ngondoiwela
Member
- Jan 15, 2014
- 12
- 2
Well and good...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usahihi wa neno (Meningitis) hebu tembelea hapa bonyeza Meningitis - Wikipedia, the free encyclopedia au bonyeza hapa Meningitis - Wikipedia, kamusi elezo huru Mkuu unatumia jina wakati maana ya jina lako hulielewi? Ahhh vipi mkuu?
hiki kisingizio cha wagonjwa kuwa wengi kinatumiwa sana na watumishi wa afya!ingawa ukimuuliza ameona wagonjwa wangapi kwa siku na avarage time ya kumuona mgonjwa mmoja utakuta hakina ukweli ndani yake.
Kwangu mimi ni heri ukatumia muda mwingi kumuona mgonjwa mmoja vizuri na akapona kuliko kulipua na baadae mgonjwa huyo akakurudia akiwa na complications.
Naamini madaktari waliozoea kutumia utaratibu huu mara kwa mara wanapata uzoefu ambao unawafanya kuhudumia wagonjwa kwa haraka na usahihi.pia kwa uzoefu wangu mgonjwa hujenga imani kubwa ya matibabu iwapo atahojiwa kwa jinsi hii kuliko kuulizwa swali moja na kuambiwa akapime.
Mkuu lakini si unajua kuwa kwa Tanzania ratio ya Patients per Dr. ni kubwa sana? Kwa msingi huo ina maana wagonjwa wengi watakuwa wanarudi nyumbani bila kutibiwa!
Mimi nadhani ili ushauri wako uweze kutekelezeka vizuri inabidi pia Serikali ijitahidi kusomesha madaktari wengi zaidi ili kuwe na madaktari wa kutosha katika kila hospitali / kituo cha afya.
Karibu sana mkuu!Meningts nakukubli sana MD ushauri ulio utoa una faida sana. Naomba kuchangia wakat mwngne napo kujieleza sana huwa kuna changia usfanyiwe lab investgation inavyo takiwa kwn huwa wana wka posblity kubwa ya ugonjwa kihas kwamba wanaptsha bla kupma...!!! Ila nahamn nikwa bahadhi ya healt center.nawasilisha
Unjua kuna watu wanaenda kwa doctor anamwambia mimi nna malaria sasa kama unaujua ugonjwa umeenda kufanya nini si ununue tu dawahuwa ni mtihani sana hasa kwa STDs
iko poa sana hiiiLeo naandika kuhusu jinsi ya kujieleza vizuri kwa daktari. Jinsi mgonjwa anavyojieleza kwa daktari ni muhimu sana, kwa sababu inaathiri moja kwa moja ubora wa tiba atakayopatiwa mgonjwa. Ni muhimu tukafahamu kuwa, maelezo yako kwa daktari yanachangia mpaka asilimia 75 ya daktari kuweza kugundua tatizo linalokukabili! (asilimia 25 iliyobaki ni ya daktari kukufanyia uchunguzi wa mwili kwa mikono yake, na vipimo vya maabara). Hii ina maana ya kwamba, historia anayoipata daktari kutoka kwako, ina mchango mkubwa sana katika kumuelekeza daktari kwenye tatizo sahihi linalokusumbua; ama kumpelekea daktari kukosea kabisa aina ya tatizo ulilonalo, ama hata kushindwa kabisa kufahamu ugonjwa unaokusumbua hasa ni nini. Mambo yafuatayo yatakusaidia kuweza kujieleza vizuri kwa daktari
1.Usimwambie daktari ugonjwa wako( diagnosis), bali mueleze daktari dalili ulizonazo:
Hapa ninawazungumzia wale ambao wanaingia chumba cha daktari na kuanza kujieleza "daktari nina malaria" au "nina typhoid". Hii sio njia sahihi kabisa ya kuanza kujieleza kwa daktari! Kufahamu aina ya ugonjwa unaoumwa (diagnosis) ni kazi ya daktari, unachotakiwa kufanya ni kuelezea dalili zako, kwa mfano "kichwa kinaniuma na ninaharisha tangu juzi". Hii ndiyo namna bora kabisa ya kuanza kujieleza mbele ya daktari! Hakuna kitu ambacho kinamfanya daktari aghafilike kama mgonjwa kuanza kusema diagnosis yake badala ya kuelezea dalili zake.
2.Epuka kutumia maneno ambayo yanaweza kuwa na maana zaidi ya moja kwa watu tofauti
"daktari nina homa tangu juzi" siku zote mgonjwa akianza kujieleza kwa kauli hii kwangu, swali linalofuata ambalo huwa nauliza ni "unamaanisha nini unaposema homa"? Na huwa napata maana tofauti kwa watu tofauti. Wengine husema wanamaanisha mafua na kukohoa, wengine wanamaanisha kuwa joto la mwili liko juu, wengine husema wanamaanisha kuwa wanaharisha, na kadhalika. Hivyo basi, badala ya kuanza kujieleza kuwa una "homa" (ambayo kiukweli,kwa daktari asiekuwa makini, na akachukulia homa kwa maana ya kidaktari, anaweza kukupa ugonjwa ambao wala hauna kabisa), ni vyema ukajieleza kwa kutumia maneno ya moja kwa moja na kwa kutaja dalili zote ulizonazo, moja baada ya nyingine.
3.Usiseme uongo wala kuficha kitu chochote kwa daktari kuhusu afya yako:
Hakuna kosa kubwa (mimi huita suicidal mistake) kwa mgonjwa kufanya, kama kumdanganya kwa makusudi daktari, au kuficha kitu fulani kuhusu afya yake au kuhusu ugonjwa wake. Huna sababu yoyote ya kumdanganya daktari au kumficha kitu daktari kwa sababu zifuatazo;
-Kwanza, kumdanganya daktari kutapelekea daktari kushindwa kubaini tatizo lako, au hata kumpelekea kukosea ugonjwa unaokusumbua; kwa sababu kama tulivyoona awali, daktari anatagemea maelezo yako kwa asilimia 75 kuweza kugundua tatizo lako.
-Pili, hicho unachoogopa kumwambia, kuna uwezekano mkubwa kabisa ya kuwa ameshawahi kukisikia/kukiona na haitakuwa mara ya kwanza yeye kusikia/kuona hicho kitu, hivyo huna sababu ya kuogopa.
-Tatu, nakuhakikishia kuwa kuna uwezekano mkubwa sana (asilimia 99.9) kuwa, daktari atasahau hata sura yako mara baada tu ya wewe kutoka nje ya chumba chake, achilia mbali tatizo lako ulilomwambia!! Kwa mfano, kwa wastani siku ambayo naona wagonjwa naweza kuona wagonjwa zaidi ya 50; na nara zote mwisho wa siku huwa sikumbuki sura za wagonjwa niliowaona, achilia mbali matatizo yao.
4.Unapoenda hospitali, nenda na dawa zako zote unazotumia au uliwahi kutumia kwa tatizo ulilo nalo:
"Nilikuwa natumia vidonge fulani hivi vyeupe vikubwa vya duara" usitegemee kabisa daktari aweze kugundua kuwa ni aina gani ya dawa uliyokuwa unatumia kwa maelezo ya aina hii! Maana, rangi ya dawa haina umuhimu wowote katika kile ambacho kipo ndani ya dawa. Na kimsingi, kuna dawa ambazo zinapatikana katika rangi tofauti kutegemea na kiwanda zilipotengenezwa, lakini zina kitu kile kile ndani yake!!
Hivyo basi, kama tatizo ulilo nalo ni la muda mrefu, na uliwahi kwenda hospitali na ukapewa dawa ni vyema ukaenda na dawa hizo pale unapokwenda tena hospitali kwa tatizo hilo; au angalau ukabeba kikopo ambacho kilikuwa na dawa hizo.
5.Kwa watoto, aende mtu ambae anakaa na mtoto na/au anafahamu vizuri historia ya ugonjwa wa mtoto:
Huwa napata tabu sana pale ninapomuona mtoto anaesumbuliwa na dalili fulani, halafu namuuliza aliemleta, "amekuwa na dalili hizo kwa muda gani" halafu jibu ninalopata linakuwa "sijui". Jibu la aina hii linakuwa halina msaada wowote ule kwa daktari, bali huleta usumbufu usio wa lazima kwa daktari; Hivyo basi ni muhimu aende mtu ambae anafahamu vizuri historia ya tatizo la mtoto.
6.Uliza maswali kuhusu ugonjwa wako, vipimo na matibabu:
Mara nyingi madaktari huwa tunajisahau kuwaelezea wateja wetu kwamba ni nini tumegundua anaumwa, na ni vipimo gani anatakiwa kufanya (na majibu ya vipimo hivyo), na matibabu ni yapi. Hivyo basi, daktari akimaliza kukuhudumia na kukwambia "nenda maabara" kwa mfano, unatakiwa umuulize kwa utaratibu, kuwa je, daktari anadhani una ugonjwa upi? na amekuandikia vipimo gani? Na pia, hata ukirudi kwa daktari na majibu ya vipimo vyako, ni vyema ukamuuliza majibu yanasemaje, na yanamaanisha nini; Vile vile kwa dawa atakazokuandikia. Daktari ambae anajua anachokifanya hatapata shida kabisa kukuelezea yote hayo (labda kama umeuliza kwa ukali au kwa kutumia lugha isiyo ya kistaarabu).
umewahi kujieleza kwa madaktari wangapi? Labda tuanzie hapo...Mimi naweza sana kujieleza vizuri kiasi kwa Dr tatizo sijawahi Labda pata daktari mzuri wakunihudumia matokeo Yake hua naishia kutohudumiwa vyema.
mkuu naomba unikosoe kama nitakosea, mimi ninavyojua hii ni kazi ya daktari, yeye ndo anapashwa kumuuliza mgonjwa hayo maswali na mgonjwa ajibu, yaani mimi niingie tu kwa daktari nianze kujieleza yote hayo bila kuulizwa si nitakuwa KITUKO, daktari ndo aulize maana ndo kasomea na anajua nini anatafuta.ni kweli mkuu!ni muhimu kufanya jambo au mambo kwa manufaa ya watu wa kawaida.