sina hakika sana kama uzi kama huu ulishawahi jadiliwa humu JF, kama tayari basi uunganishwe na kama bado naomba nitumie time yangu hii niwashirikishe hili japo kwa ufupi.
kujieleza kwa daktari huchangia 80%-90% kujua ugonjwa, na 10% zilizobaki ni vipimo mbalimbali mfano vya maabala. kumbe sehemu ya kuhojiwa na dakatari ni muhimu sana kwanza kwa mgonjwa kujieleza vizuri, lakini pia kwa daktari mwenyewe kuwa na " sanaa" ya kuuliza maswali na kumsikiliza vizuri mgonjwa. na mgonjwa asishangae kuona anaulizwa maswali yaleyale na madaktari mbalimballi wajibu wake ni kujieleza.
ikumbukwe pia kuongea ukweli, madaktari wamekula kiapo kutunza siri za wagonjwa, kuna mswali yatakupasua kichwa itabid ujibu tu. mfano (kama una mchepuko, kama uliwahi toa mimba, kama uliwahi tumia dawa za kulevya, kama uliwahi shiriki mapenzi ya jinsia moja, kama uliwahi kuwa na magonjwa ya zinaa n.k) usiogope kujieleza madakari washasikia mazito mengi zaidi ya hayo.
Duniani kote mfumo wa kuhoji maswali kwa wagonjwa ni uleule, Hivyo kila swali lina maana yake. na huweza hufuata mtiririko huu.
1.utambulisho 2.matatizo ya mgonjwa 3. ufafanuzi wa tatizo moja baada ya lingine 4. hali ya sehemu za mifumo ambazo haziumwi 5. historia yako tiba tofauti na ugonjwa wa sasa 6. kwa wanawake historia ya uzazi 7. historia ya kifamilia na kijamii.
baada ya hapo unafanyiwa vipimo kwa mikono ya dakari na vifaa mbalimbali vya kawaida.
1.UTAMBULISHO/INTRODUCTION.
hapa daktari anauliza taarifa za kumtambulisha mgonjwa. majina kamili, anapoishi (hii husaidia kwa sababu kuna magonjwa yapo eneo fulani tu) dini (hii husaidia kwani baadhi ya dini hawatumii nyama ya "mdudu" hivyo ni ngumu kuwa na minyoo ile itokanayo na nyama yake), umri, na jinsi ya mgonjwa. pia maasiliano na majina ya ndugu wa karibu.
2. MATATIZO/CHIEF COMPLAINS
Hapa ni sehemu fupi ila pagumu saana kwa wagonjwa kujieleza. hapa inamaanisha utaje dalili zilizokupeleka hospitali bila kuelezea kwa undani. na katika kutaja unafuta mtiririko mzuri kuwa kipi kilianza kipi kikafuata. mfano kichwa kuuma, homa, tumbo kujaa gesi, kukohoa n.k tena unataja ulianza kuumwa lini hii ni muhimu sana kwa sababu kichwa kuumwa na homa ya siku tatu huenda daktari akaanza kujifikiria malaria, lakini ikiwa dalili hizo hizo ila ni miezi 6, haiwezekani ikawa malaria hapo. hapa utakuta mgonjwa anajieleza eti ana U.T.I sijui mara ana pressure, yule naye atasema ana tezi dume.. hapa hutakiwi kutaja ugonjwa hata kama ulishawahi pimwa.
3. UFAFANUZI WA MATATIZO (HISTORY OF ILLNESS).
Hapa ndo pa kujimwaga kuelezea shida moja baada ya nyingine. KWA KILA SHIDA utaulizwa haya yafuatayo.
-dalili hiyo ilianza lini?
-ilianzaje? ghafla au taratibu
-je tatizo linaongezeka siku kwa siku au lipo vilevile?
-je kitu gani kinaongeza dalili hizo.. mfano kulala flati, chakula, baridi nk?
-kitu gani kinapunguza tatizo hilo.
kisha daktari anamalizia maswali kwa kujiridhisha kuwa sehemu zingine za mfumo wa mwili ambapo umepata ugonjwa zipo salama. mfano kama unalalmika kuwa unatapika kwa siku 6. daktari ata uliza maswali ya mfumo wa chakula, mfano kama unaweza kumeza chakula, tumbo kuuma, kuharisha n.k
lakini pia sehemu hii unajieleza historia ya ugonjwa uliokuleta hospitali, ikiwa ni pamoja na dawa ulizotumia, na vipimo ulivyofanya.
inatosha kwa leo... ntamalizia yaliyo baki siku nyingine.