Elimu ya Uraghbishi na jinsi inavyosaidia jamii kujikomboa katika maendeleo

Elimu ya Uraghbishi na jinsi inavyosaidia jamii kujikomboa katika maendeleo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Maana ya Uraghbishi
Si rahisi kuwa na maana moja kamili ya Uraghbishi, hii ni kwa sababu Uraghbishi ni falsafa, mtazamo na namna ya kuwachochea Wananchi washiriki kwa pamoja katika kujiletea maendeleo yao. Uraghbishi ni mtindo wa maisha.

Lengo la Uraghbishi
Kuwahamasisha wanajamii katika ngazi zote, kuwachokoza kifikra ili wakumbuke kwamba wao ndio watendaji wakuu katika maisha yao.

Wananchi wajione kwamba wao si wanyonge, hawalazimiki kungoja msaada na kugundua
kwamba mabadiliko ya hali zao yanaletwa na wao wenyewe.

Kuwakumbusha wananchi kuwa wajasiri katika kutimiza wajibu wao, kuhoji viongozi wao na kutetea haki zao.

Kuwaona wanaume na wanawake kama watu wenye ubunifu kamili juu ya mazingira yao.

Kuibua vipaji vya watu ambao hapo awali walijiona wamenyimwa haki kwa kuwapa natasi ya kubuni na kushiriki katika mabadiliko na maendeleo ya jamii zao.

Uraghbishi unafanyika wapi?
Nchini kote wapo watu wengi wanafanya Uraghbishi, wengi hata hawajui kama wanatanya Uraghbishi kwa sababu wengi wao wanasukumwa na hulka zao tu kuwatia moyo wananchi kushiriki kikamilifu katika mipango na shughul mbalimbali za maendeleo.

Hata hivyo, Twaweza imekuwa ikishirikiana na mashirika mengi ya kijamii na asasi za kiraia
katika kuendeleza dhana hii ya Uraghbishi ili kuweza kuongeza ushiriki wa wananchi, kuboresha uwezo wa serikali za mitaa na kuimarisha upatikanaji wa huduma za jamil katika wilaya tano nchini. Wilaya hizi ni Kigoma-Uji, Lindi, Maswa, Mbogwe na Pangani

Sifa za Mraghbishi
Kiu ya haki kwa wote, hasa wale ambao wamenyanyaswa, kukandamizwa, kunyonywa,
kupuuzwa, kusahauliwa na kutengewa na mfumo.

Imani kwamba binadamu wote wana uzoefu na ubunifu wao na hamu ya kuona kwamba uwezo na ubunifu huu unapewa uzito unaostahili.

Uwezo wa kuwachokoza watu ili waweze kuchambua hali halisi inayowakabili na mbinu za uibadili hadi wachukue hatua wenyewe.

Uwezo wa kuwasiliana na watu kuwawezesha kama mwenzao.

Uwezo wa kukabili hali ya migogoro na hata ugomvi
 
Back
Top Bottom