Pre GE2025 Emmanuel Chacha: Mbowe akichaguliwa tena Mwenyekiti nitaachana na CHADEMA milele

Pre GE2025 Emmanuel Chacha: Mbowe akichaguliwa tena Mwenyekiti nitaachana na CHADEMA milele

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama wajumbe wakifanya hilo kosa, watakuwa wamemwunga mkono Mbowe katika jitihada zake za kuiua CHADEMA ili kutimiza mkataba wake wa kuhakikisha mgombea wa CCM anakosa mpinzani.
 
Kwa Ujumla vyama vya Upinzani Tanzania specifically CHADEMA mmeonyesha bado sana. Mmewakatisha watu wengi sana tamaa this time. Itachukua miaka mingi sana watu kuanza kuwafikiria. Maturity 0% Emotional intelligence 0%, selfishness 100% etc
Jebu tueleze wamewakatisha tamaa watu wengi kivipi?
 
Tumpe Pole Emmanuel CHACHA alikuwa hajui Kuwa siasa Ya Tanzania ni Mchaga Original itoke iende Wapi!?

View attachment 3207267








Wikipedia
Tafuta

Wachagga​

kabila la Kenya na Tanzania

Wachagga[1] ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu (lakini pia mchanganyiko wa damu, hasa ya Kikushi) wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro.
Nyumba ya asili huko Marangu.
Wachagga ni kabila la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania.[2] Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi yao ni watu 2,000,000. Hata hivyo kabila hilo ni kama mchanganyiko wa makabila madogomadogo yenye lugha tofauti, jambo la pekee nchini Tanzania.
Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara, kilimo na kazi za ofisini.

Vikundi vya Wachagga/Fitina​



Lugha ya Kichagga/FITINA​





Koo za Kichagga/FITINA​









Utawala wa jadi wa Wachagga/FITINA​



Elimu kati ya Wachagga/FITINA​








Ardhi/FITINA​




Kilimo na chakula/FITINA​









Maoni juu ya Wachagga/FITINA​
















Tanbihi/FITINA​




Marejeo/FITINA​






Viungo vya nje/FITINA​




mwisho imehaririwa miezi 5 iliyopita na Riccardo Riccioni


Wikipedia

Acha uzushi, hiyo sensa ya makabila ulifanya na bibi yako?
 
Sasa chama kitapungukiwa nini akiondoka, kama aliondoka nyerere na ccm inadunda hadi leo
Aliondoka Nyerere, chama kikabaki, ndio, lakini CCM ni ile ile ?

Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Nyerere kakalia kiti cha mbele, wangethubutu ku waste time and attention ya Taifa kuimbiwa na Zuchu na Bozi Boziana na Mwijaku na Konde Boy na Baba Levo na Marioo akaimba mwimbo wa mapenzi pale mbele ?

Chama kinabaki ndio, lakini kinabadilika. Kwani NCCR ya Marando na Mrema imekufa ? Ipo. Ni ile ile ??? Imepwaya!

CUF ya Maalim Seif, Ismail Jussa, na Hamad Radhid imekufa ? Ipo. Ni ile ile ????? Imepwaya!

Heshimuni michango ya watu wote chamani.
 
Acha uzushi, hiyo sensa ya makabila ulifanya na bibi yako?
Walau ni Bibi nilidhani babu yangu Wikipedia unataka tushindane na mtandao wa kijamii utaanzia wapi!

Sema tu wamesema unichukie kwa sababu sitashiriki maandamano 2025 maana Fitina zote mnamiliki nyie

600px-Marangu19.jpg
 
Siyo yeye tu, ana watu mamilioni ya watu tutakaoondoka Chadema
Wenyeviti wa mikoa wanaomuunga mkono Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, wameibuka na kukanusha madai kwamba Tundu Lissu anaungwa mkono na wenyeviti wa mikoa 25.

Wamesisitiza kuwa madai hayo ni propaganda zisizo na ukweli, huku wakimuelezea Mbowe kama kiongozi wa pekee mwenye uwezo wa kuimarisha chama katika uchaguzi wa uenyekiti unaotarajiwa kufanyika Januari 21, 2025.

Katika mkutano wao na waandishi wa habari uliofanyika Januari 19, 2025, jijini Dar es Salaam, viongozi hao waliweka wazi kuwa idadi kubwa ya wenyeviti wa mikoa inaendelea kumuunga mkono Mbowe.

Edward Kinabo, mwakilishi wa timu ya kampeni ya Mbowe, alisema kuwa: "CHADEMA ina wenyeviti wa mikoa 33. Hivyo, taarifa kwamba Tundu Lissu anaungwa mkono na wenyeviti 25 ni za kupotosha. Wenyeviti wa mikoa wengi wapo nasi, na leo tumewakilishwa na wenyeviti 17, huku wengine wakiwa njiani kuelekea Dar es Salaam."

Kinabo ameongeza kuwa madai ya wapinzani wao ambao ni upande wa Lissu hayana msingi wowote na yanaonekana kama juhudi za kujaribu kuathiri uchaguzi.

Masaga Kaloli, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya, ametoa kauli kali kuhusu nia ya Tundu Lissu kugombea nafasi ya Mwenyekiti:

"Hatumuungi mkono Lissu si kwa sababu tunamchukia, bali kwa sababu hatuoni nia njema katika azma yake ya kugombea. Huyu ni kiongozi anayekosa umoja na mshikamano na viongozi wenzake. Zaidi ya hayo, wale wanaomzunguka ni watu wanaotafuta madaraka kwa njia zisizo za heshima."

Kaloli amesisitiza kuwa uchaguzi wa CHADEMA Taifa unapaswa kuwa wa kuheshimiana na si wa kutoa madai yasiyo na ukweli.

Naye Henry Kileo, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kinondoni, amewashutumu baadhi ya wafuasi wa Tundu Lissu kwa kile alichokiita kuvuruga chama kwa kutoa kauli za kichochezi. Amesema kuwa kauli za Godbless Lema, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, zimekuwa chanzo cha sintofahamu ndani ya chama.

"Lema anavuka mipaka na kutoa kauli zisizo na heshima kama vile 'asiposhinda fulani sitakuwa mwanachama wa chama hiki.' Hii siyo demokrasia tunayopigania. Tunawaomba wote wawe watulivu na waheshimu taratibu za chama." Amesema
 
Walihama kina Zitto Kabwe na bado Chadema kilibaki kuwa imara.
Ilibaki imara? Pending ujio wa Lowassa chadema was heading to abyss. Pia zitto alikua suspect sana kwa collusion na CCM tofauti na Lissu ambaye ni Anti-establishment na ameonyesha kuwa ni mpinzani halisi tokea enzi za Mkapa mpaka leo hakuwahi kuyumba.

Mbowe hakuwa amechokwa then ila sasa amechokwa, so kama zitto angekua zama hizi yangejirudia haya haya. Mbowe akishinda ndio kifo cha chadema,
 
Jebu tueleze wamewakatisha tamaa watu wengi kivipi?
Hili linajieleza..bado vyama vyetu ni vichanga sana kwenye uongozi.. hakuna chama cha siasa kinaweza kuwa na viongozi wanaoweka kila wanachozungumza kuwa Public. Kila kiongozi anaanda press conference kuanzia taifa hadi ngazi ya Tawi. Inamaana chama kimekosa utaratibu wa ndani au lilikuwa kundi la watu ambao hawajafikia level inayotakiwa ya kiuongozi...
Kwa ujumla mmeushangaza ulimwengu...nendeni Kenya au Zambia mkajifunze kama mmeshindwa kujifunza CCM..
 
Awamu hii cdm itabaki na wahuni machawa tu.
Tumewaonya wajumbe wenye matamanio ya kugombea ubunge na udiwani waachane na Mbowe.
Mbowe kakataliwa na umma na kuambatana naye ni kupishana na kura za watz walio wengi.
Kesho ndio mwisho wa kelele zenu timu Lisu atakapopigwa chini kwenye uchaguzi
 
Aliondoka Nyerere, ndio, na chama kipo, lakini CCM ni ile ile ?

Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Nyerere kakalia kiti cha mbele, wangethubutu waste time and attention ya Taifa kuimbiwa na Zuchu na Bozi Boziana na Mwijaku na Konde Boy na Baba Levo na Marioo akaimba mwimbo wa mapenzi pale mbele ?

Chama kinabaki ndio, lakini kinabadilika. Kwani NCCR ya Marando na Mrema imekufa ? Ipo. Ni ile ile ???

CUF ya Maalim Seif, Ismail Jussa, na Hamad Radhid imekufa ? Ipo. Ni ile ile ?????

Heshimuni michango ya watu wote chamani.
Yaani kusema ukweli huku kugombea kwa Lissu uenyekiti wa CHADEMA kumefanya wana JF waanike utupu wa vichwa vyao.
Yaani mtu anadiriki kuonyesha kuwa mchango wa mtu mmoja mmoja hauheshimiwi kisa tu kupinga kitu fulani!!!???
 
Back
Top Bottom