Emmanuel Mbasha Afunguka sakata la Gwajima katika Twitter

Emmanuel Mbasha Afunguka sakata la Gwajima katika Twitter

Tokea nazaliwa sijawahi kuona mtu mpumbavu kama huyu kaka. Kama ni kwely umetweet hivi na sio ufekelo Wa watu. Mr problem solved anahitaji watu kama wewe mbasha muambatane nae hawapeleke milembe. Ovyo zako mbasha. Ovyo Mara elfu nane huna akili we mpk akili zako hazina akili. One of the stupid people have ever seen in my life. Ur among them. Foolish en very foolish. Shwain to you Emmanuel mbasha.

duh.....binadamu kazi kweli kweli....hivi kweli inawezekana mtu ambaye humuoni ukamtukana hivi? If I may ask...kakukosea nini kaka wa Watu? It is his life. Get over it please. Kwa nini tunapenda Watu waishi maisha tunayotaka sisi? Iam afraid wewe unaweza kuwa na matatizo makubwa zaidi ya huyu kaka.
 
Watu wanapenda kujadili pumba,watu wameshasema kuwa hiyo ni photoshop siyo twit ya Mbasha.!
 
hamna hiyo account twitter - photoshop hiyo....
 
Aise mleta mada kabumba message , hii inaonekana kabisa sio screen shot
 
BACKANI.jpg


LICHA ya Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kukanusha mara zote kwamba, hahusiki na kusambaratika kwa ndoa ya Mwimba Injili Flora Mbasha na mumewe, Emmanuel Mbasha, lakini mume huyo ambaye amekuwa akimshutumu Gwajima ameibuka na jipya, Amani linakupa zaidi.Mwimba Injili Flora Mbasha na mumewe, Emmanuel Mbasha

Jipya aliloibuka nalo Mbasha ni kudai kuwa, msala uliompata Mchungaji Gwajima wa kumtolea maneno yenye kuudhi Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kadinali Pendo na kisha kuhojiwa polisi na kupata mshtuko, kuzimia hadi kulazwa hospitali ni malipo ya Mungu kwake kutokana na kilio chake.
ATUMIA DAKIKA 15
Akizungumza na Amani kwa njia ya simu kwa dakika 15 juzi, Mbasha alisema: "Ile hali (kupoteza fahamu) ya Gwajima ni malipo. Mimi nilishasema jamani, mtu akikutendea ubaya malipo ni hapahapa duniani, hakuna kwingine.

"Mimi ndoa yangu haipo, mke wangu anajua yeye anavyoishi. Kwa hivyo mimi nimekuwa nikiishi kwa manung'uniko kila siku, unadhani nini kitatokea kwake?"

AMTAKA AKAMWOMBE MSAMAHA
Mbasha alikwenda mbele zaidi kwa kutoa tamko na agizo kwa mchungaji huyo kwa kusema:
"Tena namwomba Mungu ampe afya Gwajima, akitoka hospitali alikolazwa (TMJ, Dar) anitafute kuniomba msamaha.
"Ni vyema na itakuwa vyema zaidi akinitafuta na kuniomba msamaha ili kila mmoja aishi kwa amani. Mimi nisiwe na kinyongo na yeye na wala yeye asiwe na kinyongo na mimi."

KUHUSU ALICHOKIONGEA GWAJIMA
Mbasha hakumalizia hapo, alipoulizwa kama kauli ya Gwajima iliyosababisha mtafaruku ilikuwa sawasawa au la! Mbasha alisema:

"Hilo atajua yeye mwenyewe na Mungu wake, mimi sijui. Ila ninachojua mimi ni kitu kimoja tu, kwamba Mungu amenilipia basi, sasa aniombe msamaha."

MCHUNGAJI WA GWAJIMA ANENA

Naye mchungaji mmoja wa kanisa la Gwajima alipopatikana kwa simu na kuulizwa kuhusu madai ya Mbasha, alisema: "Yule hajui maandiko sawasawa. Hakuna uhusiano wowote kati ya kilichompata mchungaji wangu na hisia zake kuhusu mkewe Flora.

"Gwajima na Flora hawana uhusiano wowote usiofaa. Sasa yeye anaposema kalipiwa, kalipiwa kitu gani? Mungu anaweza kulipa jambo la hisia?"

WANACHOAMINI WENGINE

Mbali na Mbasha, baadhi ya wasomaji wa gazeti hili walisema kwamba, wanamwamini Mchungaji Gwajima ni miongoni mwa watumishi wa Mungu waliojaliwa hekima hivyo kauli aliyoitoa yenye maneno yenye kuudhi huenda ulikuwa mpango maalum wa roho chafu aseme yale ili yamkute yaliyomkuta na kujifunza kitu.

"Gwajima ana hekima bwana. Ni Mchungaji mwenye kujitambua, yale maneno aliyomsema Askofu Pengo lazima ni mpango wa roho chafu, pale Gwajima ana kitu cha kujifunza.

"Mimi sisemi kama alichokutananacho ni kwa sababu ya ‘maombi' ya Mbasha kwa Mungu wake, ila nasema Gwajima ana kitu cha kujifunza kwa matamshi yake na mazingira ya utumishi pia," alisema Johnson Mwaduma, mkazi wa Mwananyamala, Dar.

WITO KWA SERIKALI

Kufuatia manenomaneno ya chini kwa chini kwamba, huenda serikali ikalifungia kanisa lake lililopo Kawe jijini Dar, baadhi ya wasomaji waliitaka serikali kutofikiria kufanya hivyo kwani Gwajima ni mchungaji mwenye waumini wengi sana nchini.

"Yule ana makanisa nchi nzima, sasa serikali ikisema ilifungie kanisa lake ina maana waumini maelfu kwa maelfu watarudi nyuma kiroho na matokeo yake ni kuanza kupata watu watenda maovu.

"Lazima ikumbukwe kwamba, mchungaji anapowahubiria waumini wake kutenda mema, kuacha dhambi pia anaisaidia serikali katika kupambana na maovu.

"Halafu yule Gwajima mwenyewe ni mchungaji wa kweli, ana imani, ana nguvu ya kiroho, amesaidia wengi kimwili na kiroho pia. Anatakiwa kuendelea kutiwa moyo kwa vile ni mtu mwongofu," alisema Simon Salele, mkazi wa Sinza D, Dar es Salaam.

TUJIKUMBUSHE

Wiki mbili zilizopita, kwenye Viwanja vya Tanganyika Perkers ambako kuna kanisa, Gwajima alitoa mahubiri yaliyolenga kumshutumu Kadinali Pengo kwa kitendo chake cha kwenda kinyume na maazimio ya Baraza la Maaskofu Tanzania kuhusu msimamo wao wa Mahakama ya Kadhi nchini.

Hali hiyo ilimfanya Gwajima kuitwa Polisi Kituo cha Kati, Dar na kuhojiwa. Akiwa katika mahojiano, ghafla alisikia kizunguzungu, akaanguka na kupoteza fahamu. alikimbizwa katika Hospitali ya Polisi Baracks kisha Hospitali ya TMJ, Dar kwa matibabu zaidi.

Juzi, Gwajima aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo lakini akachukuliwa hadi Kituo cha Polisi

CHANZO: GPL
 

Attachments

  • Gwajima.jpg
    Gwajima.jpg
    67.8 KB · Views: 228
ivi ilikuwaje Gwajima akaugua hadi kulazwa TMJ?
unajua kuna jambo kumbwa sana ambaalo usipokaa makini litakuagusha nalo ni kujizidishia hekima
mhubiri ameyasema haya sijui kwann Gwajima hakulikumbuka hili

hata kama Pengo kakosea yeye sio kazi yake kumuonya na kama alipewa mafunuo na Mungu ili amuonye basi Mungu angempa na mazingira mazuri ya kumuonya na sio kumdhalilisha mpakwa mafuta ya Mungu kama alivyo fanya.
au
Gwajima arudi asome kisa cha Sauli na Daudi. ingawa mara nyingi daudi alijikuta akitegwa na roho ya kutaka kumuua sauli lkn Daudi alipingana na ile roho na alifika mahali akamwambia sauli waziwazi. daudi alisema hata pale mtumish wake alipotaka kumuua aliwmambia usimguse mpakwa mafuta wa Bwana.

kumbuka daudi alidiriki kumuua aliyemletea habari za kifo cha sauli na mwanawe kwani aliamini kabsa ile haikuwa kazi yake. sasa Gwajima kwanza kadondoka mbele ya askari sijui ni presha ama ni nini. Mpakwa mafuta wa Bwana atabaki kuwa mpakwa mafuta tu ata kama wewe utakuja na kelele zako nyingii za kuijua bibo nk.

my take gwajima amwombe msamaha PENGO
 
Shigongo naweeeee... mscheeeeew yani bonge la opportunist mambo ya wenzio unayavalia kibwaya subiri nawewe uwakosee wakuu 1 day... watakupekua hadi usukuma wako kama ni halali au wa kuchovya
 
ivi ilikuwaje Gwajima akaugua hadi kulazwa TMJ?
unajua kuna jambo kumbwa sana ambaalo usipokaa makini litakuagusha nalo ni kujizidishia hekima
mhubiri ameyasema haya sijui kwann Gwajima hakulikumbuka hili

hata kama Pengo kakosea yeye sio kazi yake kumuonya na kama alipewa mafunuo na Mungu ili amuonye basi Mungu angempa na mazingira mazuri ya kumuonya na sio kumdhalilisha mpakwa mafuta ya Mungu kama alivyo fanya.
au
Gwajima arudi asome kisa cha Sauli na Daudi. ingawa mara nyingi daudi alijikuta akitegwa na roho ya kutaka kumuua sauli lkn Daudi alipingana na ile roho na alifika mahali akamwambia sauli waziwazi. daudi alisema hata pale mtumish wake alipotaka kumuua aliwmambia usimguse mpakwa mafuta wa Bwana.

kumbuka daudi alidiriki kumuua aliyemletea habari za kifo cha sauli na mwanawe kwani aliamini kabsa ile haikuwa kazi yake. sasa Gwajima kwanza kadondoka mbele ya askari sijui ni presha ama ni nini. Mpakwa mafuta wa Bwana atabaki kuwa mpakwa mafuta tu ata kama wewe utakuja na kelele zako nyingii za kuijua bibo nk.

my take gwajima amwombe msamaha PENGO


Mdomo uliponza kichwa....huyo Gwajima alikosea hakika.
 
Wabongo bwana kila jambo wao ni kuchuriana tu...

Muone huyu bweg.e naye yaani akili yake inaanza kumuaminisha kuwa yaliyotokea kwa Gwajima ni kisasi cha Mungu wake...
 
Wabongo bwana kila jambo wao ni kuchuriana tu...

Muone huyu ----- naye yaani akili yake inaanza kumuaminisha kuwa yaliyotokea kwa Gwajima ni kisasi cha Mungu wake...

yaani wewe umenena kweli,
hivi unafikiri mpaka Mungu akulipie kisasi ni kazi ndogo? yeye Mbasha anaousafi gani hadi Mungu amlipie kisasi?
ukweli utabaki kwamba Gwajima kategwa na mdomo wake na sio kisasi na hili ni kosa hasa pale mtu unapotaka kujizidishia hekima ukasahau kwamba hata wenzio wameskia na wamekaa kimya manake ni bora kuwa mjinga machoni pa watu lkn mbele za Mungu ukawa mwenye hekima.

simshangai Gwajima kwa kuropoka kwake manake aliwah kusema amefufua misukule ambayo mpaka leo sijawah kuona aliyefufuka hata mmoja akipita njian licha ya kwamba ana mwaka karibia wa 10 sasa na hilo kanisa lake
 
Mbasha na yeye anazidi kuweweseka huwezi kula kuku na mayai yake na huwezi kula bata na Utumbo wake,yeye kaiharibu ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe harafu anasingizia Gwajima,Na kwa ujinga anasema Mungu kamlipa kwani mke wake karudi????nijuavyo mimi Mungu hamlipi mtu hivyo labda Mungu Mwingine.
 
Wacha wee ngoja niagize popcorn nichek vizuri
 
Hebu wanajanvi naomba msaidie mme wa Frola mbasha, anajisikiaje baada ya Gwajima kujaribu kujipima ubavu na mtu wa Mungu Pengo. bila shaka mbasha sasa hasira zimepungua na anamuonea huruma tajiri huyu gwajima mbali na kumtusua mke wake. au BAVICHA mnalionaje hili la kamanda mwenzenu Gwajima mna la kuongezea karibuni makamanda wa mtandaoni.
 
UnaHamUuu ya MuHoGo wewe BiLa shAka. kuwA maKini utAfuMuLiWaaa mAriNdaaaa na haO bAvIchAa.
 
Seriously!!! A Great Thinker?! Mods hivi hii ni habari ya Siasa? Hata kama sio ya siasa, muktadha wake una manufaa kwa jamii? Naomba mfanye kazi yenu.
 
Seriously!!! A Great Thinker?! Mods hivi hii ni habari ya Siasa? Hata kama sio ya siasa, muktadha wake una manufaa kwa jamii? Naomba mfanye kazi yenu.
usihofu kuanzia kesho tutaanza kumsifia baba yako Mbowe, kwa leo vumilia. tunarekebisha tabia ya wezi wa wake za watu ili wanasiasa wetu wawe makini hivyo tulia hivyohiyvo endelea kunywa mnazi wako taratibu.
 
Back
Top Bottom