Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,200
Kama lipo kosa analojilaumu Emma basi ni la yeye kuanzisha uasi kwa kile kilichotangazwa na na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wakati huo ndugu Jakaya .M. Kikwete kuhusu kukatwa kwa jina la bwana E. N. LOWASA kwenye kinyang'anyiro cha kuteuliwa kuwa mgombea wa u Rais kupitia CCM.
Kwa kawaida alichokifanya Nchimbi ki demokrasia hakukuwa na ubaya wowote lakini lijapo upande wa pili ni kosa kubwa la kudharau mamlaka iliyo juu yako na adhabu yake ni KUTOKUAMINIKA TENA na hilo ndilo limemuondelea sifa kuu ya yeye kuja kuwa kiongozi mkubwa ndani ya Taifa hili. Jambo hilo hata yeye mwenyewe alipo analitambua na huenda anaendelea kujutia hakika!
Kwa Nchi kama yetu hii ukiona unatupwa Ubalozini huku nyuma ulipata kuleta ukakasi kwenye jambo/mambo fulani kama alivyofanya Nchimbi tambua ndiwo mwisho wako wa kuwa mwana siasa utamaniye kuwa mkubwa hapo baadae.
Sielewi ni sababu ipi ilimfanya Nchimbi ajitokeze hadharani na kufanya kile alichokifanya ilhali wazi utaratibu wa namna ya kushugulikiwa kwa mtu wa aina ile aliyoichagua kufanya aliielewa vizuri!
Kwa nini hakujizuia kwanza?!
Kwa nini alijilipua kwa kiwango cha juu namna ile?!
Ilistaajabisha!
Masikini wa Mungu baada ya tukio lile wakubwa wakamwandika kwenye lile daftari liandikwalo kwa kalamu yenye wino mwekundu.
Mods, naomba mnisaidie isomeke NCHIMBI na siyo Chimbi.