Elimu yetu iwe ya mfumo wa 6+3+2+3, miaka 20 mtu kashahitimu chuo

Elimu yetu iwe ya mfumo wa 6+3+2+3, miaka 20 mtu kashahitimu chuo

Wazazi wako hawakuwa na uwezo wa Housegirl ila Sera yetu Inataka miaka 7 na mwaka huu wengi wamerudishwa nyumbani
Huu Mfumo wa miaka saba kuanza shule Tulicopy kutoka kwa waingereza.
Of which sio mbaya, ila tatizo tulicopy kitu kiomoja tu Umri pekee, badala ya kucopy na Mfumo wao wa Elimu.
Physiologically and Philosophically inaaminika kwamba Mtoto kuanzia kuzaliwa had miaka 6, Huwa anajifunza kutokana na mazingira(Kumbuka hata lugha anayoongea hajafundishwa amejifunza kwa kusikia zaidi hafundishwi. Sasa kutokana na hili uakaanzishwa huo utaratibu kwamba mtoto anaanza kufundishwa akiwa na miaka 7, yaan kwa kifupi ni kuanza Kuchanganya Anachoambiwa na kile ambacho amejifunza.

Ila wao kuna kitu kinaitwa Montessori/Academy ambazo huku kwtu hakuna, Dogo wa miaka 2,3,4,5 anashindiliwa madude tu wakati inatakiwa Mwalimu ndio ajifunze kwa mwanafunzi, Sasa kwenye Hizi shule kuna walimu maalumu ambao wana fanya monitoring ya mtoto na kugundua kuwa ana uelekeo gani; Kisha watatoa COmment kwa mzazi husika, ili anapoanza Kufundishwa aelekee shule ya Mlengo husika.
Ndio maana wao wanaenda Direct kwenye point, maana anatengenezwa Mapema sana.
Ndio maana kumekuwa na watoto wengi sana wanaofaulu darasani lakini Maisha wanafeli, Kuna tofauti kati ya Elimu na Akili/maarifa; nchi za Ulaya na Amerika wamejikita sana kwenye Maarifa; hata pepa zao maswali ni yale yanayohusiana na Operation za Ktengo husika, So mambo ya Kitu fulani kilizinduliwa mwaka gani? Sijui nani alifanya nini mwaka gani? No, hiyo ni history tu, ambayo haisaidii chochote katika utendaji wako, isipokuwa kujaza ubongo na mitaarifa isiyo na msaada.

Kwa huko Tz, asilimia kubwa ya Wanafunzi/wahitimu wa Form six, Mtu hajui anataka kuwa Nani (Professionally). Kutokana na Mifumo yetu Unakuta Mtu anasukumwa kusoma Kozi fulani kutokana na TCU wamempangia, Au Kozi anayotaka hawatoi Mkopo na yeye hana uwezo hivyo anachagua kozi yenye Mkopo.

Ulaya Passion ndiyo inaamua sio mihemko, Ndio maana watu wanafanya perfomance vizuri sana; Kama kuna kitu muhimu kinatakiwa basi Passion ya kufanya unachofanya, yaan kiu ya ndani ya Mtu.

Kwa Kipindi nimekaa huku, nimegumdua mdhaifu mengi sana kwenye Elimu yetu; Inahitaji modification kwenye Mfumo ili ilete Tija miongoni mwa wanaoipokea.

Kwako Mto mada, hata kama umri utapunguzwa kama mfumo wa Kudeliver Elimu utabaki hivyo hivyo, Basi ni ukweli itachukua muda mrefu sana nchi yangu Kufikia Level za juu kwenye Elimu na Utendaji. Umri sio tatizo, tatizo Mfumo wa Elimu, haujawekwa kuwatengeneza watendaji;
 
Back
Top Bottom