Na kama Dunia tambara, langu lishatoboka Sina hata pa kulala,Nakesha kwa boka
Hii ni mistari iliyopo katika Wimbo wa SINA wa msanii wa Bongofleva,Harmonize.
Emmanuel Eboue Alicheza katika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya 2006, alikusanya mamilioni ya pesa katika miaka 7 aliyocheza katika EPL, hi kwenye nyumba nzuri a kuendesha magari ya kifahari Mambo yamebadilika sasa kwa beki huyo wa zamani wa Arsenal.
Kwa sasa anaishi kwa kuwakimbia watu wa mahakama, muda mwingine analala kwenye sakafu za nyumba za rafiki zake, anasafiri kwa basi na hata pia kufua kwa mikono yakekwa sababu hana mashine ya kufulia Akihojiwa na gazeti la Daily Mirror Eboue,34, amesema kuwa hali hiyo inamfanya mpaka atamani kujiua.
Ninataka Mungu anisaidie." Anasema Eboue, Pekee yeye anaweza kuyaondoa haya mawazo kichwani mwangu Eboue amepoteza utajiri wake wote kutokana na usimamizi mbaya pamoja na kuachana na mke wake ambapo ametengwa mbali na watoto wake Watoto wake wote watatu,hajaonana nao tangu mwezi juni.
Mtoto wake wa kiume,Mathis anacheza katika Academy ya Arsenal.
Baada ya kushindwa ka vita ya talaka, mahakama iliagiza mali zake zote ziende kwa mkewe, Aurelie ambaye ni raia wa Ubelgiji Pia anataraji kukabidhi kwa mkewe jumba lake la kifahari lililopo Enfield,London, endapo atashindwa kufanya hivyo jaji atasaini kuruhusu madalali waende kumtoa.
Eboue anasema kuwa, sasa hana pesa ya kuwalipa mawakili ili kufattilia mali zake. Nipo ndani ya nyumba lakini ninaogopa.
Kwa sababu sijui muda gani polisi watakuja, Muda mwingine ninazima taa kwa sababu sitaki wajue kama nipo ndani," Alisema Kutokana na kuwa na elimu ndogo,alikuwa anatuma karibia mshahara wote kwa mkewe. Na wakati wowote mkewe alikuwa akimtaka asaini hati (Document) yoyote alikuwa anasaini.
Mipango yake ya kurudi katika EPL iliota mbawa msimu uliopita, alisajiliwa na Sunderland lakini hakucheza hata mechi 1 kufuatia kufungiwa na Fl FA kutokana na kushindwa kumlipa wakala wake wa Zamani
Cc ws14