Embu tumjadili Rais ajaye wa awamu ya sita 2025

Embu tumjadili Rais ajaye wa awamu ya sita 2025

Akidhi vigezo vya kuwa Rais kwa mujibu wa katiba
 
Hiyo namba 3 nakuunga mkono kabisa, inaelekea waislamu wana somo la ubinadamu sana.
 
Kama mwenyewe alisema Raisi ajaye lazima awe kijana angalieni kwenye baraza la mawaziri ni nani kijana, hapo utajua Rais ajaye ni nani
 
Maneno mengi ya nini, Rais tayari yupo
Jina lake ni Hussein, kumrithi aliyepo
Na yupo mazoezini, abishae mimi sipo
Dua tuna muombea, asipatwe na ghururi.

Atosha kila idara, Brazajei nisikie
Na wala hana papara, anafanya yatimie
Si wa kukuru kakara, ya Rabbi utupatie
Kiti ni cha Hussein, Ali mtoto wa Mwinyi.

CC: Brazaj
 
Hatutaki kwasababu iliyatupilia chooni maoni ya wenye nchi/ wananchi ikachukua maoni ya wana Ccm.
Mfano tulipendekeza matokeo ya uraisi yapingww mahakamani mkakataa kwa sababu ya wizi wenu wa kura.
Tulipendekeza serikali tatu mkakataa kwa sababu mnataka kuendelea kuitawala zanzibar.
Tulipendekeza mbunge angalau awe na bachelor mkakataa kwa sababu mnawategemea kina kibajaji
Nk
Mlipendekeza wewe na nani mm mbona sikubaliani nawe? Jitahidi kujisemea wewe usisemee wengine
 
Raisi ajaye atazungumziwa 2024. Anaweza kuwa huyu huyu kama watz wakimlazimisha.
Mm nafikiri huyu huyu anatufaa bado sijaona mwingine ambaye ni bora kuliko huyu nafikiri ikibidi tutamlazimisha huyu huyu aendelee walau kwa miaka kumi mingine
 
Kwa rotation vya dini, kabila na ukanda inabidi saa hizi Rais ajaye atoke North .
 
Mm nafikiri huyu huyu anatufaa bado sijaona mwingine ambaye ni bora kuliko huyu nafikiri ikibidi tutamlazimisha huyu huyu aendelee walau kwa miaka kumi mingine
Ikiwapendeza wananchi na iwe hivyo. Ndo demokrasia hiyo.
 
Endelea kuota wafadhili mpaka uzeeke. Dunia inakwenda kasi ndugu hela ya wafadhili ina macho. We komalia wafadhili wafadhili, kwa kweli ni wimbo uliotuchosha kuusikia. Tunaomba uje na wimbo mpya ili tukusikilize.
Umeshinda kwa wizi wa kura na kumwaga damu unataka uungwe mkono na nani. Watakuunga mkono waliokupa kura na kukusaidia kuiba kura. Na kama ni wafadhili wasitoe hela zao, maana ndio zinatumika kumwaga damu za wananchi.
 
Nimecheka kwa nguvu. Ni kweli kabisa, anguko la cdm la kura za kwenye mabeg na umwagaji damu lazima linifanye niwaze pumba.
Kura za kwenye mabegi za maigizo toka kwa wahuni! Ambao sasa wanaenda kutinga mjengoni kama viti maalumu, ndio wanakufanya uwaze pumba na kujitoa akili?
 
Endelea kuota wafadhili mpaka uzeeke. Dunia inakwenda kasi ndugu hela ya wafadhili ina macho. We komalia wafadhili wafadhili, kwa kweli ni wimbo uliotuchosha kuusikia. Tunaomba uje na wimbo mpya ili tukusikilize.

Ni kweli hupaswi kutegemea hela ya mfadhali, lakini ukiwa masikini fedha ya mfadhili haikwepeki. Unapoona biashara zinafungwa na watu kuzidi kukosa ajira, unakwepaje fedha ya mfadhili labda?

Subiri kila kitu kitawa wazi japo inatumika nguvu kubwa kuhakikisha ukweli hauwekwi wazi.
 
Kura za kwenye mabegi za maigizo toka kwa wahuni! Ambao sasa wanaenda kutinga mjengoni kama viti maalumu,ndio wanakufanya uwaze pumba na kujitoa akili?

Nimeziona kwa macho, achia mbali uhuni mwingine wa wazi, ikiwemo kuwaengua wapinzani na hujuma nyingi za wazi.
 
"Mwisho wa uchaguzi mkuu mmoja ni mwanzo wa uchaguzi mkuu mwingine" JAKAYA KIKWETE.

Je, Rais wetu 2025, awe mtu wa aina na sifa zipi? Hapa chini natoa baadhi kwa maoni yangu. (nawe toa yako);

1) Awe na sifa, uzoefu na uwezo wa kusimamia vyema tunu za taifa kwa manufaa ya wote. Mfano amani, haki na usawa, uhuru, umoja, utawala bora na muungano wenye tija.

2) Atoke CCM ila asiwe mhafidhina wa U-CCM ule ulioathiri taifa na kutufanya kuendelea kuwa maskini miaka 59 toka tupate uhuru, Kwa maoni yangu upinzani kwa mwaka 2025 hautaweza kuaminika kuchukua dola kwani mifumo ya ndani ya vyama bado ni dhaifu na pia mifumo nje ya vyama bado ni hatarishi kuweza kuvipa vyama hivyo smooth operation.

3) Awe muislam na mwenye mawazo huru. Hapa sizungumzii udini, nazungumzia life principles. Kwa maoni yangu viongozi wa kiislam wanaonesha sana kusikia na kujali vilio vya watu. Tumeona kwa awamu zake nchi hii. Nina imani kwa maumivu yaliyopo sasa, kiongozi wa aina hiyo atatufaa sana.

3) Awe kiongozi atakayependa serikali mseto. Uwakilishi wa vyama kadhaa ndani ya serikali na jinsia pia.

4) Awe tayari kurekebisha mfumo wa utawala wa nchi kwa kuridhia upatikanaji wa katiba mpya itakayohakikisha, mihimili ya dola inakuwa huru zaidi, madaraka ya raisi yanapunguzwa zaidi, muungano unakuwa bora zaidi, wananchi wanafurahia uhuru wao na mipaka yake zaidi n.k

ENDELEA...
Mnaanza kunijadili mapema hivi kwani hamnijui?
 
Baada ya miaka 5 ya Magufuli bado kuna watu vichwa ngumu ziara ya Aweso tumeona jinsi wakala wa maji vijijini anavyovyurunda vitendea kazi kama magari na mitambo ya serikali chali ila mitambo ya kampuni binafsi inayomilikiwa na mwenyekiti wa taasisi inafanya kazi kama kawa.

Unajiuliza hao mamlaka ya teuzi na viongozi waliopita hawakuona conflict of interest wakati wanampendekeza huyo bwana.

Huko Chunya kwenye madini ndio balaa baada ya bunge kuvunjwa kipindi cha uchaguzi, tamisemi na kwenyewe ivyo ivyo Jaffo aliporudi jimboni huko nako ikawa fungulia mbwa.

Hapo tuna raisi watendaji wakimuona wanapata kigugumizi cha kuongea kwa woga, ila akipita tu watu wanaendelea na nayo kama kawaida as far as they are concerned anakuwa tatizo la wengine atakaokutana nao mbele ya safari.

Atuwezi kuwa na raisi ambae ukali wake ni short of Magufuli ili nchi iende, unless kama tunataka turudishe uzembe uliokithiri serikalini.
 
Back
Top Bottom