Elon Musk ana taaluma gani hadi aaminiwe kusimamia Ukaguzi wa Fedha za Misaada ya Marekani Duniani kote?

Elon Musk ana taaluma gani hadi aaminiwe kusimamia Ukaguzi wa Fedha za Misaada ya Marekani Duniani kote?

Ni Mwalimu Mwandamizi wa Diploma Korogwe TC
Huyo ndio anatakiwa asimamie na kuidhinisha na kuaandaa mipango ya research ili chanjo ya malaria na ukimwi ipatikane. ahahahahahahaaaaaa. Bora ata Ummy alikuwa anaelewa kidogo kuliko huyu wa sasa ataweza na hizi taarifa za magonjwa ya mlipuko ya kila mara????
 
Ila nahisi wafanyakazi wao wenyewe USAID ni wezi wamekuwa wakishirikiana na viongozi wa Africa kufanya wizi wa walioa Kodi za USA.
Wizi wa fedha huwa ni mnyororo

Hakuna fedha inaibwa na mtu mmoja

Ndiyo maana fedha zilipoibwa miaka ile pale Benki Kuu, jamaa wakachoma moto

Kwahiyo hakuna wa kumuuliza, na case inakuwa imeishia hapo 🙌
 
Je, Elon Musk ni mtaalam wa maswala ya Fedha kama Prof Alhaj Assad wa Tanzania?

Ni hilo tu 🐼
Sifa ya kwanza hana njaa ni mtu aliyefanikiwa sana, akili hupimwa kwa mafanikio ya mtu na si vyeti vyake, kwa mfano ukikutana na Prof afu maskini naye ni mtu hafai kwa uongozi wa umma sababu elimu yake haijamsaidia chochote.

Sisi waafrica tunafeli sababu viongozi wetu 99% ni njaa kali - anapoingia madarakani tu anaanza kujenga jumba hekalu , kununua gari la kifahari - akistaafu anajengewa nyingine tena na serikali...
Je ulishawahi kusikia haya nchi za wenzetu?

Ndiyo maana wazungu wanatuacha mbali saana. Kiongozi mwenye njaa lazima awe kidokozi wa hela za umma.
 
Siyo lazima,jinsi ya kuziona fursa na kuzitumia,mfano ukiunda teknolojia mpya na ukawa unajua jinsi ya kuitumia ikunufaishe zaidi sioni kama ni wizi,hiyo ni kufuta jasho lako,hata hivyo itakuwa jambo la muda na kadiri uelewa unaongezeka mianya hiyo inapungua na maboresho yanafanya kuondoa mapyngufu.
Hio technology mpya unaundaje? Elon anaanza mambo ya tesla tayari ana ukwasi wa maana, kutoka 0 kuwa milionea ama Bilionea hapo ndio watu wanapoiba ila kutoka Bilioni 5 kwenda 10 ama 100 ndio hapo unapopewa stori jinsi gani fulani ni genius.
 
Mkuu kumbe USAID walikuwa wanatoa na msosi kwa wagonjwa wa TZ, ila viongozi wa ccm wanazila ?.
Na.nauli mkuu ,vifurushi hivyo viwili alikuwa anachukua nani ...furushi lilikuwa na bando TATU(dawa,chakula na nauli)
 
BIla kuwa na kichwa kinachochaji vyema ubillionia utausikilizia kwenye bomba.Bahati iliyoje kaaminiwa na bilionea mwenzake akihitaji umahiri wake kwenye technology umsaidie kuwa nyoosha wavivu,warasimu,omba omba na wala kwa kamba.
Bila utapeli na ulaghai huwezi kuwa bilionea dunia hii ninavyoona mimi.
 
Unataka kutuambia Mabilionea wote wa Tanzania ni wezi na wakwepa kodi ?
Tanzania tumewahi kuwa na Mabilionea wawili tu, Mohammed Dewji na Rostam Aziz, sasa hivi tuna Bilionea mmoja kama data hazijabadilika karibuni. Na wote hawakwepi hizo tuhuma.
 
Back
Top Bottom