mbali na midoli, mimi nawaza kwenye kasi ya Internet.
watakapoongeza output bandwidth ya Internet.
Nafikiri chapa ya mpinga kristo itakuwa ni namba ya NIDA tu πππ
hata kununua nyanya lazima uweke finger print hapo ndio upewe nyanya.
Pesa itakua ni namba tu, hakuna kuzibeba physically
Pesa ishaanza kuhamia digital muda mrefu tu mkuu, na inasaidia kupunguza root of infection.
AI itasaidia kwenye mambo mengi endapo na sisi tutaweka regulation zetu,we fikilia kama AI inaweza kukuchekesha kwa sura na sauti ile ile ya joti tunategemea nini, AI ikitumika vibaya inakua ni saa na wizi kwenye nyanja tofauti tofauti kama vile sanaa n.k
Mfano kwenye Animation zile watu wa sauti huchukuliwa ikiwa wengine ni wasanii wakubwa tu, na hawawezi kuruhusu AI zigenerate sauti ikiwa wasanii hao wapo labda tu wafanye makubaliano, kwasabu inaweza fanya vitu ambavyo mmiliki wa sauti hakuvitaka.
AI inakua so powerful na sheria zinahitajika sana katika AI, kikubwa ni kutokubali AI iruhusiwe kuwa na self decision.
AI Artificial intelligence ktk huduma za afya
AI au akili bandia imekuja kuleta mtizamo mpya katika karne hii tuliyopo sasa kutokana ana mapokeo tofauti kulingana na jinsi teknolojia inavyozidi kukuwa.
Wataalamu wa kompyuta waliweza kutumia AI kama sehemu mojawapo ya kuzifanya machine ziwe na uwezo wakurespond kama binadamu kulingana na weakness kubwa aliyonayo binadamu ya kutumia hisia na akili japo ndio ubinadamu wenyewe, japo kuna muda binadamu anatimilisha agano ya kuwa hayuko perfect, hasa muda anao changanya hisia katika mambo ambayo yangehitaji akili na sio hisia na kwenye mambo ambayo yanaweza hitaji hisia kuliko akili.
Akili bandia (AI) Imejikita katika akili kwasababu jinsi inavyo interact na binadamu ni kwa namna ambayo imeundwa kufanya hivyo kwa kutumia programming languages mbali mbali na ikumbukwe computer ina YES/NO 0/1
Lakini hapa tutajikita zaidi katika afya hususani sehemu zile ambazo kwa dunia ya sasa tutahitaji kutumia, mfano Hospitali, Zahanati, Famasi na katika Vifaa Tiba.
Baadhi ya teknolojia ambazo zilikuwa zikitumika na baadhi mpaka leo hazijatumika katika baadhi ya inchi zinazoendelea ni Vital Bracelet Meter ambazo ni bracelet zinazotumika kumonitor vital situation ya mgonjwa na kureport kama anahitaji response from Nurses or Doctors from department, lakini tunapokuja katika AI suala la hisia linakuja kuingia na ndipo tutaona faida na pia hasara zake katika hali halisi inayoweza kutokea katika huduma za afya.
Faida za AI katika upasuaji
Tunaweza kuona faida nyingi za Ai katika upasuaji wa binadamu mfano zipo robots zilizotengenezwa kufanya au kusaidia katika operation surgery tofauti tofauti zinazo hitaji Laparatomy au Laparascopy na surgery nyingine kadha wa kadha ambazo zimekishafanyika kwa uwezo wa AI japo robots zikiwa sio final katika ufanyaji a maamuzi, lakini katika dunia ya sasa tunakoelekea na kujikita Zaidi ni kuweza kuzipa akili bandia uwezo wa kufanya maamuzi kati ya what is right and wrong.
Faida za AI katika Data Analysis
Katika data analysis AI inaweza tumika kufanya analysis ya data za magonjwa mbalimbali yanayokuwa diagonised katika instituitional level, regional level na mpaka national level at real time tofauti na manual way ambazo zimekuwa zikitumika hivi sasa.
Matumizi ya AI katika kurank wagonjwa wanaohitaji huduma.
Hii inaweza kuonekana sehemu nyingi katika utoaji wa huduma za afya mfano kwa wagonjwa ambao wanakuwa wamelazwa endapo itatumika AI kufanya vital surveillance kwa wagonjwa endapo wagonjwa Zaidi ya mmoja watakuwa katika hali mbaya AI kwasabu inatumia akili inaweza fanya alert kwa mgonja ambae hana shida sana kuliko mengine na kurank ndivyo sivyo.
Matumizi ya Camera katika kudetect criminals.
Katika instituition mbalimbali ambazo tunaweza kuona uhitaji wa AI CCTV system ambazo zitakua na uwezo pia wakudetect criminals na kutoa feed kwa response agencies kama vile police n.k, itakuwaje kama AI imefanya wrong calculations na kufanya body foresic ambayo ni totally wrong ?
Hii itamzuia mgonjwa au mteja kupata huduma stahiki au kupatiwa huduma huku akiwa chini ya ulinzi, na inakuaje kwa mgonjwa ambae ni mahututi hata hawezi kuongea au kujieleza ya kuwa sio mwizi ?