Uchaguzi 2020 Embu tuambizane ukweli, CHADEMA inatumia kigezo gani kusema itashinda?

Uchaguzi 2020 Embu tuambizane ukweli, CHADEMA inatumia kigezo gani kusema itashinda?

paul sylvester

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2020
Posts
3,503
Reaction score
3,499
Moja kwa moja hojani,

Kwa mjibu wa website ya CCM, na Kwa mjibu wa kauli ya mwenezi wa CCM ndugu Hamphuley Polepole, CCM inawanachama wa kudumu M.14+
Na kikawaida, ili uwe mwanachama wa Chama chochote, maana yake uwe umefikia umri wa miaka 18+

Na kwa idaadi ya waliojiandikisha kupiga Kura nchi nzima ni M.29+

Kama ndio hivyo, maana yake CCM, Kati ya wapiga Kura M.29+ CCm inamtaji wa nusu ya wapigakura wote ikiwa wote watakuwa wamejandikisha na kuipigia Kura CCM siku ya uchaguzi

Sasa basi, Ni Kwa namna Ipi Chadema wataishinda CCM?

Let go...

Mada hii imejikita kutaka kujua ni kwa kigezo kipi Chama cha Chadema kinatumia hadi washabiki na wanachama wake hasa mitandaoni kusema eti kitashinda?

Je, ni kwa sababu ya mwitikio wa watu kwenye Kampeni za mgombea wa Chama chao?

Je, ni kwa sababu ya kuhesabu uwingi wa washabiki na wachangiaji kupitia Mitandao ya kijamii?

Je, ni kwa sababu mgombea wa Chama hicho anajua sana sheria?

Je, ni kwa sababu mgombea wake anafahamiana na kujulikana na viongozi wa mataifa mengi duniani

Ni kwa sababu zipi haswa hawa Chadema kujiaminisha kuwa watashinda uchaguzi huu?

Kama ni Kwa sababu ya watu wengi kujaa katika mikutano yake, mbona hata haifikii uwingi wa watu wa mgombea na mpinzani wake Kutokea CCM?

Mbona Mikutano yake na jinsi watu inavyo jaa, ni kama Tu Ile mikutano anayoifanya waziri mkuu Majaliwa?

Mitaani watu wengi ukiwahoji, wanasema kwamba, Mgombea uriais kupitia Chadema, atashindana, lakini kushinda atashinda wa CCM

Nimalizie kwa kuuliza, je, ni kwa kigezo kipi kinachowapa wanachadema waseme Chama Chao kitamwangusha Magufuli?
 
Kizego cha mitandaoni kingine hakuna
Unajua mkuu, najitahidi sana kufuatilia Kampeni hizi, mwitikio wa watu, ukipima vizuri ukaondoa mihemko ya ushabiki wa vyama, utagundua kabisa, hata mwitikio wa watu Kwa mgombea Uraisi Chadema, unafanana Tu na mwitikio wa watu kwenye mikutano anayoendesha waziri mkuu
 
Ei_Hm12XsAMlqcE.jpeg


Wapiga kura wa CCM wakielekea samora

CCM inakatisha masomo wanafunzi na kuwavalisha hayo majezi ya kijani
 
Sababu zipo nyingi sina ila mimi nakupa dalili chache tu :-

1. Mkurugenzi wa uchaguzi umemsikia leo akimfanyia kampeni Magufuli? Hii ni moja ya dalili kama kuna kila dalili cdm kushinda uchaguzi huu, mkurugenzi amefanya jambo ambalo kwa akili za kawaida halikutakiwa kutokea,wasomi wanasema mkurugenzi wa uchaguzi amepanic au anaweweseka.

2. Polepole anafanya press kila baada ya 48h tena za matusi, press ambazo hazina maana yeyote ile. Kwa kifupi na yeye anarudi palepale kwa mkurugenzi kwenye kuweweseka.

3.Magufuli anasema mara kwa mara amefanya mambo mengi sana esp kwende miundombinu, ndio alikuwa anajivunia nayo kama kete yake ya ushindi, lakini Lissu jinsi alivyoua point zake za miundombinu amemfanya magufuli kucheza DEFENCE. Hii maana yake amezidiwa, Lissu anaonekana ni Rais na anajiamini na JPM ndio anaonekana mpinzani sasa.

4. Miaka yote CCM wanashinda kwa wizi, ila wagombea waliopita walikuwa wapole sana, ila mwaka huu wamempata chizi mwenzao, uzuri wa Lissu kama magufuli vile, siku zote magufili anasema yeye ni msema kweli daima, na huyu mgombea wetu pia ni msema kweli daima, anasema WAZI WAZI wakiiba kura lazima kinuke.

5. Wananchi wameichoka CCM, kila vijiwe havitaki CCM, kwa mazingira kama haya wanashindaje CCM kwa mfano.

6. Wingi wa watu unaowaona kwenye kampeni za CCM ni watu wanaosombwa na malori kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine, kwahyo wingi wa watu wa mikutano ya CCM ndio siyo halisia kabisa. Kwa mfano mama yangu mdogo anaishi Temeke ila wiki chache zilizopita alienda kwenye kampeni ya magufuli Tabora baada ya kusombwa na lori.
 
bado sana mkuu, bado hatujapata upinzani wa watu wenye akili timam ambao tunaweza sema tujaribu kuwapa nchi
Jeunamaanisha hata wakishinda hamu wapi nchi. Rejea maneno yako haya bado hatujapata upinzani wa watu wenye akili timam ambao tunaweza sema tujaribu kuwapa nchi huoni hiyo ndio sababu ya chadema kuamini wao hushinda kila chaguzi ila tu maamuzi yenu na siyo ya wapiga kura ndio huwatoa ktk ushindi. 😊
 
Wanakwambia"watu wamelala barabarani ili Lissu asimame aongee wamsikie,kweli Lissu ni Rais"

yani kwa watu kulala barabarani basi ndo kigezo cha Lissu kushinda urais.Chadema ndo matahira kweRi kweRi.
Kwa huu uzwazwa wenu mkiongozwa na mwenezi wenu wakutukana tuuu wapinzani wenu, hii ni dhahiri inaonesha uchaguzi umewashinda na mmepanik haswaaa😂😂😂
 
Back
Top Bottom