Elvis Kamsoba ni mshambuliaji mrundi kamili wa kutatua matatizo ndani ya Simba

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Naunga mkono Simba kumsajili mshambuliaji wa Burundi Elvis Kamsoba, amemzidi vitu vingi sana yule striker wa USMA Alger Leonel Ateba Mbida.

Kamsoba ana nguvu, namfananisha na marehemu Damian Kimti, mshambuliaji ambaye alileta changamoto kubwa enzi zile hasa kuhusu uraia wake hadi akafanikiwa kuchezea Simba sports club.

Kamsoba ndiye chaguo sahihi na mshambuliaji anayeweza kuisaidia Simba kwa sasa hasa kwenye nafasi ya Jeans Charkes Ahoua, Kamsoba mbali na nguvu pia ana kasi, mwepesi, ana chenga za maudhina alijua goli, mabeki wazembe wazembe kama Dickson Job na mwenzake Bacca ambao wanasifiwa wakati hawajakutana na washambuliaji wa kweli aina ya Kamsoba watasaga meno.

Nawaomba sana viongozi wa Simba, Kamsoba ni mali, Ngoma, Lakred na Freddy Michael watafute changamoto sehemu nyingine, Simba viungo wanatosha jamani.
 
Kwamba Simba wamebadili gia angani, badala ya ateba anakuja huyo mrundi?
 
Yanga wajanja wamekopa nguvu kutoka simba na azam kujiimarisha pia wakaenda congo na singida hawwjataka kabisa kwenda cameroon wala Ghana unajua kwanini?

Kwa sababu usajili ni bahati nasibu wakaona ni heri kuchukua watu wanao wajua vizuri

Huyo kamsaba simjui lakini ligi ya Rwanda ni sawa na cjampionship hapa bongo
 
Naunga mkono Simba kumsajili mshambuliaji wa Burundi Elvis Kamsoba, amemzidi vitu vingi sana yule striker wa USMA Alger Leonel Ateba Mbida.

Kamsoba ana nguvu, namfananisha na marehemu Damian Kimti, mshambuliaji ambaye alileta changamoto kubwa enzi zile hasa kuhusu uraia wake hadi akafanikiwa kuchezea Simba sports club.

Kamsoba ndiye chaguo sahihi na mshambuliaji anayeweza kuisaidia Simba kwa sasa hasa kwenye nafasi ya Jeans Charkes Ahoua, Kamsoba mbali na nguvu pia ana kasi, mwepesi, ana chenga za maudhina alijua goli, mabeki wazembe wazembe kama Dickson Job na mwenzake Bacca ambao wanasifiwa wakati hawajakutana na washambuliaji wa kweli aina ya Kamsoba watasaga meno.

Nawaomba sana viongozi wa Simba, Kamsoba ni mali, Ngoma, Lakred na Freddy Michael watafute changamoto sehemu nyingine, Simba viungo wanatosha jamani.
Hata huyu unayempigia Chapuo hapa hana lolote. Ukweli ni kwamba Simba SC kwa sasa hatuna Strong Scouting Team.
 
Itakuwa ni kosa kubwa sana na matumizi mabaya ya rasilimali za klabu kumuacha Ayoub Lakred. Simba ndiyo timu pekee duniani ambayo mchezaji akiumia tu anaachwa. Kwa staili hiyo, hauwezi kamwe kujenga timu imara ambayo wachezaji wanacheza kwa moyo wote.
 
Hata huyu unayempigia Chapuo hapa hana lolote. Ukweli ni kwamba Simba SC kwa sasa hatuna Strong Scouting Team.
Acha niendelee kuamini kama wewe hata kama tutatukanwa. Uliona wapi scout analeta mchezaji halafu kabla ligi haijaanza anaonekana fwafwa?
 
Halafu wana Simba SC tukiambiwa hatuna Akili na Kuchekwa tunaona kama vile tunaonewa wakati kiuhalisia ni Kweli.
 
Kazi mnayo watani, mtakiwa kutulia shida moja mnajilinganisha na Young Africans, mtapotezana ohooo
 
Unamfahamu big Brain defender wewe, au copro bacca? Labda atakuwa tishio kwenye mid table teams kama mashujaa na wengine
 
Back
Top Bottom