Embu tumjadili Rais ajaye wa awamu ya sita 2025

Embu tumjadili Rais ajaye wa awamu ya sita 2025

"Mwisho wa uchaguzi mkuu mmoja ni mwanzo wa uchaguzi mkuu mwingine" JAKAYA KIKWETE.

Je, Rais wetu 2025, awe mtu wa aina na sifa zipi? Hapa chini natoa baadhi kwa maoni yangu. (nawe toa yako);

1) Awe na sifa, uzoefu na uwezo wa kusimamia vyema tunu za taifa kwa manufaa ya wote. Mfano amani, haki na usawa, uhuru, umoja, utawala bora na muungano wenye tija.

2) Atoke CCM ila asiwe mhafidhina wa U-CCM ule ulioathiri taifa na kutufanya kuendelea kuwa maskini miaka 59 toka tupate uhuru, Kwa maoni yangu upinzani kwa mwaka 2025 hautaweza kuaminika kuchukua dola kwani mifumo ya ndani ya vyama bado ni dhaifu na pia mifumo nje ya vyama bado ni hatarishi kuweza kuvipa vyama hivyo smooth operation.

3) Awe muislam na mwenye mawazo huru. Hapa sizungumzii udini, nazungumzia life principles. Kwa maoni yangu viongozi wa kiislam wanaonesha sana kusikia na kujali vilio vya watu. Tumeona kwa awamu zake nchi hii. Nina imani kwa maumivu yaliyopo sasa, kiongozi wa aina hiyo atatufaa sana.

3) Awe kiongozi atakayependa serikali mseto. Uwakilishi wa vyama kadhaa ndani ya serikali na jinsia pia.

4) Awe tayari kurekebisha mfumo wa utawala wa nchi kwa kuridhia upatikanaji wa katiba mpya itakayohakikisha, mihimili ya dola inakuwa huru zaidi, madaraka ya raisi yanapunguzwa zaidi, muungano unakuwa bora zaidi, wananchi wanafurahia uhuru wao na mipaka yake zaidi n.k

ENDELEA...
Uchaguzi wa 2025 kuanza kuuzungumzia muda huu ni kupoteza muda tu mkuu, ya mbele ni mengi hivyo iwe mvua au jua 2025 hakuna uchaguzi bila tume huru, katiba mpya, au vifungu vilivyo kwenye katiba ya sasa kurekebishwa, chaguzi za kuachia watu vilema, majeraha ya moyo hakuna. Itakua busara kama hamtaki, mwongezeeni mda Rais aliyepo hata miaka hamsini ijayo ila chaguzi kama za mwaka huu hazihitajiki tena asee.
 
Huyu unaemuona utamuona hadi atwaliwe na MUUMBA na noti anabadilisha anaweka sura yake. Very soon.
 
Ndugu nakuonea sana huruma juu ya uwezo wako wa kuchambua mambo ya siasa (japo una uhuru huo wa kufanya hivyo).

3) Awe muislam na mwenye mawazo huru. Hapa sizungumzii udini, nazungumzia life principles. Kwa maoni yangu viongozi wa kiislam wanaonesha sana kusikia na kujali vilio vya watu. Tumeona kwa awamu zake nchi hii. Nina imani kwa maumivu yaliyopo sasa, kiongozi wa aina hiyo atatufaa sana.

Naomba utaje hapa jukwaani ni principles zipi za maana ambazo marais wastaafu wa Tanzanina waislamu wamezionyesha na marais wastaafu wakristo hawkuzionyesha. Usitake kuleta mada chochezi kwa mslahi yako na upeo wako mdogo wa kushabikia udini katika tifa ambalo lina diversification ya dini na uhuru wa kuabudu.

Tangu lini dini ya mtu ikawa ni sifa ya kuchaguliwa katika nafasi ya uongozi wa serikali (nchi)? Unataka kutuaminisha kwamba marais waliotangulia ambao ni waislam walifanya waliyofanya wakiwa madarakani kwa sababu ni waislamu? Kama ni rushwa kutamalaki katika kipindi cha uongozi wao ina maana dini ya kiislamu ndiyo inayoruhusu rushwa pamoja na maovu mengine ambayo yalitendeka katika awamu zao za urais?.

Hakuna kitu ninachokichukia katika Tanzania kama mtu kuweka udini na ukabila mbele kama kigezo cha kuomba uongozi. Na mwalimu Nyerere alishasema katika moja ya hotuba zake kwamba wanasiasa/watu waliofilisika hoja/sera za kisiasa mara nyingi hukimbilia kwenye udini na ukabila. Maendeleo ya Tanzania hayataletwa na dini ya mtu bali uzalendo toka moyoni mwake kwa nchi yake. Dini ni jambo binafsi la mtu. Hivyo kusema kwamba eti rais akiwa wa dini fulani ndiyo maisha ya watanzania yatakuwa mazuri huo ni ULOFA NA UPUMBAVU (in Benjamin Mkapa's Voice-RIP)
Acha ujinga na kujitoa akili mbona mtoa mada kaelezea vizuri hata mtoto wa darasa la pili anaelewa?
 
Umeshinda kwa wizi wa kura na kumwaga damu unataka uungwe mkono na nani. Watakuunga mkono waliokupa kura na kukusaidia kuiba kura. Na kama ni wafadhili wasitoe hela zao, maana ndio zinatumika kumwaga damu za wananchi.
Dah mkuu umeandika kwa machungu sana, but all in all God is alive.
 
Tunataka rais atakayekubali katiba mpya, tena ile ya rasimu ya Warioba, aheshimu maoni ya watu, na asijigeuze kuwa Mungu mtu kwa kiburi cha madaraka.
kifupi nchi irudishwe kwa wananchi. kwa sasa imeshikiliwa na kikundi kidogo cha watu
 
Ndugu nakuonea sana huruma juu ya uwezo wako wa kuchambua mambo ya siasa (japo una uhuru huo wa kufanya hivyo).

3) Awe muislam na mwenye mawazo huru. Hapa sizungumzii udini, nazungumzia life principles. Kwa maoni yangu viongozi wa kiislam wanaonesha sana kusikia na kujali vilio vya watu. Tumeona kwa awamu zake nchi hii. Nina imani kwa maumivu yaliyopo sasa, kiongozi wa aina hiyo atatufaa sana.

Naomba utaje hapa jukwaani ni principles zipi za maana ambazo marais wastaafu wa Tanzanina waislamu wamezionyesha na marais wastaafu wakristo hawkuzionyesha. Usitake kuleta mada chochezi kwa mslahi yako na upeo wako mdogo wa kushabikia udini katika tifa ambalo lina diversification ya dini na uhuru wa kuabudu.

Tangu lini dini ya mtu ikawa ni sifa ya kuchaguliwa katika nafasi ya uongozi wa serikali (nchi)? Unataka kutuaminisha kwamba marais waliotangulia ambao ni waislam walifanya waliyofanya wakiwa madarakani kwa sababu ni waislamu? Kama ni rushwa kutamalaki katika kipindi cha uongozi wao ina maana dini ya kiislamu ndiyo inayoruhusu rushwa pamoja na maovu mengine ambayo yalitendeka katika awamu zao za urais?.

Hakuna kitu ninachokichukia katika Tanzania kama mtu kuweka udini na ukabila mbele kama kigezo cha kuomba uongozi. Na mwalimu Nyerere alishasema katika moja ya hotuba zake kwamba wanasiasa/watu waliofilisika hoja/sera za kisiasa mara nyingi hukimbilia kwenye udini na ukabila. Maendeleo ya Tanzania hayataletwa na dini ya mtu bali uzalendo toka moyoni mwake kwa nchi yake. Dini ni jambo binafsi la mtu. Hivyo kusema kwamba eti rais akiwa wa dini fulani ndiyo maisha ya watanzania yatakuwa mazuri huo ni ULOFA NA UPUMBAVU (in Benjamin Mkapa's Voice-RIP)
Hakuna jambo silipendi kama hili, la watu kuchambua mambo ya kiuongozi kwa kuegemea udini. Tunachopaswa kutambua siku zote ni kwamba kiongozi siku zote huwa hana dini! Ikishakua kiongozi dini yako ni Utanzania tu basi. Kitendo cha mtu kuchaguliwa au kuteuliwa inapaswa atambue kwamba yeye ni mtu huru kiimani, hivyo watu wa michepuo yote ni ndugu zake, sasa huo uchambuzi wa kuegemea dini fulani kwa Tanzania hauna nafasi.
 
3) Awe muislam na mwenye mawazo huru. Hapa sizungumzii udini, nazungumzia life principles. Kwa maoni yangu viongozi wa kiislam wanaonesha sana kusikia na kujali vilio vya watu. Tumeona kwa awamu zake nchi hii. Nina imani kwa maumivu yaliyopo sasa, kiongozi wa aina hiyo atatufaa sana.
IMEANDIKWA KWENYE KATIBA???MBONA MBARA ANAKUJA MZENJI ILIKUFA...ACHA WATU WAPAMBANE HAKUNA SLOP KITONGA
 
Hayo yote wazungu wa Afrika kusini walifanya, lakini bwakina Mandela waliwapinga. Tunataka utawala bora, na vitu isiwe sababu ya kuonea wasiokukubali.
Hii ni akili kweli? Au uwezo wa mtu mwenye fikra finyu na potovu
 
Majaliwa, Suleiman Jafo na Hussein Mwinyi ingawa kwa Mwinyi sio lazima sana ila kama atapaform vizuri kule Zanzibar tunaweza kumfikiria.
 
Aheshimu utawala wa sheria, apeleke maendeleo kwa wananchi wote bila kujaki itikadi za chama maana wote ni walipa kodi

Pia awe ni Rais mwenye leadership skills za hali ya juu

Rais ambae hotuba yake itatoa matumaini kwa wananvhi na sio kuwafanya wananchi watamani kufa
 
Watanzania hawaangalii mtu bali vyama, yeyote watakae chaguliwa na chama ndio huyohuyo wanampigia kura.

Utasikia Watanzania wanasema fulani ni mpango wa Mungu.
 
Achana na mambo ya udini. Hayo ndo yameturudisha nyuma kila mwaka. Kiongozi atachaguliwa kutokana na uwezo wake sio dini yake au kabila lake. Ikulu hatupeleki shehe wala kasisi au mchungaji. Tunampeleka mbeba maono ya maisha ya maendeleo ya Watanzania wote. Na wala sio lazima kila baada ya Rais mkristo lazima eti aje muislam. Hiyo kasumba hatuwezi kuendelea nayo tena.
 
Unazidi kuaminisha umma wa watanzania umefirisika kifikra,nafikiri anguko la Chadema limekufanya uwe unawaza pumba.

Nimecheka kwa nguvu. Ni kweli kabisa, anguko la Chadema la kura za kwenye mabegi na umwagaji damu lazima linifanye niwaze pumba.
 
Back
Top Bottom