Elon Musk angekuwa China asingeendeleza hivi vituko vyake yeye na Trump

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
2,748
Reaction score
5,112
Huyu tajiri Elon na tajiri mwenzake Trump waliovamia siasa na kuziendesha vile watakavyo wao sioni kama watakuwa na mwisho bora.

Kwa siasa za China Trump asingefika hata hapa alipofika tena huyu chawa wake Elon muda huu nina uhahika angekuwa Jack Ma wakimarekani.

Nakumbuka Jack Ma naye alianza tabia fulani za matajiri wanaovamia siasa za nchi sijui wakomunisti wale wa Beijing walimfanya nini mpaka leo amekuwa pole kweli.

Nachokumbuka kwa udogo Jack Ma aliwaponda viongozi wa serikali ya Beijing kwenye summit moja iliyofanyika China alipopewa nafasi ya kuzungumza aliwaponda Havana wa Bank ya China,naibu waziri wa fedha alikuwa mule na viongozi wengi wa serikali walikuwa mule hili lilikuwa kosa kubwa sana Jack Ma alifanya maybe fedha na umaarufu ulimchanganya na kuhisi China ni Amerika kilichofuatia sasa ilikuwa ni habari isiyovutia kwa Jack Ma na kwa baadhi ya makampuni yake hasa Ant group.

Sasa hii room anayopata Trump na mwenzake Musk kuvamia siasa na kuleta mambo yao jinsi wanavyo jisikia wao kwa China Elon angekutana na hatua ya hatari sana kutoka katika serikali.

Elon Musk ni rahisi sana yeye kuwaponda Venezuela mara Brazil mara Afrika kusini mara Ulaya na kuhamasisha juki,mapinduzi na ubaguzi lakini kwa China hajawahi kuthubutu kufanya maybe anajua reaction ya wakomunisti wa pale Beijing hawana muda wa kucheka na mjinga tofauti na hao wengine anao wachezea kama marekani.
 
Labda ndio maana Xi Jinping alimpukutisha sana Jack Ma alipojaribu kuzivamia siasa za China!
Bund Summit 2020 ilileta kiza zaa zaa Jack ma aliwanyoosha kweli viongozi wa China hasa wizara ya fedha wiki kama mbili baadae wakaona huyu sasa anatupanda kichwani wakaanza na makampuni yake ya Ant group haaah ili wakomunisti bwana wana vituko

Ila kuna namna Jack Ma alijisahau kabisa kuwa ile ilikuwa China utajiri na umaarufu vilianza kumuendesha kuna namna uende akaona anaweza kuamuru chochote kitekelezwe kwa manufaa yake.

Ant group ilikuwa inakuja kuwa mnufaika mkubwa kama Jack Ma angekuwa na influence kubwa kwenye siasa za China ubaya alitulizwa
 
Umesema vyema China haiendeshwi na matajiri kama Marekani

Alianza na huu ujinga


Akaja na kauli zake za kipumbavu za kuukosoa mfumo wa kiuchumi na biashara wa China uliomfanya awe bilionea Xi akam-downgrade

Political ambition ndio imemsababishia yote hayo
 
Chinese are expected to be loyal to China, the state that nurtured their success. Ma was observed transferring his loyalty to a predatory state
 
Wasiporudisha mashirika ya misaada na utu ifikapo mwezi March basi wasijiingize kwenye siasa zetu maana si washirika tena wa maendeleo.
 
Watu wanafanya kazi zao, wewe unasema wamevamia mara nini. Unajielewa kweli?
Hakuna kipya anachokifanya Trump hata umuine kuwa amevamia. Kila anachokifanya aliahidi kukifanya na aliwaweka wazi wamarekani kabla na wakati wa kampeni kuwa atafanya.
 
Hata hapa vituko vilikuwa design hii hii hebu kumbuka kauli za akina 👇 baada ya teuzi
  1. Bashiru
  2. Palamagamba
  3. Polepole
  4. Hapi
 
Ile ni Marekani siyo China, mambo ya angekuwa China haiewezekani.
 
China na Marekani ni dunia mbili tofauti
 
Unafananisha Ubepari vs Ukomunisti. The latter ukizingua ni nyepes mno mfumo wa kisiasa kukunyoosha
 
umeshasema china.hawapond na yeye sio mjinga. anaponda mahali tehe tehe ambako hana maslah napo.
 
Wasiporudisha mashirika ya misaada na utu ifikapo mwezi March basi wasijiingize kwenye siasa zetu maana si washirika tena wa maendeleo.
Si tumesha kubaliana kwamba tuachane na misaada kwani ndio inaturudisha kwenye utumwa hivyo tujitegemee ili tuwe huru na mtu asitulazimishe na mambo ya ushoga au nyie mnatakaje.

Kwani hao wanaotusaidia wenyewe wamesaidiwa na nani na sisi lini tutakuja kuwasaidia wengine..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…