Emmanuel Buhohela: Hatuna taarifa rasmi kuwa Uingereza ilipiga marufuku wasafiri kutoka nchini Tanzania kuingia nchini humo

Emmanuel Buhohela: Hatuna taarifa rasmi kuwa Uingereza ilipiga marufuku wasafiri kutoka nchini Tanzania kuingia nchini humo

Utafikiri ni mtu hajasoma yani huyu jamaa bado hajui nguvu ya mitandao ya kijamii au anataka watu waende halafu wapate usumbufu ambao hauna maana. Jinsi nchi za nje wanavyoshughulikia suala la corona ni tofauti kbsa na tanzania, ajue watu wako makini na afya za raia wao siyo bongo siasa mpaka kwenye masuala ya taaluma za watu
 
Mkuu habari za mitandaoni inafuatiliwa kwa karibu sana kama jipu linalotaka kupasuka.

Tatizo nani aanze kuwasilisha hatua za barua za kiserikali.

Ingekuwa ni majahili wanatoa angalizo kuwa watashambulia, habari za kimtandao zitashughulikiwa bila barua rasmi.
Kuna tofauti ya mtu kusema atakupiga kwa kukuambia mwenyewe na kwa kusikia kwa mtu watatu.
 
Unajitekenya na kucheka mwenyewe!
Hata utumie lugha gani lakini ukweli utabaki kuwa ukweli, nao ni terrorists atatumia njia za pori kutoa habari zake na nchi/serikali zitatumia njia zinazo tambulika kutoa taarifa kwa nchi nyingine.
Period .
 
Iarifu leo JF kuwa kesho utaandamana, halafu usikie muziki wake
 
Unaendeleza ujinga wako , wa kulinganisha muhalifu na nchi au vyombo vya serikali vinavyo wasiliana
Nimekupa hiyo uelewe, officialy or not, try to threaten the status quo, you’ll face the music.
Wewe ita ujinga, lakini onja sumu ujue utamu wake!
 
Nimekupa hiyo uelewe, officialy or not, try to threaten the status quo, you’ll face the music.
Wewe ita ujinga, lakini onja sumu ujue utamu wake!
Sasa uingereza one threaten the status quo, mbona , unaweka mifano ambayo haiendani
 
Sasa uingereza ndio wana threaten the status quo, mbona , unaweka mifano ambayo haiendani
 
Mkurugenzi wa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje, Emmanuel Buhohela, amesema wao hawana taarifa rasmi kwamba Uingereza imepiga marufuku wasafiri kutoka nchini Tanzania kuingia nchini humo na kueleza kuwa hayo ni mambo ya mitandaoni na wao hawayafuatilii.

Chanzo cha Taarifa: EastAfricaTV

==========

Mkurugenzi wa Habari Wizara ya Mambo ya Nje, Emmanuel Buhohela, amesema kuwa wao hawana taarifa rasmi kwamba Uingereza imepiga marufuku wasafiri kutoka nchini Tanzania kuingia nchini humo na kueleza kuwa hayo ni mambo ya mitandaoni na wao hawayafuatilii.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 23, 2021, wakati akizungumza na EATV&East Africa Radio, na kuongeza kuwa serikali inao utaratibu maalum wa kupokea taarifa hizo za namna hiyo na kwamba ingekuwa vyema zaidi kama Ubalozi wa Uingereza ungeulizwa kama hiyo kauli ni ya kwao.

"Utaratibu wa serikali ni kwamba kuna utaratibu wa kuwasiliana, kwahiyo hayo mambo ya kwenye mitandao hatuwezi kuyazungumzia, mimi binafsi nimeiona kama wewe ulivyoiona, serikali haiwasiliani kwenye mitandao bali ina utaratibu wake", amesema Buhohela

Aidha Buhohela ameongeza kuwa, "Kwenye mitandao mambo mangapi ya uongo yanayoandikwa, kama tukipata maandishi au document kutoka Uingereza tutalizungumzia, au mngewapigia Ubalozi wa Uingereza kuwauliza kama hiyo kauli ni ya kwao"

Katibu Mkuu wa Uchukuzi wa Uingereza Grant Shapps, kupitia ukurasa wake wa Twitter, aliandika kwamba zuio la wasafiri kutoka Tanzania na DR Congo, limeanza jana Ijumaa Januari 22, 2021, ikiwa ni hatua za kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19, kufuatia kuibuka kwa kirusi kipya cha ugonjwa huo nchini Afrika Kusini
Wakati mwingine waTZ hushangaza sana.
Natamani Emmanuel akae mbele ya PC ajaze form ya kuombe visa ya kwenda UK aone majibu yake ndipo ataelewa secretary alichoandika.
 
Back
Top Bottom