Hii ni sign of power kiroho, na huwa inatumiwa na watu wanapoongea mambo yanayomake sense tu like unapoonesha msisitizo wa jambo, kwahiyo unadominate mazungumzo na kufanya watu wakuelewe vizuri.
Kwahiyo kama utaongea mambo ya kipuuzi watu watauzingatia upuuzi wako na ukimaliza tu utakuta wanakukosoa Kila pahala na kama utaongea mambo yanayomake sense watu watakuzungumzia kwa uzuri Kila pahala (haishauriwi kutimiwa kama unajua unaongea pumba😅)
Infact, ziko alama nyingi sana za mikono ambazo hutumika na watu wengi mashuhuri na Kila moja huwa inatumika kwenye eneo husika, miongoni mwa watu ambao wanazingatia sana jambo hili ni Elon.
Na nnasema anazingatia kwasababu yeye si tu akiwa anaongea bali hata akiwa ametulia anasikiliza au anatafakari jambo huwa anazingatia sana kufunga mikono yake katika mtindo ambao unamaanisha hali fulani kiroho (moja ya alama ya mikono maarufu ni kiganja kushika shavu au nusu ya kidevu huku shingo yako ikibend kidogo kufuata kiganja cha mkono wako, hii ndio huitwa kushika tama).
Na hiyo alama unayoiona hapo watu wengi wa alpha huwa wanaipenda sana kwa maana kiimani huwa inawafanya wawe na confidence na kudominate mazungumzo kitu kinachowafanya wawasilishe jambo lao kwa namna waliyokusudia kwa urahisi.
Kuna nguvu ya pekee sana katika viganja vya mikono yako, lakini pia huwa kuna connection fichi kati ya ubongo wako na viganja au mikono yako na ndio maana ni rahisi sana kumkuta mtu anatafakari jambo kwa kuongea mwenyewe huku akiwa anachezesha na mikono huku na kule pasipo yeye mwenyewe kujijua.
Au mtu anapotoa speech mbele ya watu wengi kama atakua anaogopa basi mikono yake itakupa ishara hiyo kwa namna atakavyoiweka au atakavyokua anaichezea na kama anajiamini pia utajua kwa kutumia mikono pekee(na hii sio kama mtu anapanga kwamba sijiamini wacha niweke hivi mikono au niichezeshe hivi viganja vyangu ila ni hali tu inatokea automatic kutokana na ile connection fichi iliyopo).
Kwahiyo mleta mada jitahidi ujifunze hizo alama zitakusaidia na wala hazina connection yoyote na hao freemason mnaowasemaga, isipokua labda watu wa freemason huwa wanazitumia hizo alama kwakua wanajua na kuamini kwenye nguvu iliyomo ndani yake.