Marco Polo
JF-Expert Member
- Jan 16, 2014
- 11,786
- 18,562
Ukiangalia matokeo ya form vi toka Brn ianzishwe yamekuwa yakipanda mwaka had mwaka..... Mm binafsi huwa najiuliza ni nn kinacho boost matokeo yao ikiwa walimu morali yao ya kufanya kaz iko vile vile kutokana na kudai haki zao nying tu...... Pia syllabus ni zile zile, topics ni zile zile, sasa ni kitu gan kilichobadil upepo wa matokeo?......... Kabla ya hii BRN mtu wa PCB alikuwa akipata ccc 1.9 alikuwa na uhakika wa kusoma MD chuo chochote alichohitaji leo hii mtu huyo huyo kupata hiyo MD ni mbinde je ndo kusema wanafunzi wa sssa wana bidii sana kwenye masomo yao kuliko wale wa kabla ya hii BRN? ......... Naomba tujadili wakuu.
Roho mbaya zitawaua ,ingekua viwango vya ufaulu vinashuka ungelaumu ,Leo vinapanda unalaumu !!
Je unatakaje ?
Acha kuropoka Kuna post moja ulisena ufaulu umeongezeka kwa vile vitendea kaz ambavyo havikuwepo huko nyuma vimeongezwa....... Nikakuuliza naomba unitajie hivyo vitendea kaz hujanijibu mpaka Sasa.
Hiyo post nahisi imefutwa
Ila mkuu mbona hujibu maswal yangu hapo juu? Hakuna mtu mwenye Roho mbaya hapa.... Jadil hoja na uache ku attack watu
Jibu mbona rahisi tu "kujituma"
Watoto wanajituma walimu kugoma sio sababu ya wao kufeli mitihani ,
Kuna tuition
Kuna usomaji Wa makundi au team work mwisho Wa siku wanavuna walichopanda kwa pamoja
Kwangu Mimi hakuna mfumo mgumu kama BRN mfano mwanzo ukipata alama 25 kwenye mtihani unakua na D ila BRN 25 sawa sawa na E ni failed endapo ukiipata hivyo basi hii hupelekea wanafunzi kujituma hata kama walimu wana migomo baridi
Ndio mana wanatusua ipasavyo
Hongera umejibu nilichokuuliza.... Kwahiyo kabla ya hii BRN wanafunz walikuwa Hawajitum, kulikuwa hakuna team work, tuition?
Na je hivyo ulivyoandka hapo juu ndo vitendea kaz vilivyoongezwa sio?