Elon Musk Akana Tuhuma za Kutoka Kimapenzi na Nicole Mke wa Mwanzilishi Wa Google

Nicolaus Trac

Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
5
Reaction score
3
Bilionea namba moja duniani, Elon Musk amekana uhusiano wowote na Nicole Shanahan, ambaye ni mke wa mwanzilishi wa Google, Sergey Brin.

Kauli ya mmiliki huyo wa kampuni ya magari ya uneme ya Tesla, imekuja baada ya ripoti katika Jarida la Wall Street kieleza kwamba urafiki wa Musk na Brin ulikufa kutokana na madai ya Musk kuwa na uhusiano na mke wa Brin.

Kupitia mtandao wa Twitter, Musk alitoa maoni yake katika jarida la Wall Street, akisema ripoti hiyo ilikuwa "Upuuzi mtupu", kwamba urafiki wake na Brin haujafa, na kwamba "Walikuwa kwenye hafla pamoja jana usiku."

Gazeti la Wall Street Journal lilibaini kuwa liliegemea ripoti yake kwenye vyanzo vya habari, likisema kwamba mwaka jana Musk alikuwa akichumbiana na Shanahan.

Hii ilisababisha Brin kuanzisha kesi ya talaka mapema mwaka huu na kufuta urafiki wa muda mrefu kati ya wakuu hao wawili wa teknolojia, jarida la Wall Street lilisema.

Lakini Musk aliandika ujumbe kwenye Twitter, "Kwa miaka mitatu, nimemuona Nicole mara mbili tu, na katika matukio hayo mawili kumekuwa na watu wengi karibu. Hakuna kitu cha kimapenzi."
 
Huyu mjomba baada ya miaka kadhaa kutakuwa na msululu wa kupima DNA kuthibitisha kama mwanae yupi na anaesingiziwa ni yupi, maana wamarekani kwenye pesa ni makauzu kupita maelezo.
 
Bilionea namba moja duniani, Elon Musk amekana uhusiano wowote na Nicole Shanahan, ambaye ni mke wa mwanzilishi wa Google, Sergey Brin.

Kauli ya mmiliki huyo wa kampuni ya magari ya uneme ya Tesla, imekuja baada ya ripoti katika Jarida la Wall Street kieleza kwamba urafiki wa Musk na Brin ulikufa kutokana na madai ya Musk kuwa na uhusiano na mke wa Brin.

Kupitia mtandao wa Twitter, Musk alitoa maoni yake katika jarida la Wall Street, akisema ripoti hiyo ilikuwa "Upuuzi mtupu", kwamba urafiki wake na Brin haujafa, na kwamba "Walikuwa kwenye hafla pamoja jana usiku."

Gazeti la Wall Street Journal lilibaini kuwa liliegemea ripoti yake kwenye vyanzo vya habari, likisema kwamba mwaka jana Musk alikuwa akichumbiana na Shanahan.

Hii ilisababisha Brin kuanzisha kesi ya talaka mapema mwaka huu na kufuta urafiki wa muda mrefu kati ya wakuu hao wawili wa teknolojia, jarida la Wall Street lilisema.

Lakini Musk aliandika ujumbe kwenye Twitter, "Kwa miaka mitatu, nimemuona Nicole mara mbili tu, na katika matukio hayo mawili kumekuwa na watu wengi karibu. Hakuna kitu cha kimapenzi."

Kuna kitu hakipo sawa
 
Back
Top Bottom