100 others
JF-Expert Member
- Aug 5, 2017
- 4,766
- 16,191
Ni habari ambayo imeacha watu vinywa wazi baada ya CEO wa Tesla na Space X Elon Musk kupendekeza kuisaidia wikipedia msaada wa dola bilioni moja kwa masharti kama itaweza kubadili jina kutoka wikipedia kuwa 'Dickipedia', 😳 Elon Musk amesisitiza ametoa kipindi chini ya mwaka mmoja wajitafakari.
Hata hivyo inadaiwa si mara ya kwanza Musk kutoleana mbovu na wikipedia. Inadaiwa moja ya waanzilishi wa wikipedia Jimmy Wales alimkosoa Elon Musk kwa kuzuia uhuru wa kujieleza mtandaoni baada ya kukubali matakwa ya serikali ya Turkey kuzuia baadhi ya Tweets katika nchi ya Turkey wakati wa uchaguzi May 2023.
Wikipedia ambayo inaendeshwa na wikimedia, shirika linalojiendesha pasipo kutengeneza faida(non profit organization) inaweza kufanya mapinduzi makubwa katika encyclopedia ya mtandaoni endapo tu itapata kiasi hiko.
Watu wamekuwa na maoni tofauti wengine wakimponda Musk kuwanyanyasa wenzie kwa kwa kutumia utajiri alionao. Wengine wakiisisitiza wikipedia ikatae msaada huo.