Elimu ya Ufundi Katika Utumishi wa Umma

Elimu ya Ufundi Katika Utumishi wa Umma

Mlenge

R I P
Joined
Oct 31, 2006
Posts
2,125
Reaction score
2,306
Elimu ya Ufundi Katika Utumishi wa Umma

Serikali imeamua kutekeleza kwa vitendo uamuzi wake wa kutokuwa na watu wasio na elimu ya kutosha katika utumishi wa umma. Katika kutekeleza hilo, Serikali imeamua kuwa wale wote wasio na vyeti vya kidato cha nne waondolewe kutoka kutumikia umma kwa vile hawakidhi vigezo, mradi tu wawe ni wale walioajiriwa baada ya Mei 20 2004. Naunga mkono uamuzi wa kuimarisha utumishi wa umma kwa kuzingatia viwango vya elimu. Kwa nyongeza, uamuzi wa Serikali unaweza kuboreshwa zaidi kwa kuzingatia pia elimu ya ufundi katika utumishi wa umma.

Zamani, kusoma elimu ya ufundi kulionekana ni kama njia ya kambo kupatia elimu. Elimu ya ufundi ilionekana kuwa ni kwa wale ambao "hawakupasi" vya kutosha kwenda elimu ya sekondari. Watu hao njia yao ya kujiendeleza kielimu ilikuwa na vipingamizi vingi, njia isiyoeleweka inakoanzia wala inakoishia.

Mtu aliyeingia kwenye mkondo wa elimu ya ufundi, kwa mfano, ilimuwia vigumu kusoma masomo ya shahada ('digirii') kwa vile hakukuwa na masomo ya namna hiyo, walau ya kutosha. Watu hao walipokuwa wakijaribu kutoka kwenye mkondo wa elimu ya ufundi kurudi kwenye mikondo mingine, walijikuta wakikabili vikwazo vingi vilivyofanya ionekane 'haiwezekani' wao kusoma masomo ya shahada.

Kwenye baadhi ya vyuo vya elimu ya juu, palitengwa nafasi chache, za ngama, kwa wale waliopitia elimu ya ufundi ("FTC" au vyeti vinginevyo). Hawa waliingia kama 'Watu Wazima waliochelewa kusoma" (Mature Age Entry) hata kama umri wao ulikuwa sawa tu na wa wenzao waliokuwa wanajiunga. Kisha, kulikuwa na kozi chache tu ambazo waliruhusiwa kuzisoma.

Matokeo ya vikwazo vingi kwenye elimu ya ufundi kulifanya jamii idharau elimu ya ufundi na wengi kuikwepa walipoweza kwani haikuwa na njia zilizoeleweka za kujiendeleza kielimu mpaka elimu ya juu. Elimu ya ufundi ikanyanyapaliwa na kuonekana kana kwamba ni kwa wale "waliofeli" kuingia katika mkondo wa elimu "rasmi" ya masomo ya sekondari na vyuo vinavyotoa "elimu", ikiwa na maana ya vyuo vyote visivyotoa "mafunzo" ya ufundi. Matokeo yake vijana wengi walikwepa kuingia mkondo wa elimu ya ufundi.

Kwa kutambua mapungufu haya, serikali iliamua kubadilisha sera na sheria ili kuwezesha ufundi kuonekana nao pia ni "elimu", na ambao "ni sawa tu" na "elimu ya sekondari" iliyoonekana kana kwamba ndio "elimu ya kweli". Mtu aliyemaliza elimu ya msingi akienda sekondari aweze kujiendeleza mpaka kufika elimu ya juu. Mtu huyohuyo aliyemaliza elimu ya msingi akienda elimu ya ufundi aweze kuwa na njia hukohuko elimu ya ufundi ya kujiendeleza mpaka afike elimu ya juu. Ndipo Bunge letu tukufu lilipotunga sheria za elimu ya ufundi, na kuanzisha baraza la kusimamia elimu ya ufundi (NACTE). Baraza hilo, hata hivyo bado halijazoeleka. Wengi hulichanganya na baraza la mitihani (NECTA). Na hata viwango vya elimu vinavyotambuliwa na NACTE havijakubalika kwenye mfumo wa utumishi wa umma namna vile ya NECTA vilivyokubaliwa.

Mfano halisi na rahisi ni huu wa ulazima wa vyeti vya kidato cha nne kwenye utumishi wa umma. Ni wazo zuri, lakini linalotekelezwa kwa mapungufu. Vyeti vinavyotambuliwa na baadhi ya waajiri wa umma ni vile vya NECTA tu katu si vya NACTE. Huu ni upungufu mkubwa sana. Unarudisha nyuma kwa miongo kadhaa mafanikio ya serikali katika kuboresha elimu ya ufundi. Elimu ya ufundi ni muhimu mno katika kujenga uchumi wa viwanda, sawa tu, na pengine kuzidi elimu isiyo ya ufundi. Kumlazimisha mtu aliyepitia mkondo wa elimu ya ufundi inayotolewa na baraza la NACTE alete cheti cha kidato cha nne kinachotolewa na baraza la NECTA ni sawa na kupima weledi wa samaki kuogelea kwa vigezo vya uwezo wa samaki huyo kukwea minazi.

Watumishi wa umma wenye elimu ya ufundi sawa na kidato cha nne (wengi wao kuzidi) wamesimamishiwa mishahara na wako kwenye taharuki kubwa kutegemea waliajiriwa lini. Wale ambao waliajiriwa zamani wanaonekana wamebakizwa kwenye ajira "kwa hisani tu", kwa vile tu, "bahati yao", waliajiriwa kabla ya Mei 20 ya mwaka 2004. Wale wanafunzi waliojitosa kwenye mafunzo ya ufundi (Vocational Training) mara baada ya kuhitimu elimu ya msingi, kwa malengo wakajiendeleze kwenye utaalamu wao mpaka ngazi za juu za utaalamu, bila shaka sasa wengine wao watakuwa wanajutia uamuzi huo. Wanaona Serikali iliyoahidi kutambua elimu yao hiyo, imewageuka.

Tumerudi zamani, kule ambapo ufundi siyo elimu, walau kwa muonekano, siyo elimu kama vile ile "elimu kweli" ya sekondari. Jionee tofauti. Ukisoma sekondari unapata "elimu ya sekondari". Ukisoma ufundi unapata "mafunzo ya ufundi". Hapa ndipo tatizo linapoanzia.

Mapendekezo
Serikali isitishe utekelezaji wa kuwaondoa wasio na mafunzo ya kidato cha nne kutoka kwenye utumishi wa umma, mpaka pale itakapowianisha vizuri mafunzo ya sekondari na elimu ya ufundi. Kwa mfano, kumfukuza mtumishi mwenye mafunzo ya ufundi (National Technical Awards) kutoka Chuo kinachotambuliwa na NACTE au mamlaka ya elimu ya ufundi (VETA), kwa vile tu hana "D" mbili za kumpatia "divisheni 4" ya mafunzo sekondari ya NECTA ni kupoteza nguvukazi ya taifa bila ulazima.

Serikali itambue na kutamka bayana elimu za ufundi katika miundo ya utumishi wa umma sawa na vile inavyotambua mafunzo ya sekondari katika utumishi wa umma.

Serikali iangalie namna ya kukabiliana na sintofahamu iliyoko kwenye kada za ufundi kutokana na miundo mbalimbali ya utumishi wa umma na ya udahili elimu ya juu kutotambua ipasavyo elimu ya ufundi.

HITIMISHO
Mwelekeo wa siku hizi duniani ni kuimarisha elimu ya ufundi, na kuimarisha mafunzo yanayoegemea weledi (Competence-based) zaidi kuliko nadharia.
Manufacturing boom: Trade school enrollment soars
Now is the time to forsake that liberal arts degree for skilled labor
Vocational Education Is Out; Career and Technical Education Is In | EdSurge News

Waajiri wakubwa kwa wadogo, siku hizi wameacha kuangalia vyeti, na badala yake waangalia ujuzi wa mtu, kwani vipo vyeti ambavyo huonekana si lolote si chochote.
Bill Gates And His Foundation: Employers Should Focus On Skills, NOT College Degrees
Uni degree? You don’t need one
Employers value skills over college degrees, workers say

Waajiri sasa hutafuta vipaji (aptitude) na weledi kwa watumishi; makaratasi ya vyeti yakiwa ni kutimiza mradi tu.
A Funny Book about Worthless Degrees | Minding The Campus
The 10 Skills Employers Most Want In 20-Something Employees
Google & 14 More Companies That No Longer Require a Degree

--------------
Mlenge
 
Dr Mgendi unachokieleza kina mantiki nichangie hoja kidogo
Uzoefu katika nchi zilizoendelea unaweza kutusaidia kidogo

Kuna vyuo vya chini, mwanafunzi anaweza kufanya 'bridging' kuendelea na elimu ya juu
Kuna vyuo vya chini mwanafunzi hawezi kufanya 'bridging' kuelekea juu

Hii maana yake ni kuwa kuna basic knowledge inayotakiwa ili kumwezesha mwanafunzi
Hiyo ndiyo inatoa tofauti ya 'bridging' kati ya chuo kimoja na kingine

Kigezo kinachotumiwa katika 'bridging' ni basic education inayopimwa kwa mitaala ya elimu
Kwetu tuna NECTA kama ulivyoeleza inayotoa 'cut off points' za wanafunzi kuendelea

NACTE ilianzishwa kwa ajili ya kutoa elimu ya ufundi ambayo kwasasa ina pengo.

Ni ngumu sana kumpata fundi mwenye ujuzi katika ngazi za chini kama 'brick layers' n.k.
Tuna wanaojiita mafundi waliopata uzoefu kutoka kwa mzee so and so bila formal education

Nadhani kuna nafasi ya wanafunzi wa NACTE kufanya vizuri kwa skills zao kama NACTE itasimamia utoaji wa elimu bora. Hao watafanikiwa huko waliko kwa kutumia skills zao

Endapo wanataka kuendelea, watumie foundation ya skills zao kupata 'D' mbili au tatu kutoka NECTA kama platform. Hii itawasaidia kupata basic education wakiwa na skills zao na mbele ya safari watakuwa wazuri sana.

Idea ya kuwaingiza katika utumishi wa umma si nzuri. Kwa mfano mtu amesoma VETA na ni fundi welder mzuri sana, unamwangiza katika utumishi wa umma akafanye nini?

Mtu huyo ukimwacha katika private sector, akajiajiri au kujiariwa huko, ana nafasi nzuri sana kuliko kumwingiza katika utumishi wa umma

Muhimu si NACTE kukubalika bali kufanya kazi ikubalike kwa kutoa wahitimu wazuri
NECTA ibaki kama 'filter' ili kuhakikisha hakuna 'dilution' ya elimu zaidi ya tuliyo nayo
 
Pamoja Nguruvi3.

Kwenye baadhi ya ofisi za umma, wanahitajika watu wenye ujuzi unaopatikana kozi aina ya zile za NACTE. Tuchukulie ofisi hiyo inamhitaji fundi mchomeleaji. Ipo sababu gani kulazimisha fundi huyo kuwa na elimu ya kidato cha nne?

Tumchukulie kijana Baraka [Jina la kufikirika]. Kasoma elimu ya msingi. Kisha akajiunga na chuo cha VETA kusoma kozi ya kuchomelea vyuma.
Welding and Metal Fabrication
Hapo akasoma na kuhitimu. Baadhi ya masomo aliyosoma ni:
Level I

MODULES CODES MODULE TITLES
WF 101 Maintaining safety of workshop and surroundings.
WF 102 Perform preventive maintenance of tools and equipment, machines
WF 103 Performing bench work.
WF 104 Performing sheet metal work.
WF 105 Performing all positions arc welding and ARC cutting.
WF 106 Performing gas welding, brazing on ferrous and nonferrous metals.
Level II

MODULES CODES MODULE TITLES
WF 201 Performing arc welding on alloy steels and ferrous metal.
WF 201 Performing gas welding on ferrous and non-ferrous metals.
WF 203 Performing fabrication works according to the drawing.
WF 204 Performing site installation involving welding.
WF 205 Performing resistance welding.
FA 201 Field Attachment
PW 201 Project Work

Related Subjects
Supporting Subject:

English and Communication skills
Mathematics.
Engineering Science.
Technical drawing.
Computer Application.

3.4.2. CROSS-CUTTING SKILLS
Entrepreneurship Education and Training
Life Skills

Baada ya kuhitimu akaomba ajira kwenye taasisi ya umma, na kubahatika kuajiriwa kama Fundi Mchomeleaji II, mnamo baada ya 20 Mei 2004.

Je, kijana Baraka afukuzwe kazi kwa vile tu hana cheti cha kidato cha nne?
 
Mlenge
Nakubaliana nawe ikiwa tu mtu huyo yupo katika ajira kwa sasa.
Hata hivyo lazima kuwe na kipindi kitakachowaondoa katika utumishi wa umma.

Kama unafuatilia shughuli nyingi za umma ni za administration tofauti na zamani ambapo wizara ilihitaji fundi wake. Kazi zinafanywa na contractors ambao ni nafuu kwa gharama

Baraka anatakiwa afanye kazi kwa contractor kama ''indirect employment'' itakayompa fursa zaidi za kujiendeleza mwenyewe kwa kujiajiri 'sub contractor' au kuajiriwa

Nikirudi kwa wale walioajiri, utaratibu ungetumika wa ku phase out kwa kutoajiri bila kuwaathiri walioajariwa.

Wizara ya afya ilikuwa na RMA(Rural medical aids) ambao walianza na Darsa la 7 na kadri ilivyoendelea wakachukua Form Four

Huduma za afya zimepanuka na wataalam kuongezeka, hatua ya kwanza ilikuwa kusitisha kozi za RMA. Waliokuwa kazini waliendelea hadi walipostaafu.

Hata hivyo RMA bado wana uwezo wa kufanya kazi katika private organization. Kinachowalazimu kufanya upgrading ni competition kutoka kwa Clinical officers

Utaratibu mzuri wa wizara ya afya ni kutoweka kipingamizi kwa anayetaka kuendelea
Wapo walioanzia RMA, wakawa clinical officers kisha AMO (Assistant medical officer)

Kwa mtazamo huo nakubaliana nawe milango isifungwe kwa candidate wa NACTE. NECTA iangalie utaratibu wa kuwapa second chance wakiwa na skills

Inawezakana kukiwa na utaratibu kama wa wizara ya elimu.

Kulikuwa na Walimu grade B ambao basically walikuwa kama ''VETA''.

Grade B walipewa nafasi ya kwenda grade A na katika kozi walifundishwa masomo ya secondary waliyokosa ili kuwapa basic knowledge na kufikia std kama ya Form IV

Likewaise walimu wa F IV walipewa fursa ya kufanya masomo ya A level ili mbele ya safari waweze wafikie std ya kujiunga na chuo kikuu kama graduate wa A Level.

Tunajua maprofesa katika utaratibu huu. Bottom linemhusika afikie std

Nisichokubaliana nacho ni kutafuta utaratibu wa kupinda std ili ku accomodate kundi

NECTA ndiyo std katika utahini, anayetaka afanye mitihani yake, tusijaribu kupinda utaratibu ili ku accomodate NACTE candidate.

Wakiwa na skills zao wapewe fursa ya kujiendeleza wakifikia std ile ile.
Kama cut off point ni F IV lazima wafikie std wakiwa na skills zao
 
Nguruvi3, hoja zako kutopindisha viwango ni za msingi kabisa. Viwango lazima viheshimiwe.

Viwango.

Siyo majina ya viwango.

Kwa sasa, serikali inataka kutambua jina moja tu la viwango vilevile, wakati yapo majina mbalimbali ya kiwango hichohicho ambacho serikali inakitambua. Ili kuepusha mgongano wa tafsiri, serikali iliandaa mfumo wa ulinganisho elimu Tanzania (Tanzania National Qualification Framework), kwa kifupi TzQF. Kwa mujibu wa TzQF, elimu ya Tanzania imegawanywa katika ngazi kumi zinazotolewa katika sekta mbalimbali. Angalia kiambatanisho.

Ngazi ya nne katika elimu Tanzania ndiyo ya chini kabisa ambayo serikali inataka mtumishi awe nayo. Kwa hiyo basi maelekezo ya serikali yangekuwa kwamba:
Kila mtumishi wa umma awe na kiwango cha angalau ngazi ya nne kama ilivyoainishwa na TzQF.
Na hiyo ingekuwa inatoa fursa ya ajira kwa wananchi wenye cheti cha ufaulu elimu ya kidato cha nne na wale pia wenye vyeti vingine vya ufaulu kwa ngazi hiyohiyo ya nne. Kwa nini? Tuangalie vizuri hiyo ngazi ya nne ya elimu.

Ngazi ya nne ya elimu hupatikana katika sekta nne kuu:

1. Sekta ya Mafunzo ya Ufundi (Vocational Certificate)
2. Sekta ya Mafunzo ya Ufundi Mchundo (Basic Technician Certificate
3. Sekta ya utaalamu (Technician Level I)
4. Sekta ya shule za sekondari: Hawa hupata cheti cha ufaulu kidato cha nne (Certificate of Secondary Education).

Zote hizo nne ni kiwango sawa cha elimu. Kukubali kiwango cha sekta moja tu kati ya sekta nne bila shaka ni mapungufu makubwa. Hii inatokana na sababu za muda tu.

Wakati serikali ikiamua nani aajiriwe utumishi wa umma, TzQF haikuwa hewani. Baadaye serikali iliona mapungufu ya kutilia mkazo sekta moja tu ya ngazi za elimu. Ndipo ikaleta TzQF.

Yaani, ni kupitiwa tu na kusahau kuhuisha maagizo kuhusu elimu ya kidato cha nne kwa kuzingatia TzQF. Hilo ni jambo linalowezekana kufanyika sasa na kuweka sawa mambo. Hiyo itawezesha kuongeza ari ya kujiendeleza kielimu daima dumu (lifelong learning) na itafanya maamuzi ya serikali yawe endelevu (internally consistent).
 

Attachments

Mlenge
Ahsante sana kwa michango yako. Nitarejea baada ya kupitia majedwali
Unatusaidia sana katika haya ambayo yapo lakini ni kama hayapo
 
Pamoja mkuu Nguruvi3.

Angalia vizuri hayo majedwali. Utaona kwamba cheti cha uhitimu wa elimu ya kidato cha nne ni moja ya sifa zinazomwezesha kijana kujiunga na elimu ya ufundi ngazi ya nne ya TzQF, sawa tu na mafunzo ya shule ya msingi.

Tafadhali pitia utupatie maoni yako.

--
Mlenge
 
Pamoja mkuu Nguruvi3.

Angalia vizuri hayo majedwali. Utaona kwamba cheti cha uhitimu wa elimu ya kidato cha nne ni moja ya sifa zinazomwezesha kijana kujiunga na elimu ya ufundi ngazi ya nne ya TzQF, sawa tu na mafunzo ya shule ya msingi. Tafadhali pitia utupatie maoni yako. Mlenge
Mlenge kuna mambo napenda nichangie hapa baada ya kupitia majedwali kwa utulivu

1. Ahsante kwa majedwali, nakiri kabisa sijui ni wangapi wamewahi kuyaona na sijui hata watunga sheria wetu au watendaji wanajua yapo, highly doubt

Umesaidia sana umma kwa tafsiri ya mambo mengi, TzQF, NECTA na NACTE

2. Kuto majedwali ulichosema bandiko #5 na 7 nimeelewa mantiki kwa dhati

Kwamba, Form IV-VETA na Std-VII wa VETA ni kundi moja kwa certification, katika ajira kinachotumika ni cheti cha IV kama kigezo. Ni kweli na ni wrong concept, nakuliana nawe

Wote wawili wanapata cheti cha VETA wanakuwa na qualification ile ile.

Kuwahukumu kwa kilichotokea siku za nyuma si haki. Kama ni hivyo qualification hiyo ingekuwa na madaraja kwa mfano VETA grade A au B. Kwa mujibu wa majedwali sikuona hilo

Mfano mzuri ni utaratibu wa NBAA, unatambua mtu kwa sifa aliyofikia si wapi alikotokea.

Hata wizara ya afya, kama uulikuwa RMA uka upgrade na kuwa AMO, kwavile RMA imekuwa phased out, hukumu hiyo haikuhusu, unabaki na qualification uliyo nayo

3. Baada ya kuangalia hayo, upande wa utumishi nao una hoja.Kumbuka tulichojadili ni TzQF

Utumishi wana sifa zao za utumishi. 'pengine' wanaamini fundi welder IV ataweza kuchagamana na changamoto kuliko std-VII hata kama wapo daraja moja

Ni kama Employer yoyote anayetangaza nafasi za kazi, kwa mfano Daktari.

Katika sifa anataka aweze kutumia software abcd na awe na Leseni ya udereva
Hata kama waombaji wametoka chuo na darasa moja, kwanini tumlaumu mwajiri!

Nimalizie kwa kusema, ni kweli majedwali yana contradictions nyingi, hakukuwa na reconciliation kati ya TzQF na stakeholder wengine.
Hakuna shaka juu ya hilo na apparently waliomaliza darsa la saba wanaonewa

Ndiyo maana nilikueleza mwanzoni VETA-VII watafute recognition kwa kupitia vyeti na si kusubiri recognition kwa makosa ya TzQF, kwamba akipata VETA afanye mtihani wa IV ili ku fit haja za waajiri kwasababu atasema 'yes amemaliza IV na ana VETA kama IV mwingine''

Kwa wakati huu Utumishi wanasema, regardless ya unafanya kazi gani, the benchmark ni IV.

Hawakusema VETA peke yao, wamesema watumishi wa umma.
Hata kama ni VII umejiendeleza ukapata CPA, kigezo chao ni IV , ni haki wakikuacha

Najua swali linalofuata, kama mtu ni std VII ana CPA na anaendesha kazi 101% kwanini tusiangalie skills zake badala ya vyeti?

Mlenge tukienda bila guideline, ipo siku tutaulizana hapa jamvini kwanini wale wauza dawa za nguvu za kiume ambazo ni miti ya asili na inafanya kazi tusiwaite Doctor kwa skills zao?

Ahsante
 
Nguruvi3,

Tatizo lililopo ni kwamba mwajiri huyo ndiye aliyetunga sera na maelekezo ya TzQF, NECTA na NACTE. Asipozifuata atakuwa sawa na meneja wa mgahawa ambaye hula migahawa jirani tu.

Hata nchi nyingine wanadhania kwamba mwajiri huyo mtunga sera anaamini sera na maelekezo yake mwenyewe. Ukurasa wa nane wa Kiambatanisho kifuatacho kinaonyesha jitihada za Uholanzi kulinganisha elimu ya sekondari Tanzania na ya Uholanzi.
 

Attachments

Mlenge kuna mambo napenda nichangie hapa baada ya kupitia majedwali kwa utulivu

1. Ahsante kwa majedwali, nakiri kabisa sijui ni wangapi wamewahi kuyaona na sijui hata watunga sheria wetu au watendaji wanajua yapo, highly doubt

Umesaidia sana umma kwa tafsiri ya mambo mengi, TzQF, NECTA na NACTE

2. Kuto majedwali ulichosema bandiko #5 na 7 nimeelewa mantiki kwa dhati

Kwamba, Form IV-VETA na Std-VII wa VETA ni kundi moja kwa certification, katika ajira kinachotumika ni cheti cha IV kama kigezo. Ni kweli na ni wrong concept, nakuliana nawe

Wote wawili wanapata cheti cha VETA wanakuwa na qualification ile ile.

Kuwahukumu kwa kilichotokea siku za nyuma si haki. Kama ni hivyo qualification hiyo ingekuwa na madaraja kwa mfano VETA grade A au B. Kwa mujibu wa majedwali sikuona hilo

Mfano mzuri ni utaratibu wa NBAA, unatambua mtu kwa sifa aliyofikia si wapi alikotokea.

Hata wizara ya afya, kama uulikuwa RMA uka upgrade na kuwa AMO, kwavile RMA imekuwa phased out, hukumu hiyo haikuhusu, unabaki na qualification uliyo nayo

3. Baada ya kuangalia hayo, upande wa utumishi nao una hoja.Kumbuka tulichojadili ni TzQF

Utumishi wana sifa zao za utumishi. 'pengine' wanaamini fundi welder IV ataweza kuchagamana na changamoto kuliko std-VII hata kama wapo daraja moja

Ni kama Employer yoyote anayetangaza nafasi za kazi, kwa mfano Daktari.

Katika sifa anataka aweze kutumia software abcd na awe na Leseni ya udereva
Hata kama waombaji wametoka chuo na darasa moja, kwanini tumlaumu mwajiri!

Nimalizie kwa kusema, ni kweli majedwali yana contradictions nyingi, hakukuwa na reconciliation kati ya TzQF na stakeholder wengine.
Hakuna shaka juu ya hilo na apparently waliomaliza darsa la saba wanaonewa

Ndiyo maana nilikueleza mwanzoni VETA-VII watafute recognition kwa kupitia vyeti na si kusubiri recognition kwa makosa ya TzQF, kwamba akipata VETA afanye mtihani wa IV ili ku fit haja za waajiri kwasababu atasema 'yes amemaliza IV na ana VETA kama IV mwingine''

Kwa wakati huu Utumishi wanasema, regardless ya unafanya kazi gani, the benchmark ni IV.

Hawakusema VETA peke yao, wamesema watumishi wa umma.
Hata kama ni VII umejiendeleza ukapata CPA, kigezo chao ni IV , ni haki wakikuacha

Najua swali linalofuata, kama mtu ni std VII ana CPA na anaendesha kazi 101% kwanini tusiangalie skills zake badala ya vyeti?

Mlenge tukienda bila guideline, ipo siku tutaulizana hapa jamvini kwanini wale wauza dawa za nguvu za kiume ambazo ni miti ya asili na inafanya kazi tusiwaite Doctor kwa skills zao?

Ahsante

Mnamo mwaka juzi (2015) Chama Tawala, kilitoa Ilani ya uchaguzi ya CCM 2015. Kupitia ilani hiyo, Serikali ya Mheshimiwa Rais Magufuli iliahidi kwamba, na ninanukuu:

========================
52 (b) Kuhuisha taratibu za kujiunga na taasisi zinazotoa elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa kutambua sifa zinazopatikana katika mifumo na taasisi tofauti ili kuhakikisha kwamba:-
(i) Asilimia 20 ya wahitimu wa Elimumsingi wanaendelea na masomo katika ngazi za Sekondari ya Juu na asilimia 80 kuendelea na elimu au mafunzo ya ufundi katika ngazi ya cheti, stashahada au shahada kulingana na sifa, vipaji au vipawa;
(ii) Asilimia 80 ya wahitimu wa Elimu ya Sekondari ya Juu kujiunga na Elimu ya Juu ya Taaluma na asilimia 20 kuendelea na Elimu ya Ufundi, katika ngazi ya cheti, stashahada au shahada kulingana na sifa; na
(iii) Asilimia 70 ya wahitimu wa Elimu au Mafunzo ya Ufundi na Taaluma wanapata ajira kwa kujiajiri au kuajiriwa.
=========================

Yaani, asilimia 20 itakuwa inaendelea na mafunzo ya sekondari. Kwa mujibu wa tafsiri ya sasa yenye mapungufu, taifa linategemea kujipatia watumishi wa umma kutoka miongoni mwa wachache tu. Wale wote wengine ambao ni wengi hao ajira ya umma waisahau tu. Wakati huohuo serikali iikitegemea asilimia 70 ya wahitimu wakijiajiri au kuajiriwa.

"Elimu haina mwisho" ndio kampeni iliyokuwa ikisikika sana zamani. Lakini kwa utaratibu wa kutambua kidato cha nne tu, ina maana ya kuwahukumu wale wasioipitia elimu ya sekondari kwamba wamefikia mwisho wa elimu. Hii kiaina ni kama kuendeleza "elitism", jambo ambalo limepigwa vita na sera ya taifa ya elimu na mafunzo 2014.

Katika sera hiyo, nanukuu sehemu ya usuli:

========
Aidha, bado Sekta ya elimu na mafunzo inakabiliwa na changamoto ya mfumo usiokidhi mahitaji ya elimu na mafunzo nchini. Mfumo wa elimu na mafunzo umetawaliwa na muundo wa kitaaluma wenye dhana ya kuchuja wahitimu ili kupata wachache wenye uwezo mkubwa katika taaluma na watakaosoma hadi kumaliza katika ngazi ya chuo kikuu. Hali hii inatokana na nafasi za elimu na mafunzo ngazi za juu kuwa chache kadri wanafunzi wanavyohitimu kuanzia ngazi ya elimu ya msingi na kuendelea, hivyo kuwa na muundo wa kuchuja badala ya ule wa kutoa fursa kulingana na uwezo, vipaji na vipawa.

…Vilevile, hakuna mwingiliano fanisi kati ya muundo wa elimu ya ufundi na muundo wa elimu ya jumla na hivyo kushindwa kuwawezesha wahitimu wa elimu ya ufundi kujiendeleza katika elimu ya juu. Pamoja na hayo, kuna ukosefu wa mfumo endelevu wa utambuzi wa sifa mbadala utakaowawezesha watu waliopata ujuzi kwa njia mbalimbali za elimu na mafunzo kujiendeleza kielimu na kuingia katika ulimwengu wa kazi. (uk 3 – 4).

Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 imeandaliwa ili kutoa mwelekeo wa elimu na mafunzo nchini kwa kuzingatia mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kisayansi na kiteknolojia na changamoto za elimu na mafunzo kitaifa, kikanda na kimataifa, ili kuongeza fursa, ufanisi na ubora wa elimu na mafunzo nchini na kufikia viwango vya rasilimaliwatu kwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. (uk 7)

Fursa za elimu na mafunzo zinapatikana kwa kila Mtanzania bila ubaguzi wa jinsi, rangi, kabila, dini, ulemavu na hali ya kijamii au kipato. Ingawa fursa hizo katika elimu ya msingi zimeongezeka hadi kufikia asilimia 92 ya wanafunzi wa rika lengwa mwaka 2012, bado uandikishaji wa wanafunzi wa rika lengwa katika elimu ya sekondari ya kawaida ni asilimia 36.6 tu na asilimia 2.7 ya wanafunzi wa rika lengwa kwa sekondari ya juu. (uk 10)

========

Kisha nanukuu matamko teule ya sera mintarafu mada husika:

==============
3.1.1 Serikali itaweka mfumo nyumbufu katika elimu na mafunzo ili kuwezesha wananchi wengi zaidi kujielimisha na kuwa huru kutafuta elimu katika fani wanayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wao.

3.2.22. Serikali itaweka na kusimamia mfumo wa kitaifa wa sifa linganifu wa tuzo kwa ngazi zote za elimu na mafunzo ili kurahisisha wahitimu kuweza kujiendeleza kielimu na mafunzo.

==============

Hiyo ni sera ya elimu na mafunzo, inalandana pia na ilani ya uchaguzi.

Kwa hiyo Nguruvi3 siyo suala la kutoenda na guidelines. Ni suala la kuziheshimu guidelines ambazo wenyewe tumezitunga, nyingine tumezitunga miaka michache tu iliyopita.

I rest my case.
 
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, ufafanuzi ulishatolewa siku nyingi, ila waajiri wana tafsiri anuai, nyingine zikiwa siyo sahihi. Inavyoonekana, miongozo iliyoko inaweza kufupishwa kama hivi kwenye kielelezo hiki hapa:

Discombobulation.png
 
Back
Top Bottom