Emmanuel Chimbi, ndoto iliyoiharibu ndoto yake yenyewe.

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
Kama lipo kosa analojilaumu Emma basi ni la yeye kuanzisha uasi kwa kile kilichotangazwa na na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wakati huo ndugu Jakaya .M. Kikwete kuhusu kukatwa kwa jina la bwana E. N. LOWASA kwenye kinyang'anyiro cha kuteuliwa kuwa mgombea wa u Rais kupitia CCM.

Kwa kawaida alichokifanya Nchimbi ki demokrasia hakukuwa na ubaya wowote lakini lijapo upande wa pili ni kosa kubwa la kudharau mamlaka iliyo juu yako na adhabu yake ni KUTOKUAMINIKA TENA na hilo ndilo limemuondelea sifa kuu ya yeye kuja kuwa kiongozi mkubwa ndani ya Taifa hili. Jambo hilo hata yeye mwenyewe alipo analitambua na huenda anaendelea kujutia hakika!

Kwa Nchi kama yetu hii ukiona unatupwa Ubalozini huku nyuma ulipata kuleta ukakasi kwenye jambo/mambo fulani kama alivyofanya Nchimbi tambua ndiwo mwisho wako wa kuwa mwana siasa utamaniye kuwa mkubwa hapo baadae.

Sielewi ni sababu ipi ilimfanya Nchimbi ajitokeze hadharani na kufanya kile alichokifanya ilhali wazi utaratibu wa namna ya kushugulikiwa kwa mtu wa aina ile aliyoichagua kufanya aliielewa vizuri!

Kwa nini hakujizuia kwanza?!

Kwa nini alijilipua kwa kiwango cha juu namna ile?!

Ilistaajabisha!

Masikini wa Mungu baada ya tukio lile wakubwa wakamwandika kwenye lile daftari liandikwalo kwa kalamu yenye wino mwekundu.

Mods, naomba mnisaidie isomeke NCHIMBI na siyo Chimbi.
 
Nakumbuka alikuwa na mwanamama sophia simba. Sema baadaye alifuta kauli.
Kitu pekee nilichogundua Tanzania hii, hata udanganywe una nguvu vipi ila huwezi kumshinda aliyekalia kiti cha uraisi. Maana it seems mwenye cheo cha uraisi anaweza kufanya chochote
 
Sasa Emmanuel Nchimbi naye alikua ana ndoto ya kuja kuwa Rais?? Kumbe Urais ni rahisi hivyoo??

Sitaki kuamini hata, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Prof Assad
Ndugai

Hawa wote wanajua nguvu ya Rais. Ijapokuwaa nao walikua na Nguvu kubwaa za kujimwambafy.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hilo la "kutupwa ubalozini" kuwa ni mwisho wa siasa siyo kweli. Mwinyi aliwahi kuwa balozi.
 
Huyo Chimbi ni yupi?Au unamfananisha na Nchimbi?Kama jina limekushinda,huyo mtu na simulizi unazotaka kutupatia zitakuwa za uhakika kweli?
 
Prof Assad
Ndugai

Hawa wote wanajua nguvu ya Rais. Ijapokuwaa nao walikua na Nguvu kubwaa za kujimwambafy.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Watu watakujaza kweli na wewe utajaa. Watasema ndugu yani wakikuzingua tuko nyuma yako. Yani kwa nguvu aliyokuwa nayo Lowasa sikuamini kama Magufuli angemzima vile hadi akaenda piga naye picha ikulu.
Mtu ambaye mimi huwa ananishangaza ni sumaye, sijui nia kwanini huwa anawaza kuwa ana influence kubwa tz hadi kutaka kugombea uraisi. Sumaye baada ya kuondoka kwemye uwaziri mkuu watu walishamsahau hata sasa baada ya mshikemshike wa awamu ya tano akarudi ccm hakuna anayemkumbuka.
 
Unamjua Dr. Nchimbi au unaropoka tu? Halafu toka lini shoga km wewe ukawa na moral authority ya kujua kiongozi bora wa nchi?
Namfahamu vizuri haswaaaa, afu punguza makasiriko yako, haya wee mwenye hiyo moral authority ya kujua kiongozi bora mbna haijafanya huyo Nchimbi kutimiza hiyo ndoto yake?

Umevurugwaa nn wee Poleeeeeeeh.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tz hii Rais anaweza kufanya chochote na kwa muda wowote atakao,
Katiba imempa madaraka makubwa mnoo.

JPM alisema wazi, kuna muhimili umejichimbia chini zaidi.
 
Walikuwa 3
1. Dr Emmanuel John Nchimbi
2. Sofia Simba
3. Alhaj Adamu Kimbisa (Mrangi)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…