Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Katika hali inayoonesha mambo kuzidi kumgeukia Rais Zelensky wa Ukraine, tajiri mkubwa wa mawasiliano na aliyekuwa mfadhili mkubwa wa Ukraine Ellon Musk amemdhihaki kiongozi huyo kwa kumuonesha kama mtu ombaomba aliyepitiliza viwango.
Katika picha aliyoitengeneza na kuiweka kwenye akaunti yake, Ellon Musk amemchora Zelensky akiwa darasani na mwenye wasiwasi wa kama mwanafunzi anayetaka kuuliza swali.
Pembeni mwa picha hiyo Musk akamuuliza Zelensky imekuwaje zimepita dakika 5 na hajaomba dola bilioni.
Picha hiyo inayoitwa meme imewakasirisha sana wabunge wa Ukraine ambao wameanza kumjibu Ellon Musk na wao kujaribu kuchora vikatuni vyake.
Mkasa huu unamkuta Zelensky ikiwa ni siku chache tu bunge la Marekani kusitisha misaada zaidi kwa Ukraine maamuzi ambayo yamesababisha mvurugano kwenye bunge hilo mpaka kuondolewa kwa Spika wake Kevin McCarthy kwa kura maamuzi ambayo hayajawahi kufanyika katika historia ya Marekani.
Hilo pia linakuja wakati Uiengereza imetangaza haina tena silaha za kuipatia Ukraine na kama yuko mwengine anayeweza kuisaidia achukue nafasi yake.
Sambamba na hayo kuna vuguvugu kubwa Poland aliyekuwa rafiki mkubwa na muungaji mkono wa vita ambapo ajenda za uhusiano na Ukraine zikishika nguvu kuelekea uchaguzi wa Oktoba 15 ijayo.
Vyama vinavyopinga vita na kuisaidia Ukraine vimeonekana kupata uungwaji mkono mkubwa miongoni mwa wapiga kura,

Ukraine Hits Back at Elon Musk Over Meme Taunting Zelensky