Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa heshima na taadhima napenda kuelezea utaratibu muhimu wa kujieleza kwa daktari ili kurahisisha upatikanaji wa tiba kwa usahihi.
UTANGULIZI
Ni ukweli usiopingika kuwa wengi wetu hatujui ni jinsi gani tujieleze kwa daktari ili tuweze kupata tiba sahihi na kwa wakati.
Pia kuna wakati tunashangazwa na baadhi ya maswali tunayoulizwa na daktari ambayo kuna muda yanaonekana kuwa hayana uhusiano na tatizo linalotusumbua.
Nimeona ni vyema nikaelezea ni taarifa zipi muhimu za kumuelezea daktari ili aweze kufikia hitimisho la kubashiri tatizo lako.
1: Tatizo Kuu(main complaint)
Hapa unatakiwa kumueleza daktari ni kipi kinakusumbua mpaka ukaamua kumuona.ni muhimu sana kueleza tatizo hili limechukua muda gani.
Mfano miaka kadhaa, miezi kadhaa, wiki kadhaa au siku kadhaa au limekuwa likijirudia mara kwa mara kwa muda flani.
Kwa mfano, kukohoa kwa zaidi ya wiki mbili kunaweza kusababishwa na kifua kikuu,kansa au ugonjwa wa moyo, kukohoa kwa wiki moja yaweza kuashiria ni homa ya mapafu, kukohoa kwa masaa kadhaa yaweza kuwa umepaliwa na chakula, kukohoa mara kwa mara yaweza kuwa ni pumu n.k
2: Historia ya tatizo
Hapa unatakiwa kueleza tatizo lako limeanza vipi, linatokea wakati gani(usiku, mchana au muda wote), linahusiana na nini mfano kukohoa na kutapika au tumbo kuuma na kuharisha.
Pia eleza kama tatizo lako linaongezeka au kupunguzwa na kitu flani, mfano unakohoa sana unapolala chali au moyo unakwenda mbio unaposimama lakini unapata afadhali unapochuchumaa au kiungulia kinapungua unapomeza vidonge vya magnesium n.k.
Kwa lugha fupi ya kitabibu maelezo ya ugonjwa wako yatafuata acronym ya DOPARA(Duration, Onset, Periodicity, Associating factors, Relieving or Aggreviating factors).
3: Historia ya afya yako kwa ujumla
Hapa unatakiwa kujieleza kwa ujumla kuhusu afya yako toka uzaliwe. Je umewahi kutibiwa kwa tatizo hilo hilo? Umewahi kulazwa hospitali kwa tatizo lolote, umewahi kufanyiwa upasuaji? Usiogope kutaja hata kama ulitibiwa kwa dawa za kienyeji.
Pia ni muhimu kueleza dawa au tiba zozote ulizowahi kupata miaka kadhaa nyuma au siku chache kabla ya kufika kwa daktari anayekuona mda huo.
Mfano tatizo lako kwa sasa ni mimba kutoka na hapo hapo ukawa na historia ya kutoa mimba kadhaa hapo ulipokuwa kigoli yaweza kuelezea kuwa shingo ya uzazi imelegea. N.k
Pia ni muhimu kumueleza daktari kuwa kuna baadhi ya dawa zinakuletea mzio(allergy)
4: Historia ya kifamilia
Kuna baadhi ya magonjwa yanasababishwa na lifestyle zetu na pia kuna baadhi ya magonjwa ni ya kurithi hivyo ni muhimu kueleza masuala ya kifamilia kwa ujumla.
Mfano babu, baba, mama au bibi walikuwa na tatizo flani kuna uwezekano na wewe ukawa nalo.
Mtoto anaweza kuwa na tatizo la utapiamlo kisa mama ni mfanyakazi wa TBC na hivyo hapati muda wa kumnyonyesha au mume ni dereva wa magari ya mizigo ya kwenda zambia na hivyo kamuambukiza mke wake UKIMWI n.k.
Haya ni baadhi ya maelezo muhimu yanayotakiwa kutolewa kwa daktari ili kufanikisha ugunduzi wa ugonjwa wa mteja
aliyefika kupata huduma.
Yanaweza kubadilika kidogo kulingana na mazingira ya mgonjwa au tatizo lakini huu ndio msingi wa kujieleza kwa daktari.
Baada ya kutoa maelezo haya daktari anatakiwa kukufanyia uchunguzi wa mwili(physical examnation) ili aweze kylinganisha na maelezo yako na baada ya hapo atakuandikia vipimo(investigations) ili kupata ugonjwa halisi unaokusumbua.
Kwa leo niishie hapa...
Aksanteni!
=============
Feb 2016: Nyongeza toka kwa mdau mwingine
humo pekundu, ndio nini hasa hicho ulichokiandika, yaani english language hovyo,hadi kiswahili nacho,kweli tuna miongo kadhaa kutoka hapa tu;lipo kwenda hatua moja mbele, wacha mchina aongoze kiswahili maana hakuna namna kama waswahili wenyewe ndio hawa.Meningts nakukubli sana MD ushauri ulio utoa una faida sana. Naomba kuchangia wakat mwngne napo kujieleza sana huwa kuna changia usfanyiwe lab investgation inavyo takiwa kwn huwa wana wka posblity kubwa ya ugonjwa kihas kwamba wanaptsha bla kupma...!!! Ila nahamn nikwa bahadhi ya healt center.nawasilisha
Mkuu,kwa namna moja au nyingine upo sawa.Zipo aina mbili za kufanya mahojiano, ya kwanza ndio hii ambapo mgonjwa unakuwa huru kujieleza kila kitu kwa daktari wako, pale daktari akiona unakwenda nje ya mstari ndio ataanza sasa kukuuliza maswali kwa umakini mkubwa ili kuweza kureach diagnosis.Vile vipimo vya maabara huwa na kazi ndogo na muhimu sana, ni kuweza kuconfirm kile alichodiagnosis daktari. Kiutaalam kabisa, kama hakuna urgent case yoyote ile, haushauriwi kuanza kutumia dawa bila kureach ktk final diagnosis ambayo kwa asilimia kubwa humalizwa na mahojiano kati ya mgonjwa na daktari.[/QUOTE][QUOTEhKI, post: 15387181, member: 164360"]mkuu naomba unikosoe kama nitakosea, mimi ninavyojua hii ni kazi ya daktari, yeye ndo anapashwa kumuuliza mgonjwa hayo maswali na mgonjwa ajibu, yaani mimi niingie tu kwa daktari nianze kujieleza yote hayo bila kuulizwa si nitakuwa KITUKO, daktari ndo aulize maana ndo kasomea na anajua nini anatafuta.
na lazima tukuulize, mara ya mwisho kufanya social work ulitumia ngao ya mbu...??" ole wako kama ulichepuka vichakani teh teh, just kidding mkuu ucjali, we sema tu kinachokusumbua ,ugonjwa wa mtu ni confidential report, it's me and you but none else and that is why we have been there all the time waiting for you to come,huwa ni mtihani sana hasa kwa STDs
It's okay mkuu, we are not expecting the same sequence of conversation through all patients, in case kama hii ya kwako ,a good physician will ask you like this,Umesema una amoeba sio..!!??, naomba kujua, umejuaje kama hii ni amoeba..??Unjua kuna watu wanaenda kwa doctor anamwambia mimi nna malaria sasa kama unaujua ugonjwa umeenda kufanya nini si ununue tu dawa
Au unamwambia doctor nna amoeba hii sio sahihi ni vyema ukamweleza dalili kama ni tumbo au ni kichefuchefu yeye atajua kutokana na dalili hizi upimwe kitu gani lakini sio moja kwa moja kueleza nna amoeba au malaria khaa!
then it's upto you as a physician to dig in and come out with most likely diagnosis with correct explanation.unakuta raia anamwambia daktari nahisi naumwa ugonjwa wa "kisasa".. alafu anaishia hapo.
It's okay mkuu, we are not expecting the same sequence of conversation through all patients, in case kama hii ya kwako ,a good physician will ask you like this,Umesema una amoeba sio..!!??, naomba kujua, umejuaje kama hii ni amoeba..??
mkuu, aliamka vibaya tu huyo siku hiyo ila ukweli ni kwamba lazima ufanye tathmini ya haraka kuhusu mgonjwa uliye naye mbele yako,zingatia sana utamadubni wa mahali husika na elimu ya mgonjwa wako, kutoka hapo unaweza jua jinsi ya kumsikiliza na kumhoji, pole kama ilikuwa kwa ukari.Niliwahi enda nikajieleza hivyo ya amoeba direct dooo daktari alikuwa na mood mbaya sijui siku hiyo akaniambia unaanzaje kusema una amoeba kama unajua hivyo ungenunua dawa tangu hapo nilijifunza
Interview in healthy setting should always be a client centered, doctor should avoid leading the patient,what you must know as a doctor is" a healthy history flows spontaneously from the patient in disorderly manner but the task of organizing the story into a logical sequence is yours, and that is what forming a basis of the medical professional"[/QUOTE]Mkuu,kwa namna moja au nyingine upo sawa.Zipo aina mbili za kufanya mahojiano, ya kwanza ndio hii ambapo mgonjwa unakuwa huru kujieleza kila kitu kwa daktari wako, pale daktari akiona unakwenda nje ya mstari ndio ataanza sasa kukuuliza maswali kwa umakini mkubwa ili kuweza kureach diagnosis.Vile vipimo vya maabara huwa na kazi ndogo na muhimu sana, ni kuweza kuconfirm kile alichodiagnosis daktari. Kiutaalam kabisa, kama hakuna urgent case yoyote ile, haushauriwi kuanza kutumia dawa bila kureach ktk final diagnosis ambayo kwa asilimia kubwa humalizwa na mahojiano kati ya mgonjwa na daktari.
Umeeleza kila kitu mkuuLeo naandika kuhusu jinsi ya kujieleza vizuri kwa daktari. Jinsi mgonjwa anavyojieleza kwa daktari ni muhimu sana, kwa sababu inaathiri moja kwa moja ubora wa tiba atakayopatiwa mgonjwa. Ni muhimu tukafahamu kuwa, maelezo yako kwa daktari yanachangia mpaka asilimia 75 ya daktari kuweza kugundua tatizo linalokukabili! (asilimia 25 iliyobaki ni ya daktari kukufanyia uchunguzi wa mwili kwa mikono yake, na vipimo vya maabara). Hii ina maana ya kwamba, historia anayoipata daktari kutoka kwako, ina mchango mkubwa sana katika kumuelekeza daktari kwenye tatizo sahihi linalokusumbua; ama kumpelekea daktari kukosea kabisa aina ya tatizo ulilonalo, ama hata kushindwa kabisa kufahamu ugonjwa unaokusumbua hasa ni nini. Mambo yafuatayo yatakusaidia kuweza kujieleza vizuri kwa daktari
1.Usimwambie daktari ugonjwa wako( diagnosis), bali mueleze daktari dalili ulizonazo:
Hapa ninawazungumzia wale ambao wanaingia chumba cha daktari na kuanza kujieleza "daktari nina malaria" au "nina typhoid". Hii sio njia sahihi kabisa ya kuanza kujieleza kwa daktari! Kufahamu aina ya ugonjwa unaoumwa (diagnosis) ni kazi ya daktari, unachotakiwa kufanya ni kuelezea dalili zako, kwa mfano "kichwa kinaniuma na ninaharisha tangu juzi". Hii ndiyo namna bora kabisa ya kuanza kujieleza mbele ya daktari! Hakuna kitu ambacho kinamfanya daktari aghafilike kama mgonjwa kuanza kusema diagnosis yake badala ya kuelezea dalili zake.
2.Epuka kutumia maneno ambayo yanaweza kuwa na maana zaidi ya moja kwa watu tofauti
"daktari nina homa tangu juzi" siku zote mgonjwa akianza kujieleza kwa kauli hii kwangu, swali linalofuata ambalo huwa nauliza ni "unamaanisha nini unaposema homa"? Na huwa napata maana tofauti kwa watu tofauti. Wengine husema wanamaanisha mafua na kukohoa, wengine wanamaanisha kuwa joto la mwili liko juu, wengine husema wanamaanisha kuwa wanaharisha, na kadhalika. Hivyo basi, badala ya kuanza kujieleza kuwa una "homa" (ambayo kiukweli,kwa daktari asiekuwa makini, na akachukulia homa kwa maana ya kidaktari, anaweza kukupa ugonjwa ambao wala hauna kabisa), ni vyema ukajieleza kwa kutumia maneno ya moja kwa moja na kwa kutaja dalili zote ulizonazo, moja baada ya nyingine.
3.Usiseme uongo wala kuficha kitu chochote kwa daktari kuhusu afya yako:
Hakuna kosa kubwa (mimi huita suicidal mistake) kwa mgonjwa kufanya, kama kumdanganya kwa makusudi daktari, au kuficha kitu fulani kuhusu afya yake au kuhusu ugonjwa wake. Huna sababu yoyote ya kumdanganya daktari au kumficha kitu daktari kwa sababu zifuatazo;
-Kwanza, kumdanganya daktari kutapelekea daktari kushindwa kubaini tatizo lako, au hata kumpelekea kukosea ugonjwa unaokusumbua; kwa sababu kama tulivyoona awali, daktari anatagemea maelezo yako kwa asilimia 75 kuweza kugundua tatizo lako.
-Pili, hicho unachoogopa kumwambia, kuna uwezekano mkubwa kabisa ya kuwa ameshawahi kukisikia/kukiona na haitakuwa mara ya kwanza yeye kusikia/kuona hicho kitu, hivyo huna sababu ya kuogopa.
-Tatu, nakuhakikishia kuwa kuna uwezekano mkubwa sana (asilimia 99.9) kuwa, daktari atasahau hata sura yako mara baada tu ya wewe kutoka nje ya chumba chake, achilia mbali tatizo lako ulilomwambia!! Kwa mfano, kwa wastani siku ambayo naona wagonjwa naweza kuona wagonjwa zaidi ya 50; na nara zote mwisho wa siku huwa sikumbuki sura za wagonjwa niliowaona, achilia mbali matatizo yao.
4.Unapoenda hospitali, nenda na dawa zako zote unazotumia au uliwahi kutumia kwa tatizo ulilo nalo:
"Nilikuwa natumia vidonge fulani hivi vyeupe vikubwa vya duara" usitegemee kabisa daktari aweze kugundua kuwa ni aina gani ya dawa uliyokuwa unatumia kwa maelezo ya aina hii! Maana, rangi ya dawa haina umuhimu wowote katika kile ambacho kipo ndani ya dawa. Na kimsingi, kuna dawa ambazo zinapatikana katika rangi tofauti kutegemea na kiwanda zilipotengenezwa, lakini zina kitu kile kile ndani yake!!
Hivyo basi, kama tatizo ulilo nalo ni la muda mrefu, na uliwahi kwenda hospitali na ukapewa dawa ni vyema ukaenda na dawa hizo pale unapokwenda tena hospitali kwa tatizo hilo; au angalau ukabeba kikopo ambacho kilikuwa na dawa hizo.
5.Kwa watoto, aende mtu ambae anakaa na mtoto na/au anafahamu vizuri historia ya ugonjwa wa mtoto:
Huwa napata tabu sana pale ninapomuona mtoto anaesumbuliwa na dalili fulani, halafu namuuliza aliemleta, "amekuwa na dalili hizo kwa muda gani" halafu jibu ninalopata linakuwa "sijui". Jibu la aina hii linakuwa halina msaada wowote ule kwa daktari, bali huleta usumbufu usio wa lazima kwa daktari; Hivyo basi ni muhimu aende mtu ambae anafahamu vizuri historia ya tatizo la mtoto.
6.Uliza maswali kuhusu ugonjwa wako, vipimo na matibabu:
Mara nyingi madaktari huwa tunajisahau kuwaelezea wateja wetu kwamba ni nini tumegundua anaumwa, na ni vipimo gani anatakiwa kufanya (na majibu ya vipimo hivyo), na matibabu ni yapi. Hivyo basi, daktari akimaliza kukuhudumia na kukwambia "nenda maabara" kwa mfano, unatakiwa umuulize kwa utaratibu, kuwa je, daktari anadhani una ugonjwa upi? na amekuandikia vipimo gani? Na pia, hata ukirudi kwa daktari na majibu ya vipimo vyako, ni vyema ukamuuliza majibu yanasemaje, na yanamaanisha nini; Vile vile kwa dawa atakazokuandikia. Daktari ambae anajua anachokifanya hatapata shida kabisa kukuelezea yote hayo (labda kama umeuliza kwa ukali au kwa kutumia lugha isiyo ya kistaarabu).