Elon Musk afanikiwa kuinunua Twitter

Elon Musk afanikiwa kuinunua Twitter

KISIWAGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
8,022
Reaction score
16,563
Baada ya figisu figisu za muda mfupi kumzuia mkurugenzi mkuu wa kampuni ya space X na mtu tajiri zaidi duniani kwa paper assets bwana Elon Musk hatimaye amefanikiwa kuununua mtandao wa twitter

Mpaka sasa makundi ya haki za binadamu hayaelewi twitter chini ya mmiliki huyo mpya kama itaweza kupambana na matamshi ya chuki

Pia mpaka sasa haijawa wazi juu ya mamillion ya accounts za twitter ambazo zilipigwa permanent ban ikiwemo ya mrepublican Donald Trump kama zitaondolewa zuio

Tajiri Elon Musk ametoa ahadi ya kuondoa censorship na kuweka wazi source code za mtandao wa twitter open source ili mtu yeyote aweze kuona namna mtandao huo unaendeshwa

Nadhani hapa bwana Maxence Melo utakuwa umepata cha kujifunza
 
Mtakumbuka kwamba Donald Trump alifungiwa account yake ya Twitter kutokana na kauli zake kwamba uchaguzi wa Marekani aliibiwa na kwamba yeye ndie alikuwa raisi halali wa Marekani.

Sasa Twitter imenunuliwa na Bilionea tajiri namba 1duniani, ambae ni mwanachama ngangari wa Republicans, na rafiki yake Trump.

Dunia inajiandaa kuona Donald Trump akirudi Twitter kwa nguvu!
 
Mtakumbuka kwamba Donald Trump alifungiwa account yake ya Twitter kutokana na kauli zake kwamba uchaguzi wa Marekani aliibiwa na kwamba yeye ndie alikuwa raisi halali wa Marekani.

Sasa Twitter imenunuliwa kutoka kampuni inayomilik Face Book ya Mark Zuckerberg na Bilionea tajiri namba 1duniani, ambae ni mwanachama ngangari wa Republicans, na rafiki yake Trump.

Dunia inajiandaa kuona Donald Trump akirudi Twitter kwa nguvu!
Tokea Lin Zuckerberg alikua mmiliki wa Twitter, na lini Elon musk Ali declare ni mwanachama wa republican
 
Kuna uhusiano gani wa huyo tajiri kununuwa Twitter na kumrudisha Trump?

Hivi hujui Mrepublican anaweza kuwapigia kura Democrats?
1651058488898.png
 
Share za tesla zilidrop baada ya kutangazwa kuwa anainunua
Zitapanda sana mkuu sababu ya kushuka ni hizi fujo fujo za Ukraine, lockdown za huko China na wasiwasi wa FED kuongeza interest rates ili kupambana na mfumuko wa bei ambao kwa sasa umekaribia kufika mawinguni
 
Sababu waliyotoa ni kwamba kulikuwa kuna hofu jamaa atachukua mpunga kutoka kwenye share zake na kwenda kununulia twitter. Pia wanadai investors wanasema siku hizi anatumia muda mwingi space x sasa kaongeza tena na twitter.
 
Ni kweli lakini sasa Elon baada ya kufanikiwa kuimiliki Twitter kwa asilimia 100 ataweza kuitumia kama chombo chake cha kufanyia manipulation yaani ni sawasawa na ONTARIO angekuwa anaimiliki JF kipindi kile cha kudownload pesa
 
Yah mzee wa dodge coin...
 
Back
Top Bottom