Marekani, baada ya kuinunua Twitter kaanza kuruhusu kuwe na neutral ground kinyume na democrats wanavyotaka mawazo yao peke yao yasikike, hiki chama huwa kinacheza rafu sana, huanza kwa makesi kibao ya kubambikiwa, wakishindwa wanakuchomoa Kama walivyotaka kumfanyia mtu maarufu mwaka huu. Elon kapata sapoti kubwa sana ya Republicans ya Trump na Democrats waliohamia Reublican lakini katengeneza uadui mkubwa kwa democrats
Brazil kaanzisha ligi nyingine dhidi ya Serikali, kiranja akiwa Alexanda Moraes, Support ya wabrazil ni kubwa kwa Elon Musk lakini hao jamaa anaowachokonoa they are dangerous.
Hapo kabla mtandao wa Twitter ulikuwa anti israel, post za Israel zilikuwa zinabanwa sana (censored), kwa hali ya sasa mambo yamebadilka, Post za Israel nazo zinapewa uwanja, Support kwa wanaosapoti Israel imekuwa kubwa lakini wafuasi wa Hamas, Hezbollah, n.k. wanamuona kama adui.
Hapo kabla watu wanao kosoa sana uislamu walikuwa wanabanwa kwa kigezo cha kuwa anti islam, kwa hali ya sasa uwanja upo huru, Kapata sapoti kubwa ya watu wanaopenda uwanja huru kwenye ukosoaji wa dini lakini katengeneza uadui na radical muslims.