya watanzania eti Elimu yetu nzuri.
 
Ukitaka kumtawala masikini mnyime elimu,ukitaka kumsaidia masikini mpe mwanae elimu!!ukitazama vizuri hiyo elimu ni ya wananchi wahali ya chini na wahali yakati kwa uchache je niviongozi wangapi na matajiri wangapi watoto wao wanasoma hizi shule,hata raisi wawa nyonge wanae wanasoma hapo??
 
Siyo jibu. Tusaidiane kutafuta hili tatizo kwa mawazo

Tatizo litatatuka endapo mfumo wa elimu utarekebishwa kuendana na hitajio letu na dunia kwa ujumla...

Wenzetu mambo mengi wamepunguza au kuachana nayo kabisa... mifumo yao ya elimu wanairekebisha siyo kwa ajili ya kupata ufaulu mkubwa ili kuonesha shule fulani inafaulisha zaidi...hapana na kuendana na matakwa na mabadiliko ya dunia...

Cc: mahondaw
 
Bado tunatumia elimu ya mkoloni na mwalimu ya kuwafunza majority kujua kusoma,kuhesabu nakuandika!!lakini si yakufuta ujinga nadhani njia sahihi ya kubadili mfumo wa elimu ni kubadii utawala na watawala waliopo nakuleta viongozi sahihi!!kuanzia kwa mzee Mkapa kilio likuwa hiki walipofanya marekebisho ndo elimu ikazikuwa worse,Kikwete nae akajaribu kurudisha alicho ondoa mwenzie na kuongezea maboresho yake ndio tukaibuka na darasa la saba wasiojua kusoma nakuandika na wamefaulu kwenda sekondari,kinachoendelea awamu hii nadhani kila mmoja anakiona kutoka kwa watoto wasiojua kusoma na kuandika kwa ufasaha mpaka kwa waandaji wavitabu vya kufundushia vye makosa katika upande wa lugha nakadhalika
 
Kwa nchi kama Tanzania elimu inayotufaa kwasasa ni elimu vocational kwanza yaani tuachane kwanza na phd,masters hizi elimu za wakina mafundi mchundo ndio zinachochea ukuaji wa uchumi tujifunze kwa Bangladesh,Korea kusini n.k
 
mie still naona inawezekana kwa serikali hii kuimprove sekta ya elimu kwa kuangalia AWAMU ZOTE ZILIZOPITA walipatia wapi na walikosea wapi,kisha waje na PLAN yao wenyewe…..
 
mie still naona inawezekana kwa serikali hii kuimprove sekta ya elimu kwa kuangalia AWAMU ZOTE ZILIZOPITA walipatia wapi na walikosea wapi,kisha waje na PLAN yao wenyewe…..
Tulitegemea kuyaona mapema pale ndalichoko alipoteuliwa lakini nini kipya mpaka sasa maana yeye nimiongoni waliopinga mwenwndo wa awamu iliopita mpaka sasa kuna innovation ipi katika sekta ya elimu mwaka watatu huu
 
Tulitegemea kuyaona mapema pale ndalichoko alipoteuliwa lakini nini kipya mpaka sasa maana yeye nimiongoni waliopinga mwenwndo wa awamu iliopita mpaka sasa kuna innovation ipi katika sekta ya elimu mwaka watatu huu

naona tuna culture ya kuleana,nchi nyingine ni performance ndiyo inakuweka ofisini,sasa damage inaonekana mapema ila mtu anaachwa ofisini kwa miaka mitano,by then damage imekua inakua kubwa sana….this is sad mkuu
 
Elimu irekebishwe kuanzia msingi lugha ya kufundishia iwe ni kiingereza hii itasaidia kuondoa wale wanaoshindwa kwenda na mabadiliko ya kutoka kiswahili (msingi) kwenda kingereza (sekondari). Nadhani hiyo pia ingesaidia kupunguza miaka ya kukaa shule kwa sababu kuna baadhi ya vitu vinavyofundishwa ktk shule za msingi ndio vinakuja kurudiwa sekondari kwa lugha ya kiingereza. Kuna nchi za wenzetu utashangaa kijana mdogo kiumri tayari amemaliza elimu yake hivyo anakua na muda mrefu wa kuitumia taaluma yake.
 
swali la kujiuliza kwanini wa ughaibuni wanatumia na elimu yao ipo juu,au wanafunzi wa bongo hawana akili ya kujitawala hasa katika kutumia simu?
Kuna utafiti wa UNESCO ulisema kuna udumavu wa akili miingoni mwa watoto Sababu zilikuwa nyingi.
 
Je ni Kwa kiasi gani na Kwa dhamira/nia dhabiti kabisa Kwa miaka hii ya karibuni tumewekeza katika kujenga mfumo bora wa elimu?

Tukianza kujitathmini hapo tunaweza sasa fikiria kuanza kujilinganisha na wengine ambao tayari wameendelea.

Hatuwezi kuanza kulinganisha elimu yetu kwa hatua hii na nchi zilizoendelea wakati ambapo vifaa vya kufundishia bado no mtihani kupatikana mashuleni , maslahi ya walimu na wengine walio Kwenye sekta ya elimu ipo Chini, ualimu kuonekana ni fani duni na mengine mengi ya kufanyiwa maboresho.
 
Moja ya point muhimu sana hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…