Elizabeth Michael (Lulu) afunguka haya juu ya kesi yake

Elizabeth Michael (Lulu) afunguka haya juu ya kesi yake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Ikiwa imebakia siku moja kuanza kusikilizwa tena kwa kesi ya mauaji ambayo inamkabili, msanii Elizabeth Michael (Lulu) amesema yupo tayari kukabiliana na kesi hiyo, ambayo alijua ipo siku itarudi tena.

20589849_160943114475922_2222556347734425600_n.jpg

Lulu ameyasema hayo leo alipokuwa akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kuwa alikuwa na taarifa ya kesi hiyo kabla watu hawajaipata kwenye mitandao, na utaratibu wa kisheria ulifuatwa.

“Unajua watu hawajui sheria, kesi haikuwahi kuisha ni pocedure ya kawaida ya mahakama imefuatwa na ni muda wake umefika sasa , siyo kama imeibuka tu, na kwasababu mimi ndiye muhusika nimepata taarifa kwa njia ya kisheria siyo kama nyie kwenye mitandao, na pengine niliipata kabla yenu”, amesema Lulu.

Lulu ameendelea kusema kwamba kuwepo kwa kesi hiyo kunamuathiri kwa kiasi kikubwa kwenye kazi zake na maisha yake kiujumla. Kesi inayomkabili muigizaji huyo wa bongo movie inatarajia kusikilizwa tena kesho Oktoba 19, 2017 baada ya kuwa nje kwa dhamana kwa muda mrefu.

Elizabeth Michael (Lulu) anakabiliwa na kesi ya kusababisha kifo bila kukusudia cha aliyewahi kuwa muigizaji wa filamu nchini, Steven Kanumba, mnamo April 7, 2012 .

EATV
 
Kanumba alikuwa hatari kwa jamii, maana kaanza kukitafuna kilulu tangu kikiwa kitoto. Who knows, labda angekuwepo mpaka leo angemuona Lulu mzee angekuwa anatafuna vitoto vingine visivyokuwa na matiti. Yule jamaa alikuwa Paedophile.
 
Kibubu chake kinamfanya atuone hatujui sheria!!?

Dharau mbaya, atapumuliwa shingoni na kila kada, wanasiasa, mipolisi, makarani, mahakimu, mabwanajela n.k n.k.

Mungu amrehemu.
 
Na wala hakumkuta virgin dogo kaanza michezo kabla ya kanumba na ndo maana aliacha shule
 
Kibubu chake kinamfanya atuone hatujui sheria!!?

Dharau mbaya, atapumuliwa shingoni na kila kada, wanasiasa, mipolisi, makarani, mahakimu, mabwanajela n.k n.k.

Mungu amrehemu.
Hivi huyu binti hana hata ndugu wa kumshaur? cuz huwa anaongea lolote linalomjia kichwani bila hata kufikir!
 
Back
Top Bottom