LGE2024 Emmanuel Nchimbi: Tuna Mtaji wa Imani ya Watanzania

LGE2024 Emmanuel Nchimbi: Tuna Mtaji wa Imani ya Watanzania

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Political Jurist

Senior Member
Joined
Sep 6, 2021
Posts
143
Reaction score
120
TUNA MTAJI WA IMANI YA WATANZANIA: NCHIMBI

Azindua kampeni Mwanza akitamba na takwimu za kura za uhakika

Awasihi wanaCCM kila mmoja kutafuta kura 10 kwa ajili ya ushindi wa kishindo

Ahamasisha kampeni za nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu, isiachwe kura hata moja, wakiwemo wapinzani

Awataka washindi kuwatumikia Watanzania kwa kupinga dhuluma na rushwa


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema CCM inaingia kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa kikiwa na imani kubwa ya Watanzania kutokana na uimara wa chama na uongozi wa Mwenyekiti wake, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema kuwa uimara wa CCM unatokana na wingi na umakini wa wanachama wake, akitoa takwimu jinsi wanachama wapatao milioni 8 wa CCM walivyojitokeza kupiga kura wakati wa mchakato wa ndani ya chama hicho kupata wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Balozi Nchimbi amesema mtaji wa imani ya Watanzania, utumishi wa CCM kupitia sera zake, na uongozi makini unakipatia chama hicho uhakika wa ushindi mkubwa wa kishindo katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.

Katibu Mkuu huyo wa CCM aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni za CCM kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mkoa wa Mwanza, uliofanyika katika Viwanja vya Furahisha, jijini Mwanza, leo tarehe 27 Novemba 2024.

Katika kujihakikishia ushindi huo wa kishindo, Balozi Nchimbi alisisitiza kampeni za kuomba kura ziwalenge hata wanachama na viongozi wa vyama vya upinzani, ili kuhakikisha kila kura inapatikana kwa ajili ya CCM, akiwahamasisha kupiga kampeni “nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu” nchi nzima.

“Pamoja na uhakika wa kura, msiridhike na ushindi. Twendeni nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu. Tusiache kura hata moja. Kila mwanachama atafute kura 10. Hata wa vyama vya upinzani, wawe ACT, NCCR, Chadema, na wote, watatupigia kura. Tumalizeni huu mchezo kwa kuipatia CCM ushindi mkubwa wa kishindo.

“Wajibu wetu ni kuwakumbusha tu Watanzania kazi kubwa ambayo CCM imeendelea kufanya katika kutoa uongozi wa nchi hii. Uhakika wa kesho ya Tanzania uko CCM. Watanzania wana imani kubwa na CCM kila wanapofikiria maendeleo, umoja wa nchi yetu, utaifa wetu, amani na utulivu. Tunataka wagombea wetu mtakapochaguliwa mkalinde heshima na imani hii ya Watanzania kwa kuwatumikia vizuri, mkijiepusha na dhuluma na rushwa,” alisema Balozi Nchimbi.

Aidha, akisisitiza kuhusu uimara wa CCM, Balozi Nchimbi alisema CCM ndiyo chama pekee ambacho wanachama wake, kwa mamilioni, walijitokeza kushiriki mchakato wa ndani wa kupata wagombea, hasa kupitia kura za maoni. Hii ndiyo sababu kimesimamisha wagombea maeneo yote nchi nzima katika uchaguzi huo, kwa kuwa kimeenea nchi nzima, tofauti na vyama vingine vya upinzani.

#Ends
 

Attachments

  • IMG-20241120-WA0759.jpg
    IMG-20241120-WA0759.jpg
    773.2 KB · Views: 4
  • IMG-20241120-WA1022.jpg
    IMG-20241120-WA1022.jpg
    666.1 KB · Views: 5
Balozi Nchimbi amesema mtaji wa imani ya Watanzania, utumishi wa CCM kupitia sera zake, na uongozi makini unakipatia chama hicho uhakika wa ushindi mkubwa wa kishindo katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Duh,
Watanzania na unafiki ni kama samaki na maji.

Anavyoongea huyo jamaa utafikiri this time wananchi watapiga kura na kuchagua viongozi wanaowataka kwa uhuru na haki bila figisu, wizi, dhuluma na uovu wa kila namna..

View: https://youtube.com/watch?v=H77NTG71YW0&si=3CZY4C8eLW_FkT9J
 
Mmengejua watanzania walivyowachoka wala msingejilisha upepo. Halafu kama mna mtaji huo wa watanzania kwanini mnaihujumu chadema?
 
Mmengejua watanzania walivyowachoka wala msingejilisha upepo. Halafu kama mna mtaji huo wa watanzania kwanini mnaihujumu chadema?
Wanajinadi kuaminika ila kutwa kuibinya CHADEMA. Kila wanalopanga utaskia tuna intelijensia CHADEMA wanataka kufanya jambo flani la taharuki😂
 
Mmengejua watanzania walivyowachoka wala msingejilisha upepo. Halafu kama mna mtaji huo wa watanzania kwanini mnaihujumu chadema?
Hapo sasa, chama kinachotegemea mapingamizi kutangazwa washindi kwa shuruti.
 
Hapo sasa, chama kinachotegemea mapingamizi kutangazwa washindi kwa shuruti.
Hovyo kabisa hili lichama waseme tu mtaji wao ni wawajinga na vibibi ambavyo ni less informed.
 
Back
Top Bottom