vifaa na Installation ni milioni 1.
kifurushi kinadumu kwa mwezi, nadani anapanga bei kwa kuangalia uchumi wa nchi, Marekani ni 230,000/= , Nigeria ni 98,000, Hapa Kwetu si ajabu ikawa 70,000 kwa mwezi.
Ni internet ya kisasa, Speed yake ni kubwa sana, unaweza kushusha file la gb 1 speed ikiwa chini utatumia sekunde 20 tu, ni kugusa tu hakuna kusubiri, kucheki video ama video call hakuna mambo ya kuganda.
Haina kikomo, ukitumia hata gb 20 kwa siku ni wewe.
Inaweza kupatikana mpaka mbugani, milimani, kwenye makorongo na sehemu remote ambazo mitandao ya simu haijaweza kufikia, Ni kama vile dstv.
Kwa ninachokiona Elon Musk akiileta hii internet akasomba wateja wengi wale wenye matumizi makubwa hasa wale wanaotumia vifurushi vya laki 1 kila mwezi kwajili ya ofisi zao.
Kwa kuwa internet ni ya Satelite hapa itaweza kufika hadi maporini na vijijini ambako maeneo hayo mengi internet huwa ni changamoto, hii itakuwa changamoto kwa mitandao ya simu hasa katika miji inayokuwa wakitaka kuweka minara watakuta tayari watu wameshazoea starlink.
HITIMISHO:
Vita inayopiganwa kwa sasa, mosi ni bwana Elon kuingilia mkate umoja wa mitandao ya simu, pili ni ugumu wa kuibana huduma hii kama ilivyo kwa mitandao ya simu.
Kwa hali hii nadhani naanza kuelewa kwanini vibali vinacheleweshwa na huenda tukaja sikia hapo mbele kisingizio chochote cha kuifyekelea mbali, ujio wake unaweza kupora wateja wengi wenye matumizi makubwa, hii ni hatari kwa makampuni ya simu na kama mjuavyo kuna watu wana hisa zao huko.
huyu Elon Musk ni mpiganaji wa haki za uhuru na hata hii internet kaileta kwa mkakati wa kupigania zaidi uhuru wa mtandaoni kuzidi faida, Ni hatari hasa ukizingatia hio internet anaisimamia yeye na anaweza kukataa amri ya kuizima hasa kwenye uchaguzi, Pia hata Twitter ni yake inakuwa ngumu kuwabana watu wasiitumie ikitokea mitandao mingine ya simu imezuiliwa kutumia twitter.