MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Ni kwa sababu kilichomleta Afrika hakipo TanZania, amekwenda Uganda kwa sababu Baba yake alikuwa moja ya mateka waliouliwa Entebe wakati Wayahudi walipochukuliwa mateka, amekwenda Kenya kwa sababu ya mambo ya usalama na mambo ya Al Shabab ambapo Israeli inataka kuizuia Kenya silaha ili ipambane na Ugaidi na isitoshe Raisi Uhuru Kenya alimualika alipokuwa huko Israeli, amekwenda Rwanda kwa sababu wana makubaliano na Serikali ya Rwanda kurudisha wakimbizi wa kiafrika waliokuwa Israeli, Israeli haiwataki hivyo wamekubaliana au wana mpango wa kukubaliana na Rwanda iwachukuwe halafu Israeli itailipa Rwanda fedha, sasa ulitaka aje TanZania kufanya nini?
Au ulifikiri Wazungu ni Waafrika wanajiendea tu kila mahali? Labda nikuulize kulikuwa na ulazima gani wa Raisi Uhuru Kenya kwenda Uganda wkt Netanyahu alikuwa anakuja Kenya kesho yake tu?
Kuna mambo mengi Kenya iliingia kwenye makubaliano na Israel kwenye kikao baina ya Uhuru na Israel, ni zaidi ya usalama.
Pia na yale majadiliano yaliyofanyika kiukanda baina ya marais na Israel ambapo Uhuru alikwenda Uganda kuhitimisha.
Zaidi pia marais nao wakakutana baina yao na kuingia kwenye majadiliano.
Juzi niliona sehemu kwamba mpo tayari kuhusisha mkarimani ili mtumie Kiswahili kwenye vikao vya kimataifa. Bora mharakishe hilo maana kuendelea kuogopa ogopa hivi, kuna mambo mengi yatawapita.