Elimu ya unajimu

Elimu ya unajimu

Najua kama tumetofautiana Imani, mitizamo pamoja masuala ya kiitikadi. Lakini nipo hapa kwa ajili ya wale wote wanaotaka kuisoma hii elimu na kuweza kuwasiadia wenyewe katika mambo yao binafsi.

Mi nina kazi mbili tu kwenye unajimu ambazo ni kufundisha na kutoa ushauri kuhusiana na masuala ya nyota.

Nilikua natak niandike makala ndefu ambayo ningeeleza mambo mengi kuhusiana na hii elimu, lakini nikagundua tayari si wote watakaoelewa na kuamini kutokana na background ambayo kila mtu ametokea.

Hivyo sitaki kusema sana hapa kuhusiana na hii elimu kwa sababu kuibadilisha imani ya mtu ambayo imejengwa miaka takribani 20 si kazi ndogo. Maana nina uhakika 100% humu ndani kuna watu ambao nawaheshimu sana, sasa sitaki ifike pahala tutoleane kauli mbovu kwa sababu ya bandiko hili.


Nimetumia miaka 2 na nusu kuisoma hii elimu. Nimesoma course hizi zote kupitia online. Na kuanzia machapisho, majarida, vipeperushi, vyote nimesoma kwa lugha ya kiingereza. Lakini mimi nitafundisha kwa kiswahili kwa faida ya wote wasiofahamu vyema lugha ya kiingereza.


Branches of Astrology. (Matawi ya Unajimu).


Kwanza tufahamu matawi muhimu ya Astrology (Unajimu). Ambayo yapo mengi, yanaweza kufikia hata 9. Lakini yenye umuhimu mkubwa na maarufu yapo manne ambayo ni;

1. Mundane astrology
2. Natal Astrology
3. Horary Astrology
4. Election astrology.

Katika kozi yetu tutaanza na tawi la Natal Astrology, hilo ni tawi muhimu na lina mambo mengi sana.

SYLLABUS YA NATAL ASTROLOGY.

Huu ni mtaala ama mambo ambayo kwa mwanafunzi yeyote anayeanza unajimu unatakiwa ajifunze na kuyajua. Nitafundisha kwa kiswahili ingawa kuna maneno mengine tafsiri zake hazipatikani ama hazieleweki kwa kiswahili. Kwa hiyo kwa maneno machache kama hayo ambayo tafsiri zake hazipo basi tutatumia kiingereza. Lakini 95% ya masomo yetu tutatumia kiswahili ili kila mmoja aelewe.


Kwa watakaojiunga na group jipya watajifunza mambo haya;

DARAJA LA KWANZA. (level 1.)

1. Historia ya unajimu.

2. Ten planets (sayari 10)

Sun, Moon, Mercury, Venus, Mars, Jupiter, Saturn, Uranus, Neptune, Pluto.

3. Twelve zodiac sign (alama au maumbo 12 ya Nyota).

Aries (Kondoo), Taurus (Ng'ombe), Gemini (Mapacha), Cancer (Kaa), Leo (Simba), Virgo (Mashuke), Libra (Mizani), Scorpion (Nge), Sagittarius (Mshale), Capricorn ( Mbuzi), Aquarius (Ndoo), Pisces (Samaki).


4. Twelve houses (nyumba 12).

Kwa hapa nitataja mambo makuu (viwakilishi) katika kila nyumba ila tukifikia hii kozi basi tutasoma kwa undani zaidi.


Nyumba ya 1: Muonekano wa mwili mitazamo yako kuhusu dunia.


Nyumba ya 2: Kipato, utajiri, mali unazomiliki, namna unavyoingiza na kutumia pesa yako binafsi.


Nyumba ya 3: Ndugu zako, maduka, Jirani zako,vyombo vya mawasiliano, vyombo vya usafri, safari fupi (ndani ya jamii yako).


Nyumba ya 4: Nyumbani ulipokulia, familia, historia yako ulipotokea, makazi, ardhi, kilimo, Taifa, asili yako, makabila, uzalendo, hisia.


Nyumba ya 5: mtoto wako wa kwanza ,sherehe, mapenzi,michezo na anasa za kila aina, elimu ya awali, uwekezaji, kamari, ubunifu.


Nyumba ya 6: Kazi unazofanya kila siku (kujitolea au kulipwa),usafi binafsi, mifugo, chakula, matunda, afya, utumishi, jeshi la nchi. Mazoezi.


Nyumba ya 7: Mkeo au mumeo, ndoa, mikataba, amani, mahusiano ya kila aina, mpinzani, biashara, rafiki wa karibu, mapatano.


Nyumba ya 8: Mali ya mkeo au mumeo, Madeni, kodi, mabadiliko, kufa na kuzaliwa, zinaa, umasikini, vita, michango ya aina zote, talaka, chini ya ardhi na vilivyomo, magenge ya kihalifu.


Nyumba ya 9: Elimu ya kiwango cha juu, safari za mbali, nchi na tamaduni za kigeni, dini, bahati nasibu, falsafa, sheria, ndugu wa mkeo au mumeo, mjukuu wako, utalii.


Nyumba ya 10: Heshima,Ufalme, Mamlaka, Serikali, cheo, mahakama, jinsi watu wanavyokuongelea,
mafanikio.


Nyumba ya 11: Marafiki, Makundi tofauti ya watu, malengo, matumaini, sayansi na taknolojia, ugunduzi, mitandao ya kijamii, asasi za kiraia, wanaharakati, mambo ya ghafla, mambo yote mapya.


Nyumba ya 12: Hujuma, majini na mashetani, jela, hospitali, wagonjwa wasiojiweza, ala za muziki, filamu, wapelelezi, maadui tusiowaona, siri, ugaidi, kujitoa kafara, pombe, madawa ya kulevya, mauaji, majuto, mafichoni, ndoto, maono. Uwongo, simanzi, utabiri, unabii.


Hizo ni nyumba ambazo tutazisoma nimetaja mambo yake machache tu.


Baada ya hapo tutaangalia kitu cha mwisho katika daraja la kwanza ambacho kinaitwa aspects.


Hapa kwa nyie mnaoanza tutaangalia aspects 5 tu lakini zipo nyingi sana.

Tutaangalia hizi zifuatazo:

1. Conjunction

2. Sextiles

3. Square

4. Trine

5. Opposition.


Ukimaliza hayo utakua umemaliza basics ( msingi) wa unajimu. Ni kama mtu ambae kamliza form one. Baada ya hapo tutaingia form two.


Kwa watakaofanikiwa kumaliza daraja la kwanza tutaendelea nao daraja la pili. Ambalo ni muendelezo wa haya ya daraja la kwanza.

Kwa wanaohitaji kusoma elimu hii nicheki WhatsApp, kwa namba hii 0782 82 11 77.

Nitakuadd kwenye group la WhatsApp kwa malipo ya 3000 kwa mwezi. Hii ni kwa sasa hivi kwa watakaochelewa na kukuta kundi lishajaa basi watakaonza na kundi jipya malipo yatakua 5000.


Mwisho kabisa, nawapa nafasi mniulize swali lolote kuhusiana na unajimu, nami ntawajbu hapa hapa. Swali litakaloambatana na kejeli, dharau au matusi sitalijibu.
Mkuu nipe namba yako ya wasap au nichek 0625352984
 
Maneno mengi mkuu elimu ndoto, usijidanganye kwa kupitia vielimu vya online na tuvijitabu tulioandikwa na mtu kama wewe kila siku zinavyozidi kwenda hii elimu ndio inavyozidi kupotea na kufichwa na kuanzishwa vimambo mambo vya astrology na blah blah za numerology, hiki unachokizungumzia hapa ni numerology wewe na sio astrology elewa hizi unazozielezea hapa ni elimu ya namba na unataka ionekane kama elimu ya magimba hapana numerology ni mjukuu wa world knowledge (ilmu duniya) ambaye ndiye baba wa astrology na astrology ndio mtoto wa Elimu dunia na ndio mzazi wa numerology na vinyago vingine kama psychic powers na abilities..

Hivyo elewa kuwa hivi ni vya kuokota okota tu kwenye ilmu dunia ambayo kama umezaliwa zamani kidogo utafahamu kuwa kipindi cha enzi za mababu watemi wafalme na wakubwa wengine walikuwa wakiona muda wao wa kuondoka umekaribia wanakusanya mavitabu na elimu walizopata na kuchomelea mbali moto au kuzika na kuipoteza kabisa hii elimu isipatikane, chanzo cha elimu hii ni Nchi za Kiarabu ila ndio hivyo watu wakishatokea wakajitangaza wanacho kitu basi huonekana wao ndio waanzilishi, sometimes usiamini kila jibu linalotoka google mkuu,

Mfano mzuri ni hapa kwenye hii thread si unaona wewe umeanzisha?
Lakini mimi kwa kukurekebisha kwangu kidogo tu, naweza nikapata watu wengi wa kunisikiliza na kunielewa zaidi na wakasema hii thread alianzisha Rakims,

Ndio hii elimu ilivyovurugwa na kupotezwa, unategemea kama dunia nzima ingefahamu ukweli kuhusu elimu hii Leo ingekuwa wapi?

Rakims
Yeah hii elimu inachokonoa sana uwezo wa MWENYEZI MUNGU. Ambayo ndiye hutangaza mwisho utakuwaje tukiwa mwanzoni tu, unafikiri mtu akijua anakufa kesho unadhani itakuwaje? Hiyo kazi aliwaachia manabii anaowaamini
 
Kwanza kabisa nitoe pongezi nyingi sana kwako uliyeuliza hili swali. Inaonesha una kiwango kikubwa sana cha ustaarabu.

Pia zingatia kwamba Unajimu kwa sehemu unahusu mambo yajayo. Hivyo wakati wowote unapotaka kupanga kuhusu mambo yajayo, lazima umfuate mnajimu au uwe unaelewa kuhusiana na unajimu.
Kwa sababu Astrology is the science of probability.

Nahitaji watu wajifunze unajimu, kwa sababu mfano mkubwa ni maisha yangu binafsi kabla na baada ya kujifunza unajimu.

Swali la 1; kwa nini unataka tujifunze unajimu?


Jibu; Ili nijibu swali lako kwa mapana, yafaa nitumie matawi ya unajimu ziwe kama hoja ya kujibia swali lako. Kwa sababu kila tawi lina kazi yake.


MUNDANE ASTROLOGY.

Hili ni tawi linalohusu mambo ya nchi na miji mbalimbali yatakavyokua katika siku zijazo. Kuanzia hali yake ya kisiasa, Uchumi, Majanga na mengine mengi kuhusu eneo hilo kwa ujumla.

Hii ndio tawi kongwe na la kwanza kuliko matawi yote ya unajimu. Hili tawi lilikua linatumika kuwashauri wafalme na watawala mbalimbali kuhusiana na hali ya kitaifa kwa ujumla.

Kwa hiyo ukijifunza tawi hili itakuwezesha kujua hali ya mataifa mengi sana duniani. Kwa sababu kila Taifa limeweka chart yake mtandaoni. Mpaka chart ya Tanzania ukiitaka mi ninayo. Ila siiwezi nikaiweka hapa.

Ili uweze kufanya utabiri hapa inabidi uwe na chart ya nchi husika. Binafsi ninazo chart karibia ya nchi zote.

HORARY ASTROLOGY.

Hili tawi kazi yake inakuja, pale tu unapokua una swali halafu hujui hatma yake itakuaje. Yaani kwa mfano kuna mtu yupo nje ya nchi halafu anakupa ahadi kwamba atakufanyia mpango nawe uende alipo yeye. Lakini ukawa na mashaka huenda safari isiwepo kwa kuhisi labda anakudanganya. Unaweza ukachora chart maalum ambayo inaweza kujibu swali lako.

Kazi kubwa ya tawi la horary ni kutoa jibu la ndio au hapana. Sasa kama utajiuliza swali kama hili;

Je nitasafiri?

Basi hapo utachorewa chart maalum kutokana na muda ulioulizwa swali na mahali.


NATAL ASTROLOGY.

HIli ni ndio tawi lenye umuhimu mkubwa sana kuliko tawi lolote lile. Hapa ndo utajua kila kitu kuhusu. Na mnajimu ili akupe shauri lazima akuchoree chart ya natal.

Kinachotakiwa kwenye natal astrology, ni tarehe yako ya kuzaliwa, muda ulozaliwa (saa na dakika kama unazikumbuka). Mji ulozaliwa. Hivi ndio vitafanya sisi tujue mambo mengi kukuhusu wewe.

Hapa utapata ushauri ama kujua wewe kama ukijifunza, ni shughuli zitakuletea mafanikio maishani na zipi zitakuangamiza. Kwa ujumla inajibu chochote unachotaka kuhusu wewe na maisha yako. Siwezi nikaorodhesha vitu vyote hapa.

ELECTION ASTROLOGY.

Hili tawi ukijifunza kazi yake ni kukusiadia kuchagua muda muafaka wa kufanya jambo lako lolote muhimu ili liweze mafanikio ya muda mrefu. Inaitwa the art of timing.


Kwa ufupi kila tawi lina faida zake tena nying mno. Na hayo matawi jumla yapo 9 ila hayo manne ndio common.

Mpaka hapa ntakua nimejib swali lako la 1. Ntaendelea maswali hapo baadae. Nakuahidi ntakujibu yote.
Hiyo elimu ya Unajimu inazidi elimu ya Meditation & Third eye kwà maarifa?
 
Unajimi na hesabu, Nataka nishinde jackpot , au nitengeneze jackpot yangu mwenyewe ili nishinde ,
 
Back
Top Bottom