Fohadi
JF-Expert Member
- Jul 24, 2020
- 772
- 2,421
Natambua na nathamini sana mawazo ya Mh. Rais ya kubadili mitaala yetu ya elimu ili kuwawezesha vijana kupata elimu ujuzi itakayowasaidia kujiajiri na kuajiri watu wengine.
Licha ya umuhimu wa elimu ya ufundi katika kutatua tatizo hili, bado elimu hii hii ya ufundi inaweza kuturudisha kule kule kwenye tatizo la ukosefu wa ajira na vipato kwa vijana endapo tu baadhi ya mambo ambayo yanapaswa kwenda sambamba na elimu ya ufundi hatutayapa kipaumbele au 'tutayasahau'.
Kwanini nasema hivi:
Naomba tuutazame utekelezaji wa elimu ya ujuzi na matokeo yake kwa miaka ya baadae ( Long run). Ninaamini, tukianza utoaji wa elimu kwa mitaala mipya (elimu ya ujuzi) baada ya miaka mingi (10 au 15) kutakuwa na matokeo haya:-
1. Idadi ya vijana wenye ujuzi katika ufundi wa taaluma mbalimbali kama umeme, ujenzi, magari na ufundi au ujuzi mwingine wa aina hiyo itakuwa imeongezeka sana kama jinsi ambavyo degree zimejaa leo hii. Hii itafanya katika kila kundi la vijana 10, basi 6 au 5 kati yao wana ujuzi au ufundi kutoka vyuoni.
2. Hii itapelekea hata ndani ya familia au jamii kuwe na vijana ambao pengine wamesoma ufundi unaofanana kama ilivyo leo ambapo ndani ya familia moja unakuta kuna watu wenye fani za uhasibu wapo 3. Au ndani ya mtaa mmoja unakuta watu wenye ujuzi wa maswala ya umeme wapo hata 9 au zaidi. Sasa je, ni nani atahitaji huduma kutoka kwa mwingine? ni kwa namna gani ujuzi utawasaidia hawa wasomi kujipatia kipato chao ikiwa kila mtu ana utaalamu wa hicho kitu?
Bila shaka, baada ya miaka mingi kupita (LONG RUN), tunaweza kurudi kulekule ambapo vijana wana elimu au ujuzi ambao hauwasaidii kwa namna ya kujiingizia kipato kwa sababu wasomi au wajuzi wa fani hizo watakuwa wamejaa.
Maoni kuhusu nini kifanyike ili elimu ya ujuzi iwe na tija tunayoitarajia
Binafsi, ningependa kushauri yafuatayo ambayo inabidi yaende sambamba na mitaala hii mipya ya elimu ili kuja kusaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini kwa miaka mingi ijayo:-
1. Elimu ya msingi/lazima iwe hadi kidato cha nne.
Elimu ya kidato cha nne iwe ni ya lazima ili kumjenga kifikra mwanafunzi. Baada ya matokeo ya kidato cha nne, mgawanyo wa wanafunzi ufanyike kama ifuatavyo. Wale waliopata ufaulu mkubwa hasa DIVISION ONE tu ndio waendelee na kidato cha tano na sita hadi chuo kikuu kwa hii mitaala ya kawaida katika fani muhimu kama afya, ualimu, uchumi, sheria, biashara, kilimo, uhandisi n.k. Hili kundi litaandaliwa ili kuja kuwa wasimamizi au waajiriwa katika fani hizi. Na ni vema kuchukua Division one pekee ili kuzuia SURPLUS ya wataalamu kwenye fani hizi ukilinganisha na soko la ajira.
DIVISION TWO NA THREE hawa waende moja kwa moja katika vyuo vya ufundi katika fani mbalimbali kama umeme, kilimo, uchongaji, ushonaji,ujenzi n.k ili kutengeneza wataalamu ambao watasaidia kujiajiri na kutengeneza ajira kwa wasimamizi wale juu.
DIVISION 4 NA ZERO kwa utafiti wangu mdogo, asilimia kubwa ya wanafunzi kwenye kundi hili, huwa sio wazuri kwenye masomo na muda wao mwingi wanautumia kwenye fani wazipendazo. Hapa inatakiwa kuwe na shule maalumu za michezo na Sanaa kama mziki, uigizaji, uchongaji n.k ili kuwasaidia hawa kupata ujuzi zaidi katika fani zao. Hapa tutazalisha wasanii wazuri ambao watapata fursa mbali mbali ndani na nje ya nchi na kutengeneza ajira kwa wengine. Nadhani tukipata wasanii 15 kama Diamond, kuna ajira nyingi zitazalishwa na hii inawezekana mbona Nigeria kuna wasanii wengi wakubwa. Na wale wasanii ambao hwatakuwa wakubwa basi angalau watakuwa na kipato cha kuendesha maisha yao kwa uhakika.
NB: Kuwe na shule maalum za vipaji mbalimbali kama soka, netball, tennis, ngumi n.k. Tukiwafundisha watoto wenye fani hizi kuanzia chini basi ni rahisi kuzalisha akina samatta, hasheem thabit, mwakinyo na wengine wengi kimataifa. INAWEZEKANA.
2. Uboreshaji maslahi ya watumishi wa umma.
Hili kundi likiweza kufanyiwa haya, litaweza kuhitaji huduma kama kujengewa nyumba mpya, umeme na huduma zingine za kiufundi ambapo vijana wetu waliosoma VETA kupitia kujiajiri kwao watauza huduma kwa kundi hili. Bila hivyo, vijana wetu wenye ujuzi wataishia kukosa sehemu ya kuuza ujuzi wao.
3. Tax exemption na Grace periods kwa wawekezaji wadogo wadogo.
Vijana wengi wana ideas na wana taka kuwekeza na kukuza biashara zao. Ila tatizo linakuwa kodi ambazo zingine wanatakiwa kuanza kuzilipa hata kabla ya kuanza kusimama vizuri. Kukiwa na tax exemption kwa kipindi Fulani, itasaidia kukuza biashara hizi na kuzalisha ajira nyingi sana kwa wengine na kuajiri hata vijana wetu wa VETA. Hii iende pamoja na uongezaji wa utoaji mikopo isiyo na riba kwa vijana huku serikali ikifatilia kuhakikisha mikopo hiyo/mitaji inatumika na kuleta matokeo yaliyotarajiwa.
4. Mazingira mazuri ya uwekezaji hasa kwa wawekezaji wa nje.
Kundi hili linauwezo wa kuzalisha ajira nyingi kwa wakati mmoja. Hili halihitaji maelezo mengi maana mifano ni mingi na nashukuru Mh. Rais ameliwekea msisitizo mkubwa.
5. Mazingira mazuri kwa asai za kiraia.
Asasi za kiraia (NGOs) zina mchango kubwa sana katika kuzalisha ajira kwa watu wengi. Kuna NGOs nyingi sana ambazo zinatoa ajira kwa wengi na kuisaidia serikali. Na faida nyingine hizi asasi zinasaidia jamii kwa kutatua kero za beneficiaries wao. Ushauri wangu ni kwa serikali kuzisimamia hizi asasi ili ziweze kufanya kazi zao kwa ufanisi kwa kufata sheria, taratibu na kanuni za nchi na pia kufanya shughuli zao kwa UFANISI kama zilivyo kwenye documents zao za usajili.
6. Family Planning
Hapa nashauri mkazo uwekwe ili kuweza kuwa na idadi ya watu ambayo inaendana na rasilimali zilizopo. Kila mwaka idadi ya watoto wanaoanza shule inaongezeka kwa sababu watoto wanaozaliwa ni wengi sana. Hata tukitoa elimu ya ufundi kuanzia darasa la saba, bado tutakuwa na vijana wenye ujuzi huku wakibaki tegemezi kwa kukosa sehemu ya kufanya kazi au kuuza ujuzi wao maana idadi yao ni kubwa sana. Ni vyema tukaweka mkazo mkubwa katika agenda hii pia.
7. Mifumo mizuri ya ukusanyaji kodi.
Naunga mkono kama ambavyo mh. Rais anasisitiza uwepo wa mifumo mizuri ya ukusanyaji wa kodi na matumizi ya pesa za umma. Asilimia kubwa ya mambo niliyoshauri yanahitaji uwezo mzuri wa serikali kiuchumi. Huwezi kutoa tax exemption kwa vijana kama huna pato la kutosha. Huwezi kujenga vyuo vya ufundi kama huna pato la kutosha. Basi mifumo ya ukusanyaji na usimamizi wa kodi iboreshwe.
8. Ubanaji wa matumizi ya serikali.
Mbinu za ubanaji na upunguzaji matumizi ya serikali zipo na ambazo zinaweza kutumika ili pesa hiyo ikatumike katika moja ya mambo niliyoyagusia hapo juu ili kuleta tija katika elimu yetu ya ufundi. Tunaweza punguza idadi ya wabunge na wawakilishi na kupunguza mishahara yao na posho, na pia tukaamua nafasi moja kati ya Mkuu wa wilaya au mkurugenzi wa halmashauri ikavunjwa. Na tukafanya mengi kama alivyofanya Mwendazake kuvunja Halimashauri ya Jiji la DSM ili kubana matumizi na kuleta maendeleo kwa watanzania.
MWISHO
Elimu ya ufundi ni muhimu na ina tija ila nina amini itakuwa na tija Zaidi endapo hayo niliyoyashauri na mengine mazuri yaliyo/yatakayoshauriwa na wengine yatasimamiwa vema na kupewa kipaumbele sambamba na mitaala yetu mipya ambayo ni mizuri ili kupata matokeo chanya in LONG RUN.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA – Kazi Iendelee.