Sababu kubwa ya Chadema kushinda ni kwa vile mgombea wa CCM hakubaliki kwa makundi mengi ya kijamii kama vile wakulima, wafanyabiashara, wafanyakazi, wahitimu vyuo vikuu, bodaboda, mgombea wa CCM ni katili, mjivuni, mtu wa visasi na asiyewajali wananchi.
Hebu linganisha Magufuli wa 2015 na sasa, Magufuli wa 2015 alijipambanua kama mchapakazi lakini wa sasa anajipambanua kama katili, mjivuni na mwenye visasi.
Wingi wa watu kwenye mikutano ya wagombea hawa isikupe shida sana, wanaoenda kwenye mikutano ya CCM wanafuata mengi tukiachana na malori wengi hufuata wasanii, hukumbuki Clouds ilikuwa inajaza watu kwa kiingilio sasa ni bure kwanini watu wasijae. Tofauti yao ni kwamba wa Lissu ni wachangamfu na Magufuli wamesinyaaa na ukumbuke hao hao wanaoenda kwa Magufuli ndio wanaoenda kwa Lissu.
Kama alipata 57% kipindi kile tegemea kura zake kupungua kwa sababu kipindi kile aligombea akijipambanua kwa uchapakazi, hakuwa amewakera wakulima, wafanyabiashara, wafanyakazi wala wahitimu vyuo vikuu, kipindi kile hali ya Uchumi haikuwa mbaya, kipindi kile aligombea na mgombea mwenye tuhuma za ufisadi ambazo zilikuwa zinawakera Watanzania wengi, mgombea wa upinzani alikuwa dhaifu na ambae hakuwa na uwezo wa kujenga hoja na alikuwa ambae alitokana na chama cha mapinduzi sasa hivi upinzani wana mtu mwenye uwezo wa kujenga hoja na mpinzani halisi.